Mapingamizi yatawala Kinondoni, Mwenyekiti wa chama amuwekea pingamizi mgombea wake

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Dar es Salaam. Msimamizi msaidizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Latifa Almas amesema wagombea watatu katika uchaguzi huo wamewekewa pingamizi.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 22, 2018, Latifa amegoma kuweka wazi aina ya mapingamizi akitaka watafutwe wahusika

Amewataja waliowekewa pingamizi kuwa ni

Maulid Mtulia (CCM), Salum Mwalimu (Chadema) na Johnson Mwangosi (Sau).

Amesema watatu hao tayari wameshachukua barua zao za utetezi na kujieleza kuhusu mapingamizi hayo na kutakiwa kuzirejesha haraka iwezekanavyo.

Amesema pingamizi la kwanza ni lile la Mwalimu alilomuwekea Mtulia, la pili ni la Mtulia kumwekea Mwangosi na la mwisho ni la mgombea wa CUF, Rajabu Salum Juma kumuwekea Mwalimu.

"Wagombea wote wameshapata taarifa na tayari wameshachukua barua (fomu) zao za kujieleza wanazotakiwa kuzijaza na kuzirejesha haraka iwezekanavyo. Kama walioweka mapingamizi wasiporidhika na maelezo yao wanaweza kukata rufaa NEC (Tume ya Uchaguzi),” amesema Latifa.

Amesema pingamizi la mwenyekiti wa chama cha Democratic (DP) Mkoa wa Dar es Salaam, David Berege dhidi ya mgombea wa chama hicho, Mary Mpangala limetupiliwa mbali.

"Berege alimpinga mgombea wake wa nafasi wa ubunge jambo ambalo ni kinyume cha sheria kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na mamlaka husika na tumelitupilia mbali baada ya kulipitia," amesema Latifa.

CHANZO: Mwananchi
 
hizi sanaa na maigizo, havita tutoa katika umasikini bali vita tukalibisha huko
 
Mwisho wa siku sisi wana kinondoni hatumtaki Mtulia hata kidogo, katuchefua sana huyu jamaa

Ni kweli kabisa hili jamaa halifai kabisa nililichagua kwa heshima ya ukawa na kutoipenda kwangu CCM lakini likaja kufanya upumbavu wa ajabu kabisa.. Nitasafiri kutoka huku mbali kuja kupiga kura kwa Salumu Mwalimu ili nionyeshe chuki kwa huyu jamaa..
 
Duh ! Hii nchi ya ovyo sana kila kitu ovyo watu awapendani wanasiasa. Awapendani sijui tutajenga vipi nchi yetu
 
hizi pesa mnazotumia kufanya chaguzi za kima***** mngejenga miundombinu SHITHOLE COUNTRY
ndo maana mpaka sasa huko vijijini hakuna maji ya uhakika wanadamu wanakunywa maji nambwa mwitu na ngombe + vinyesi vyao

NONESENSE
 
Ni kweli kabisa hili jamaa halifai kabisa nililichagua kwa heshima ya ukawa na kutoipenda kwangu CCM lakini likaja kufanya upumbavu wa ajabu kabisa.. Nitasafiri kutoka huku mbali kuja kupiga kura kwa Salumu Mwalimu ili nionyeshe chuki kwa huyu jamaa..
:eek::oops::oops: utashangaa rufaa dhidi yake imekubaliwa...xo hautaweza kuja
 
Mtulia anashinda asubuhi na mapema. Tatizo la kinondoni 2015 halikuwa CCM bali Idd Azzan alikaa muda mrefu kwenye ubunge.
Chadema, CUF na wengine wanapoteza muda wao. Sisi wanakinondoni tumekubaliana kumchagua Mtulia aweze kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM.
 
Ila siku zote shetani ana mbinu za hali ya juu za hujuma dhidi ya binadamu. Tusali na kufunga ili Mola wetu awe nasi.
 
Mtulia anashinda asubuhi na mapema. Tatizo la kinondoni 2015 halikuwa CCM bali Idd Azzan alikaa muda mrefu kwenye ubunge.
Chadema, CUF na wengine wanapoteza muda wao. Sisi wanakinondoni tumekubaliana kumchagua Mtulia aweze kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Umekubaliana wewe na ndugu zako upande wa kike labda
 
Umekubaliana wewe na ndugu zako upande wa kike labda
Hasira ya nini sasa? Naongea kwa niaba ya wanakinondoni, tumekubaliana wanakinondoni wote kumchagua Mtulia. Kama hukupata ujumbe huu basi ninakupatia. Kura zote kwa Mtulia.
 
Back
Top Bottom