Uchaguzi 2020 Mapingamizi halali kisheria dhidi ya mgombea nafasi ya Urais

Matojo Cosatta

JF-Expert Member
Jul 28, 2017
234
390
MAPINGAMIZI HALALI KISHERIA DHIDI YA MGOMBEA NAFASI YA URAIS.

Wiki ijayo tarehe 26 August, 2020 itakuwa ni siku ya wagombea kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mapingamizi halali kisheria anayoweza kuwekewa mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa masharti ya ya Kifungu cha 35 D na 40 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 yakisomeka kwa pamoja na (read in tendem with) masharti ya Kanuni ya 39 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ni haya yafuatayo;

(1) Mgombea Urais sio raia wa Tanzania.

(2) Mgombea Urais hajafikisha umri wa miaka 40.

(3) Mgombea Urais hajui kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza.

(4) Mgombea Urais sio mwanachama wa chama cha siasa.

(5) Mgombea Urais hajadhaminiwa na chama cha siasa kugombea.

(6) Mgombea Urais amekutwa na hatia ya kosa la jinai la kukwepa kodi katika kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya Uchaguzi.

(7) Mgombea Urais hajadhaminiwa na wapiga kura 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 kutoka Zanzibar.

(8) Mgombea Urais hajadhaminiwa na idadi ya kutosha ya wapiga kura.

(9) Mgombea Urais hakulipa dhamana ya Tshs 1, 000, 000/=

(10) Mgombea Urais hakuwasilisha au hakuambatinisha picha kwenye Fomu ya Uteuzi.

(11) Mgombea Urais ameshindwa kuambatanisha Tangazo la Kisheria (statutory declaration) kwenye Fomu ya uteuzi ambalo limesainiwa na mgombea na limefanywa mbele ya Jaji kudhibitisha kuwa mgombea anayo nia na anazo sifa za kugombea Urais.

(12) Mgombea Urais ameshindwa kuweka wazi pesa ambazo atazitumia katika uchaguzi.

(13) Mgombea Urais hakusaini kukubali kutii Maadili ya Uchaguzi.

(14) Mgombea Urais hakujaza au hakurudisha Fomu ya Uteuzi kwa Tume ya Taifa Uchaguzi kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

(15) Mgombea Urais amefanya makosa ambayo yamezuhiwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.

(16) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, mgombea hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar zilizoainishwa na Katiba husika.

(17) Taarifa ambazo mgombea Urais amewasilisha kwa Tume ya Taifa uchaguzi hazijitoshelezi kumtambua mgombea.

(18) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoainishwa na Katiba.

Haya ndo mapingamizi 18 pekee ambayo anaweza kuwekewa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo.
 
MATAGA,Lissu anaingia wapi hapo kwa hoja ya kufanya kampeni kabla ya wakati?

Umefanya jambo la maana sana kuleta hii habari.

Hapa pia anajiuliza,mtu huyu ambae hajapitishwa na Tume, anaitwaje mgombea uraisi?

Sasa kuna maana gani ya kumuwekea pingamizi mtu asigombea na hapo hapo tayari anatambulika/anatajwa kama mgombea?

Je,tumekosa msamiati wa kiswahili katika hili au mimi ndio sielewi?
 
Yaani CCM nawahurumia sana

Na mwaka huu tume haitakubali kuwabeba upepo ukiwa mbaya yaani mtapata tabu Sana

Lissu atapitishwa tena mapema Sana hakuna mtu ambaye haipendi Tanzania ambaye atakubali ujinga kuchafua nchi.

Sio tume sio watu wa usalama mwaka huu watu wanasimama na umma.
 
MATAGA,Lissu anaingia wapi hapo?

Umefanya jambo la maana sana kuleta hii habari.
Mkuu

Election Commision ipo ndani ya mifuko ya mwenye enzi kuu duniani....

Itapigwa simu au text msg atakatwa mtu.....ni lazima...

Dictator yeyote duniani ni muoga kupita maelezo kuona kwenye sanduku la kura kuna jina la worthy challenger.....

Taasisi zote zipo held by the balls na mwenye enzi duniani na mbinguni....

Utaona vituko sana...just wait and seee!

Electoral Commision itakua weaponized to delete the threatening candidate to the dictator.....
 
MATAGA,Lissu anaingia wapi hapo kwa hoja ya kufanya kampeni kabla ya wakati?

Umefanya jambo la maana sana kuleta hii habari.

Hapa pia anajiuliza,mtu huyu ambae hajapitishwa na Tume, anaitwaje mgombea uraisi?

Kuanza Kampeini mapema (pre-mature election campaign) sio kosa chini ya sheria za uchaguzi za Tanzania. Kuanza Kampeini mapema hakumuondolei mtu sifa za kugombea Urais katika Sheria za Uchaguzi za Tanzania.

Kuanza Kampeini mapema ni kosa chini ya sheria za ndani za CCM lakini sio kwenye sheria za nchi.
 
CCM watakuloga, ngoja johnthebaptist aende kwa Sheikh Sharif majini!
 
Mapingamizi namba 4 na 5 yanavunja misingi ya haki ya Watanzania kuchaguliwa uongozi.

Nafikiri hata Ripoti ya Jaji Nyalali ilishauri tuondoe sharti la wagombea kuwa wanachama wa vyama vya siasa.
Ni kazi ya Bunge kupitia constituent assembly wafanyie marekebisho katiba na kufuta ibara inayotoa hilo sharti.
 
Mkuu

Election Commision ipo ndani ya mifuko ya mwenye enzi kuu duniani....

Itapigwa simu au text msg atakatwa mtu.....ni lazima...

Dictator yeyote duniani ni muoga kupita maelezo kuona kwenye sanduku la kura kuna jina la worthy challenger.....

Taasisi zote zipo held by the balls na mwenye enzi duniani na mbinguni....

Utaona vituko sana...just wait and seee!

Electoral Commision itakua weaponized to delete the threatening candidate to the dictator.....
Tanzania itaingia kwenye machafuko ambayo hayajawahi toke tangu dunia imeumbwa
 
MATAGA,Lissu anaingia wapi hapo kwa hoja ya kufanya kampeni kabla ya wakati?

Umefanya jambo la maana sana kuleta hii habari.

Hapa pia anajiuliza,mtu huyu ambae hajapitishwa na Tume, anaitwaje mgombea uraisi?

Sasa kuna maana gani ya kumuwekea pingamizi mtu asigombea na hapo hapo tayari anatambulika/anatajwa kama mgombea?

Je,tumekosa msamiati wa kiswahili katika hili au mimi ndio sielewi?
Ukiangalia hapo mbona kuna kanuni nyingi tu ambazo zinamgusa mtu kabla hajateuliwa na tume.
 
Mapingamizi namba 4 na 5 yanavunja misingi ya haki ya Watanzania kuchaguliwa uongozi.

Nafikiri hata Ripoti ya Jaji Nyalali ilishauri tuondoe sharti la wagombea kuwa wanachama wa vyama vya siasa.

Mtikila alijaribu mara 3 kupigania haki ya Mgombea binafsi mahakamani lakini mwishowe alishindwa kesi . Mtikala alishinda kesi katika Mahakama Kuu mara 2 yaani mwaka 1993 kwa Jaji Lugakingira na 2006 kwa majaji watatu (3) wakina Mihayo na wenzake, hatahivyo, alishindwa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Attorney General Vs Mtikila, Civil Appeal No. 45 of 2019.
 
Mapingamizi namba 4 na 5 yanavunja misingi ya haki ya Watanzania kuchaguliwa uongozi.

Nafikiri hata Ripoti ya Jaji Nyalali ilishauri tuondoe sharti la wagombea kuwa wanachama wa vyama vya siasa.
Na hii inasababisha wagombea wenye vipaji vya uongozi ktk jamii husika kukoswa nafasi ya kugombea kwa sbb ya ukilitimba uliomo ndani ya vyama vya siasa vyote.
Rasimu ya katiba ya jaji Warioba inapendekeza kuwe na mgombea binafsi pia.
 
Mkuu

Election Commision ipo ndani ya mifuko ya mwenye enzi kuu duniani....

Itapigwa simu au text msg atakatwa mtu.....ni lazima...

Dictator yeyote duniani ni muoga kupita maelezo kuona kwenye sanduku la kura kuna jina la worthy challenger.....

Taasisi zote zipo held by the balls na mwenye enzi duniani na mbinguni....

Utaona vituko sana...just wait and seee!

Electoral Commision itakua weaponized to delete the threatening candidate to the dictator.....
Ccm ni utopolo,mtu mwenye akili timamu huwezi kutamani kuongozwa na miaka mitano mingine
 
MATAGA,Lissu anaingia wapi hapo kwa hoja ya kufanya kampeni kabla ya wakati?

Umefanya jambo la maana sana kuleta hii habari.

Hapa pia anajiuliza,mtu huyu ambae hajapitishwa na Tume, anaitwaje mgombea uraisi?

Sasa kuna maana gani ya kumuwekea pingamizi mtu asigombea na hapo hapo tayari anatambulika/anatajwa kama mgombea?

Je,tumekosa msamiati wa kiswahili katika hili au mimi ndio sielewi?
11,12, & 13
 
Back
Top Bottom