Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Du!h Historia iliniacha mashariki na iko magharibi sasa.

Kumbe Karume aliuliwa?
duh, hao watu hawapo siku hizi eh.
 
Kila mtu mtaalamu wa haya mapinduzi kumbe!

Mkuu tupe source tafadhali
 
Si kweli, John Okello hakuwa na tamaa ya madaraka kwani ukisoma kitabu cha Ghassany utaona ndio sababu ya kupigwa marufuku asirudi tena visiwani.

Karume baada ya kuchukua nchi Okello akawa na tamaa ya yeye kuwa rais na Karume akataarifiwa kuhusu hili na akaamuru achunguzwe mambo yote anayofanya. Baada ya muda Karume aliletewa tape aliyorekodiwa Okello akimkashifu Karume kuwa hatuwezi kutawaliwa na mtu ambae hajasoma na mbumbumbu huku watu wasomi kama sisi tupo ambao tunastahili kuwa rais wa nchi hii.

Baada ya kusikia maneno hayo Karume akamtoa kiujanja kuwa amempa livu aende dar kupumzika. Alivyofika Dar Karume akampigia simu Nyerere na kumuambia kuwa Okello asikanyage tena visiwani znz. Nyerere akamtia kizuizini na baada ya muda alimpeleka Kenya na baada ya muda mfupi Kenya nao wakamrudisha kwao Uganda na alipofika huko aliishia Gerezani.
 
Huyu mtu aitwaye John Okello alikuwa ni mercenary, Kwa Kiswahili sanifu anaitwa Mamruki...! Sasa ni nchi gani ambayo imetumia majeshi ya kimamruki kupindua nchi kisha wakaitwa mashujaa!?

Ninavyojuwa mimi mamruki wote ukodiwa kwa kazi chafu yoyote na wakishalipwa biashara inakuwa imekwisha, sasa John Okello yeye alitaka kulowea kabisa na kutaka kutawala, sasa aliposhtukiwa ndio kama hayo yaliomkuta.
 
Kinachotakiwa ni kuwaenzi wale wanamapinduzi wa kweli, wale waliopigana vita na mkoloni, mfano vita vya majimaji vilipoteza mashujaa wasio pungua 75,000.

Mashujaa wa kweli wa kuwaenzi ni wale waliopigana vita dhidi ya mkoloni, wakiwaongoza wananchi wao kishujaa, japo walikuwa na zana duni. Machief kama Chief wa Wayao Chief Mataka, Chief Chabruma, Mangi Mandara, Mangi Sina, Chief Mkwawa, Kinjikitile Ngwale, Wakina Isikie na wakuu wote walioshiriki kwa hali na mali kujaribu kupigania uhuru wa kweli wa Mwafrika, na si kuwakumbuka vibaraka mamhuruki wakina Okello.

Labda akumbukwe tu, kwa ukatili wake, kwani jamaa alikuwa chinja chinja kweli.
 
Asante kwa kutukumbusha historia, though wamefuta kabisa historia hizi, ndo maana naye aliuawa kwa roho mbaya.
 
Yawezekana karume alikua katiri sana ndo kisa cha kumfukuza Okello japo ndo alifanya mapinduzi ya kuondoa utawala wa kisultan.niambieni Karume kifo chake kilikuaje?
 
Kuna mengi yanasemwa sana humu kuhusu John Okello na wengi wanamzungumzia kutokana na wao kusoma articles zinazozungumzia mapinduzi ya Zanzibar

Lakini nimebahatika kusoma CHAPER 9 ya kitabu cha (Mlango wa Tisa: John Okello ) Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia ni matokeo ya utafiti na ufuatiliaji wa kina wa Dkt. Harith Ghassany ambao ameufanya kwa zaidi ya muongo mmoja.

Sasa kitabu kiko tayari na ndani yake muna maelezo ya kinagaubaga juu ya nini kilitokea, vipi kilitokea, wapi kilitokea, kwa nini kilitokea na, juu ya yote, nani hasa aliyekifanya kitokee na kwa malengo gani. Kinaelezea upya historia ya Zanzibar , hasa ya tukio lile la Mapinduzi ya 1964, kwa kutumia mwanga na maneno ya wahusika wenyewe na nyaraka za kimataifa.

I'm sure GREAT THINKERS mtachukua muda kusoma huu ukurasa wa huyu bwana aliyeamua kujiita ''FIELD MARSHALL''

Lakini more interesting hebu sikiliza haya mahojiano:

Sauti:Mjadala wa meza ya duara – Mapinduzi | MZALENDO.NET

Sijui kwa nini hiki kitabu kiko free online lakini nadhani itakuwa ilikuwa ni PhD thesis yake kule HARVARD. Either way hiki kitabu kilichojaa nondo za kumwaga kinaweza kuwa blessing in disguise kwa watu.

1. Kuna habari kuwa kuna watu (Serikalini) hakupendezwa na extensive research iliyofanyika kwa sababu waliona kuwa mambo mengine bora yakasahaulika

2. Kundi la pili ni la wanafunzi (wa Tanzania) mithili ya waziri wa mambo ya nje wa ujerumali aliyejiuzulu baada ya kugundulika kuwa alicopy & paste Phd thesis yake. I can only imagine mwanafunzi aliye mjanja akiamua ku fanya copy & paste ya hiki kitabu aka Plagiarise.

All in all, I only wish ma Professa wetu wangeweka academic works zao online kama Harith alivyofanya na hii ya KWAHERU UHURU KWAHERI UKOLONI

As it stands I will trust this scholarly ya OKELLO ya Harith kuliko newspaper articles toka kwa supermarket journalists wetu.

Ombi kwa mwanakijiji. Can you try to get a radio interview na Harith? Kama ukihitaji contacts zake plse niPM
 
JohnGalt,

Kwanza karibu JF. Pili, Dkt. Harith Ghassany mwenyewe ni memba humu, alishakileta humu hicho kitabu, kilichambuliwa kama karanga!

Wanazuoni wa JF walimbana mwandishi kwa hoja left, right and centre, alishindwa kuzijibu hatimaye aliishia kukimbia!.

Kwa kukusaidia tuu, mimi ni mmoja wa waliokisoma hicho kitabu,kama ningekuwa ndio msimamizi wa thesis ya Ph.D ya huyu Dr, asingeipata ng'o kwa kujenga premise based on fasihi simulizi na kuigeuza fasihi andishi, wakati akifanya research yake,tayari ilishajijengea picha fulani kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,hivyo aliamua kuihalalisha picha hiyo kwa simulizi alizoziona ziko favaurable na mind opinion yake.

Mimi nilisema, napenda sana kusoma hadithi hivyo nilimshukuru mwandishi kwa kuwa ni story teller mzuri.

Hoja moja muhimu ambayo nilimpongeza ni kwa kuandika something kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, mengi hayajaandikwa na makovu hayajapona hivyo hitaji la truth and reconciliation commission lilikuwepo japo limeshapoozwa na GNU!.

Asante kutukumbushia, JF inasajili member wapya kila kukicha, hivyo acha wapya pia wapate na wasome.
 
JohnGalt,
Kwanza karibu jf, pili Dkt. Harith Ghassany mwenyewe ni memba humu, alishakileta humu hicho kitabu, kilichambuliwa kama karanga!.

Wanazuoni wa JF walimbana mwandishi kwa hoja left, right and centre, alishindwa kuzijibu hatimaye aliishia kukimbia!.

Kwa kukusaidia tuu, mimi ni mmoja wa waliokisoma hicho kitabu,kama ningekuwa ndio msimamizi wa thesis ya Ph.D ya huyu Dr, asingeipata ng'o kwa kujenga premise based on fasihi simulizi na kuigeuza fasihi andishi, wakati akifanya research yake,tayari ilishajijengea picha fulani kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,hivyo aliamua kuihalalisha picha hiyo kwa simulizi alizoziona ziko favaurable na mind opinion yake.

Mimi nilisema, napenda sana kusoma hadithi hivyo nilimshukuru mwandishi kwa kuwa ni story teller mzuri.

Hoja moja muhimu ambayo nilimpongeza ni kwa kuandika something kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, mengi hayajaandikwa na makovu hayajapona hivyo hitaji la truth and reconciliation commission lilikuwepo japo limeshapoozwa na GNU!.

Asante kutukumbushia, jf inasajili member wapya kila kukicha, hivyo acha wapya pia wapate na wasome.

Pasco

Asante kwa kuja na kuniweka sawa lakini kuna couple of things.

1. Nimetafuta threads zenye kuonyesha kitabu kilivyochambuliwa kama karanga sijazoja hata moja zaidi ya threads ambazo zinasema watu wakisome au wanarefer kama reference

In otherwords sijaona critical review of the book au thesis ya Ghassany

2. Naomba unipe walau mwelekeo wa hao wana zuoni wa JF maana at least naweza kuwauliza hata kwa PM wanionyeshe hizo post ambazo walizotoa kama ulivyosema hapo juu yaani LE,RIGHT & CENTRE

3. Je unaweza kunifafanulia at what point did Ghassany run away from hao "wanazuoni" wa Jamii Forum (baada ya kutolewa hoja gani?

4. Umesema kuwa wewe ni mmoja kati ya waliokisoma hiki kitabu na ungekuwa msimamizi wa thesis ya hii P/h D usigeitoa/ kwa sababu:

a) Thesis ilikuwa based on fasihi simulizi
b) Fasis simulizi kugeuzwa kuwa andishi
c) wakati akifanya research yake,tayari ilishajijengea picha fulani kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar
d)aliamua kuihalalisha picha hiyo kwa simulizi alizoziona ziko favaurable na mind opinion yake.

Mimi ninachosema ni kuwa kwanza ningependa kusoma Critical literary review yako on this book ili tuweze kuwa sambamba. Sasa kwa sababu hii ni scholarly work tena ameifanya akiwa mwanafunzi toka kwenye Chuo ambacho ni credible (HARVARD) sidhani kama hao waliomsupervise na hilo jopo la baraza lilokaa naye wakati anatetea hii academic work yake ni watu ambao hawakujua jinsi alivyofanya research yake na mwishowe wakamu award hiyo Doctorate yake. Mind you hii ni kazi ambayo ni NON-FICTION hivyo maswali ambayo obviously ile panel waliyafanyia kazi ili kujua yalikuwa ni:

1. Je Subject ilikuwa ni nini na hiki kitabu kilikuwa kinadeal na period gani?

2. Je how thorough Ghassany amekuwa katika research yake?

3. Je alitumia sources zipi?

4. Je hizo simulizi zilikuwa in broad/detailed?

5. Je style ya uandishi ni wa kigazeti gazeti (reportorial ) au ile ya interpretive writing? (ambayo inampa msomaji uelewa na ufafanuzi zaidi wa matukio)

6. Je thesis yenyewe iilikuwa na maana gani?

7. Je treatment ya hii thesis ni superficial au profound?

8. Je walengwa wa hiki kitabu walikuwa akina nani? ( vyuo vya elimu ya juu au ndio wale wale wasoma riwaya kama zile tunazozisoma magazetini?}

9. Kwa sababu ni kitabu kinachozungumzia mapinduzi je kuna biographical writing toka kwa Ghassany kwenye hiki kitabu?

10. Je Ghassany ameweka emphasise yoyote kwenye social or political history ?

11. Je tarehe zimetumiwa barabara ?

13. Je zipo maps, illustrations, charts, etc. kwenye kitabu if so je jopo la Harvard lilippitia au lilifanyia evaluation?

Kwa uelewa wangu mdogo hayo ndio machache ninayoyakumbuka nilivyofundishwa na mwalimu wangu (nakumbuka nilifanya mambo ya environmental Political Theory) na ilikuwa mara yangu ya kwanza kuambiwa nifanye critical review ya journal article fulani.

Anyway tatizo kubwa ambalo nimeliona humu JF so far ni hili la kuwa BIASED based solely on prejudice na feelings ambalo kiini chake naona ni huko mashuleni ambako wanafunzi wetu wanatokea.

It would be interesting kama hii forum ikawa na members wachache lakini inakuwa ni Agora ya mijadala yenye marefu na mapana kuliko the current trend ya kuogopa controversy (as long as watu wako within the Forum guidlines sioni sababu ya kufuta au kufunga threads) Maana kila thread niliyotafuta yenye posts za hiki kitabu ilikuwa imefungwa!

Sasa najua utakuwa uko bize na mimi hapa natazama hili panga la DFID kwa akina Lesotho, India na Burundi lililotangazwa jana.
 
Wakati huo huo tusisahau kuwa wengine ambao tunalazimishwa kuwasahau ni
Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu, Tewa Said Tewa,Ali Migeyo , Suedi Kagasheki,Dossa Azizi,Abdulkarim Karimjee,Chifu Abdieli Shangali wa Machame, Kleist Sykes,Ally Sykes na Abdulwahid Sykes

kwa uchache sasa huyo Okello alikwa ni just one in a million na at least eyey leo anazungumzwa

Mnaojua tunaomba mtujuze juu hawa wazalendo waliopigania nchi hii kiukweli....
 
Pasco Dr Ghassany anayo PhD yake zamani, hiki kitabu ilikuwa ni kuandika historia kama alivyofasiri yeye kutokana na mahojiano na walioshiriki.

Nampongeza kuweza kusafiri mpaka Algeria kwa akina Ahmed Benbella na kuwahoji. Wengine tulikuwa tunasikia tu hatukujua rile ya Algeria kwenye siasa za Zanzibar.
 
Huyu mtu aitwaye John Okello alikuwa ni mercenary, Kwa Kiswahili sanifu anaitwa Mamruki...! Sasa ni nchi gani ambayo imetumia majeshi ya kimamruki kupindua nchi kisha wakaitwa mashujaa!?

Ninavyojuwa mimi mamruki wote ukodiwa kwa kazi chafu yoyote na wakishalipwa biashara inakuwa imekwisha, sasa John Okello yeye alitaka kulowea kabisa na kutaka kutawala, sasa aliposhtukiwa ndio kama hayo yaliomkuta.

Mkuu samahani kwani Kiswahili sanifu si Mamruki bali ni Mamluki. Samahani sana, ni katika kuelekezana tu.
 
Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.

Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.

Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.

Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]

Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?

Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?

"Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?"

Tukuulizeni nyinyi mliomleta Zanzibar kuendesha mauaji ya kimbari.
 
Pasco

asante kwa kuja na kuniweka sawa lakini kuna couple of things.

1. Nimetafuta threads zenye kuonyesha kitabu kilivyochambuliwa kama karanga sijazoja hata moja zaidi ya threads ambazo zinasema watu wakisome au wanarefer kama reference

In otherwords sijaona critical review of the book au thesis ya Ghassany

2. Naomba unipe walau mwelekeo wa hao wana zuoni wa JF maana at least naweza kuwauliza hata kwa PM wanionyeshe hizo post ambazo walizotoa kama ulivyosema hapo juu yaani LE,RIGHT & CENTRE

3. Je unaweza kunifafanulia at what point did Ghassany run away from hao "wanazuoni" wa Jamii Forum (baada ya kutolewa hoja gani?

4. Umesema kuwa wewe ni mmoja kati ya waliokisoma hiki kitabu na ungekuwa msimamizi wa thesis ya hii P/h D usigeitoa/ kwa sababu:

a) Thesis ilikuwa based on fasihi simulizi
b) Fasis simulizi kugeuzwa kuwa andishi
c) wakati akifanya research yake,tayari ilishajijengea picha fulani kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar
d)aliamua kuihalalisha picha hiyo kwa simulizi alizoziona ziko favaurable na mind opinion yake.

Mimi ninachosema ni kuwa kwanza ningependa kusoma Critical literary review yako on this book ili tuweze kuwa sambamba. Sasa kwa sababu hii ni scholarly work tena ameifanya akiwa mwanafunzi toka kwenye Chuo ambacho ni credible (HARVARD) sidhani kama hao waliomsupervise na hilo jopo la baraza lilokaa naye wakati anatetea hii academic work yake ni watu ambao hawakujua jinsi alivyofanya research yake na mwishowe wakamu award hiyo Doctorate yake. Mind you hii ni kazi ambayo ni NON-FICTION hivyo maswali ambayo obviously ile panel waliyafanyia kazi ili kujua yalikuwa ni:

1. Je Subject ilikuwa ni nini na hiki kitabu kilikuwa kinadeal na period gani?

2. Je how thorough Ghassany amekuwa katika research yake?

3. Je alitumia sources zipi?

4. Je hizo simulizi zilikuwa in broad/detailed?

5. Je style ya uandishi ni wa kigazeti gazeti (reportorial ) au ile ya interpretive writing? (ambayo inampa msomaji uelewa na ufafanuzi zaidi wa matukio)

6. Je thesis yenyewe iilikuwa na maana gani?

7. Je treatment ya hii thesis ni superficial au profound?

8. Je walengwa wa hiki kitabu walikuwa akina nani? ( vyuo vya elimu ya juu au ndio wale wale wasoma riwaya kama zile tunazozisoma magazetini?}

9. Kwa sababu ni kitabu kinachozungumzia mapinduzi je kuna biographical writing toka kwa Ghassany kwenye hiki kitabu?

10. Je Ghassany ameweka emphasise yoyote kwenye social or political history ?

11. Je tarehe zimetumiwa barabara ?

13. Je zipo maps, illustrations, charts, etc. kwenye kitabu if so je jopo la Harvard lilippitia au lilifanyia evaluation?

Kwa uelewa wangu mdogo hayo ndio machache ninayoyakumbuka nilivyofundishwa na mwalimu wangu (nakumbuka nilifanya mambo ya environmental Political Theory) na ilikuwa mara yangu ya kwanza kuambiwa nifanye critical review ya journal article fulani. Anyway tatizo kubwa ambalo nimeliona humu JF so far ni hili la kuwa BIASED based solely on prejudice na feelings ambalo kiini chake naona ni huko mashuleni ambako wanafunzi wetu wanatokea. It would be interesting kama hii forum ikawa na members wachache lakini inakuwa ni Agora ya mijadala yenye marefu na mapana kuliko the current trend ya kuogopa controversy (as long as watu wako within the Forum guidlines sioni sababu ya kufuta au kufunga threads) Maana kila thread niliyotafuta yenye posts za hiki kitabu ilikuwa imefungwa!

Sasa najua utakuwa uko bize na mimi hapa natazama hili panga la DFID kwa akina Lesotho, India na Burundi lililotangazwa jana.

Inaonyesha una utaalamu mkubwa juu ya masuala ya uandishi ingawa sijabahatika kuona kitabu chako chochote.

Haya unayoeleza/ unayouliza pengine ni masuala ya msingi lakini kwa sisi tuliobahatika kukisoma na kwa sababu yako tulioyashuhudia, tumeridhika kuwa ni kazi well done.

Kwanini hii kazi usiifanye wewe kama uko that much interested kuliko kuachia wengine kuifanya?

Hapa naona dalili za wivu lakini pia si mbaya sana.

"Kuuzunguka mbuyu si kazi, kazi kuukumbatia"
 
kwanza umentamanisha sana hayo makaimati...lakini muhimu zaidi inabidi uyapate kwenye kikombe cha kahawa iliyopikwa ahhhhh

anyway nimependa GG alivyomweka sawa bwana Pasco ambaye naona hakurudi tena kumjibu

Je Pasco ana PhD ya nini mpaka anasema kuwa ingekuwa yeye asingempa maksi yoyote mwandishi bwana Harith?

Unless Pasco knows something some of us might have overlooked!
 
Wakati mwalimu wangu ananifundisha somo la historia nikiwa darasa la nne alitufundisha kwamba kiongozi wa mapinduzi ya zanzibar alikuwa field marshal john okello ambaye kwa asili yake alitokea uganda.

Mwalimu wangu huyu alitueleza kwamba usiku wa mapinduzi huyu karume hakushiriki kamwe kwani alikuwa amejificha. Lakini katika kufuatilia historia ya mapinduzi ya zanzibar ni wazi karume hausiki na wala hastahili kuhenziwa kama shujaa wa mapinduzi yale.

Ukweli utabaki, john okello ndiye kiongozi na shujaa wa mapinduzi ya zanzibar ya januari 1964. Hawa wanaohenziwa ni maghumashi tu ukizingatia historia halisi ya tanzania imefisadiwa kwa kiwango kikubwa.
 
Wakati mwalimu wangu ananifundisha somo la historia nikiwa darasa la nne alitufundisha kwamba kiongozi wa mapinduzi ya zanzibar alikuwa field marshal john okello ambaye kwa asili yake alitokea uganda. Mwalimu wangu huyu alitueleza kwamba usiku wa mapinduzi huyu karume hakushiriki kamwe kwani alikuwa amejificha. Lakini katika kufuatilia historia ya mapinduzi ya zanzibar ni wazi karume hausiki na wala hastahili kuhenziwa kama shujaa wa mapinduzi yale. Ukweli utabaki, john okello ndiye kiongozi na shujaa wa mapinduzi ya zanzibar ya januari 1964. Hawa wanaohenziwa ni maghumashi tu ukizingatia historia halisi ya tanzania imefisadiwa kwa kiwango kikubwa.

"History does not repeat itself. The historians repeat one another".
- Max Beerbohm
 
mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru john okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.

Baada ya mapinduzi kufanikiwa john okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa zanzibar mzee karume na babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza john okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.

Baada ya hali kutulia okello anamtangaza karume rais na abdulrahman babu kuwa waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.

Baada ya siku chache mzee karume akamfukuza zanzibar kama mbwa john okello [field marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]

naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya john okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?

Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la field marshal dedan kimathi...mbona wapenda hitoria zanzibar na tanganyika kwa jumla hamumtendei haki john okello [fieldmashal]?
hizi ndo shukran za viongozi wetu-maana wanachoweza wao ni kugeuza ukweli kuwa uongo,karumke hana mchango wowote kwenye mapinduzi
 
Back
Top Bottom