Mapinduzi!!

mzee wa kijiwe

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
936
1,000
Haya ni mapinduzi!!!
Ni mapinduzi ya wazi, kimya kimya na ni ya kimkakati,tena mkakati maalumu ulioasisiwa na wazalendo wa nchi hii!
Fursa pekee waliyokuwa wanaisubiri kwa miaka mingi ni kufanyika kwa kosa la kihistoria la kumpitisha mtu asiyetokana na fikra zao japo yumo kwenye mfumo wao,huyu sii mwingine bali ni Rais John Pombe Magufuli.
Anafanya mapinduzi ndani ya chama cha mapinduzi, jambo ambalo ni gumu kuliasisi japo sasa linatokea.
Anafanya mapinduzi ya uendeshaji wa mambo ndani ya serikali kitu ambacho sii rahisi kutokea haswa kwa serikali zetu za kiafrika.
Haya ni mapinduzi tena makubwa, ni zaidi ya kuwa na katiba mpya japo atahitajika kuhitimisha na hili la katiba mpya!!
Mapinduzi haya yanatikisa taasisi zote kuanzia zile za kijamii,siasa hata dini.
Taratibu tunawaona Kina Butiku wakiwa nyuma ya mapinduzi haya, bila shaka hiki ni kiashirio kuwa Mwl Nyerere na falsafa zake ndicho kichocheo kikubwa chá mapinduzi haya. Namwona Jaji mstaafu Warioba akicheka Kila hatua moja ya kimapinduzi inapochukuliwa, hii ni ishara nzuri haswa kwa wale ambao hawajasahau wimbo Wa katiba Mpya.

Kwa mbali naona wale waliobatizwa jina na kuitwa wapinzani katika nchi hii wanajiuliza je huyu ni mwenzetu? Je anaaminika? Naona wengi wanaanza kuvutiwa na Matendo Yake, wanaukumbuka wimbo Wa msanii mmoja, "mtawatambua kwa Matendo yao" na kweli sii kwa maneno Yao.
Natabiri mapinduzi makubwa haya ndiyo majibu ya maombi ya watanzania waliyoyaomba kwa miaka mingi sana. Kutatokea kizazi kipya ndani ya mifumo yote ambacho kitavaa sura hii ya ujasiri Kila mahali. Nafikiri mapinduzi haya yataingia makanisani, misikitini, kwenye vyama!
Nategemea sasa watu watajiunga kwenye mapinduzi haya ambayo yatapelekea mapinduzi ya Viwanda Tanzânia.
Tukumbuke mapinduzi haya hayajaletwa na chama hivyo hayataongozwa na chama. Vyama vimetugawa haya mapinduzi yatuunganishe.

Mimi ni mwana mapinduzi, wewe vipi?
BISHOP PETER JOHN
0715829576
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom