Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Fatma,mama Karume ameeleza kuwa wakati wamelala na Mzee karume alikuwa akisikia risasi nje na wao hawakuwa na taarifa yoyote ya mapinduzi na wala Karume hakujua mapinduzi yatakuwa lini,lakini mpango wa kupindua ulikuwepo pia naye Karume alikuwa anajua kuwa siku moja yatakuwepo.
Mama Karume kaeleza mengi sana yanayoonesha kuwa Karume hakuhusika,ila baada ya mapinduzi kuna watu walifika kwa karume wakiwa na gari ya kijani na nyingine ya manjano walikuwa wamefunga shoka juu ndo walipofika kwa karume na kupitia mlango wa nyuma waligonga mlango na mama karume alipofungua mlango aliona sura ambazo hakuzikariri wala hakuziona tena,walifika wakasema wanamtaka mzee na kisha waliondoka nae baada ya kukamilisha mapinduzi! Nadhani mama amemaliza utata uliokuwepo hapa Jamvini.
Mkuu Gsana, wewe ulimsikia kwa masikio yako mwenyewe Mama Fatma Karume akiongea hayo?.
Mimi pia niliwahi kumuona na kumsikia Mama Fatma Karume akiongea haya kuhusu siku ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

P
 
OKELO ALIRUDI KWAO UGANDA NA KUFIA HUKO KWA WACHOLI WENZAKE, NYERER ALIMZAWADIA GARI NA PESA ZA MAFUTA ILI ARUDI NYUMBANI SALAMA ,LAKINI ALIPATA AJALI NJIANI NA AKANUSURIKA KUFA ILA GARI IKAWA RIGHT OFF,HAPO AKALA BODA KWA MABASI HADI ACHOLI.
 
OKELO ALIRUDI KWAO UGANDA NA KUFIA HUKO KWA WACHOLI WENZAKE, NYERER ALIMZAWADIA GARI NA PESA ZA MAFUTA ILI ARUDI NYUMBANI SALAMA ,LAKINI ALIPATA AJALI NJIANI NA AKANUSURIKA KUFA ILA GARI IKAWA RIGHT OFF,HAPO AKALA BODA KWA MABASI HADI ACHOLI.

okelo alikua mkenya
 
Kwadwo. Unataka watu wa Unguja na watu wa Pemba wamtambuwe Okello? Okello hakutambuliwa na ASP wala TANU leo atatambuliwa na Wazanzibari. Hebu nioneshe wapi alipotajwa na vyama hivyo kwamba yeye ndie shujaa. Okello alikua mdini na ndio kilichomponza eti anasema kwamba kapindua kwaajili ya Ukristo?.
 
Kwadwo. Unataka watu wa Unguja na watu wa Pemba wamtambuwe Okello? Okello hakutambuliwa na ASP wala TANU leo atatambuliwa na Wazanzibari. Hebu nioneshe wapi alipotajwa na vyama hivyo kwamba yeye ndie shujaa. Okello alikua mdini na ndio kilichomponza eti anasema kwamba kapindua kwaajili ya Ukristo?.
sawa sawa
 
Philemon umesema ukweli,

Historia ya Tanzania imekuwa na tabia ya kufuta michango ya wale ambao hawakupendwa na wakubwa: John Okello akiwa mmoja wao.

Ingawa sijasoma maandiko yaliyopo kuhusu historia ya Tanzania kwa muda mrefu ukweli wa kuwa majina kama ya Okello, Kambona, na Kanali Mahafudhi yamefutika kabisa katika historia ya Tanzania. Bibi Titi Mohammed alipata bahati baada ya kurudi CCM na hivyo kurudisha jina lake katika historia lakini nalo lilikuwa limeshapotea.

Tutafute utaratibu wa kutunza historia kamilifu ya nchi bila kujali uhusiano wa wahusika na "ukoo wa mfalme" ulikuwaje.
ev uyu chegevara nimtu ainagan mwalabu mcyopia au
 
Kwadwo. Unataka watu wa Unguja na watu wa Pemba wamtambuwe Okello? Okello hakutambuliwa na ASP wala TANU leo atatambuliwa na Wazanzibari. Hebu nioneshe wapi alipotajwa na vyama hivyo kwamba yeye ndie shujaa. Okello alikua mdini na ndio kilichomponza eti anasema kwamba kapindua kwaajili ya Ukristo?.
Kumbe?
 
Yan bro the article is there natumesoma na tumeelewa kwamba okello was not who u think he is was crazy we can that say that in accordance with the the article so why don't we shut up and believe that I know u just want to talk abt him even after knowing the truth just because u want to push the talk LETS BE CIVILIZED

Phillemon,

Tafuta kile kitabu aliandika Okello juu ya mapinduziya Zanzibar. Utaanza kujiuliza Karume alikuwa na role gani pale. Pia ya kusikitisha zaidi, alipofukuzwa Zanzibar hakuruhusiwa hata kuchukua mizigo yake--achilia mbali malipo/compesation yake.
 
OKELLO BABA WA TAIFA LA ZANZIBAR .ALIYEWAOKOA WAZANZIBAR TOKA ITUMWANI NA BADO HAWAMTAMBUI.


Kikubwa ni shinikizo kutoka jumuiya za kiwataifa na mashirika mbalimbali ya haki za kibinadamu, wanadai kuwa ule ulikuwa ni unyama (genocide) dhidi ya wanawake watoto na wazee wa kiarabu hasa wenye asili ya Oman, maana watu wenye asili ya Uajemi wawakuguswa hata kidogo.

Wengi waliuwa cold blooded yani unaambiwa walikuwa wanapanga mstari msururu mrefu na wote wanauwawa kwa upanga maana hata risasi zilikuwa chache yaani kifupi yale yalikuwa mapinduzi ya mapanga

Makaburi ya watu wengi(mass grave's) yalitapakaa maana ilikuwa ni ngumu kuzika watu wote kwa muda huo mfupi, sasa kutokana na pressure za media ndio kina Karume wakamrushia mpira Okelo na wao kwa kukwepa mkono wa jumuiya hizo za kibinadam wakaamua kujificha nyuma ya mgongo wa kaka mkubwa Tanganyika,

Na wao ndio waliomshinikiza mkapitalisti Nyerere aliolesoma Marekani na Ulaya na Missionary schools za haohao makapitalisti kugeukia upande wa wakomunisti chini ya uangalizi wa Abrahaman Babu(huyu jamaa unaambiwa ni hatari kuliko hata huyo Okelo mliemtia umaridadi)

Vitu vingi juu ya historia ya mapinduzi ya Zanziba havipo wazi, yani unaambiwa Okelo alikuja akadai ametumwa na Mungu cjui yesu kwenye nchi ambayo 99% ni waislam na kufanikiwa kupata sapoti ya wazawa bado haiingii akilini hata kidogo,


Kuna kitabu alikuwa nacho mwalimu wangu wa historia zamani hizo sidhani kama nnaweza kukipata nikiweke hapa, ila kuna documentary iliokwenye mfumo wa video ilirekodiwa na muitaliano mmoja akiwa kwenye helicopter inaonesha watu wanapanga mstari kwenda kuuliwa na pia inaonesha makaburi ya watu wengi na kuna mizoga ya watu wengine baharini wakijaribu kutoroka kwa kuogelea
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Field Marshall John Okello, baba wa mapinduzi ya Zanzibar, mbabe wa Sultan Jamshid.

Angalau sasa tunajua kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na vijana wa ASP lakini hayakuongozwa na viongozi wa ASP, bali yaliongozwa na Jemedari John Okello, mganda aliyepatiwa mafunzo ya kijeshi huko Cuba.

Tunajua pia viongozi wa bara, akina Oscar Kambona walipanga kufanya mapinduzi dhidi ya Sultan Jamshid, lakini walichelewa. Watu wawili waliotumwa kuomba silaha huko London walitumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya telegramu na kuambiwa wasitishe shughuli hiyo kwani mapinduzi yamekwishafanyika.

Kumbe, vijana waliokuwa wakipatiwa mafunzo kwenye mashamba ya mikonge kule Tanga ili wakamng'oe Sultan, hawakuwahi kufanya kazi waliojiandaa nayo.

Badala yake John Okello akatumia hasira za vijana wa ASP na kufanikiwa kumg'oa Sultan Jamshid aliyekuwa na ulinzi dhaifu. Silaha ambazo Sultan Jamshid aliagiza kutoka Misri, hazikufika, na waingereza nawo walimuacha bila ulinzi wa maana. Ikawa kazi rahisi kwa Jemedari John Okello.

Hivyo ndivyo! Watu wanaongea mengi lakini ni ukweli kwamba mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa 'Surprise' kwa viongozi wa bara na visiwani. Nyerere, Kambona, Karume, Babu, Hanga, Moyo, Kawawa walishuhudia tu, Sultan kakimbilia Mombasa na John Okello akijimwambafai katikati ya viyunga vya Stone Town! Sultan mpya alikuwa mjini. Mapinduzi yaliyopangwa hayakufanyika, yaliyofanyika yalikuwa ya ghafla na ya kushangaza waliopanga.

Wakati mapinduzi yakiendelea, kiongozi wa ASP, Abeid Aman Karume alikuwa amejihifadhi kwenye kijumba kimoja huko Zanzibar. (Taarifa zingine zinadai Dsm).

Akihojiwa na TBC, siku ya Tarehe 12 Januari 2012 mjane wa mzee Karume, Bi Fatuma Karume alikiri kuwa yeye na Karume walihifadhiwa kwenye kijumba huko Zanzibar. Baada ya muda walisikia sauti ya gari ikaribia huko walipohifadhiwa; ndipo Karume akamwmbia mkewe;

'Unasikia hilo gari? Wanakuja hapa. Kama mapinduzi yamefanikiwa basi mimi nitakuwa Rais, Kama hayajafanikiwa basi nitachukuliwa na hutaniona tena' maneno ya Bi Fatuma Karume, Januari 12, 2012 TBC.

Ikiwa maneno hayo ni ya kweli, basi itoshe kusema Karume alipata taarifa kuhusu mapinduzi, lakini hakushiriki kimwili. Na kama si msaada kutoka bara (baada ya mapinduzi) basi John Okello, mtu mbabe, bwanavita na jemedari mjinga angetawala Zanzibar.

Kutoka kwa,
Christopher Cyrilo
 
Imekuwa kawaida kwa gazeti la Monitor la Uganda kuadhimisha mapinduzi ya Zanzibar kwa kutoa makala zinazomtambulisha Field Marshall John Okello kama kiongozi pekee wa mapinduzi ya Zanzibar.

Mwaka huu wametoa makala iliyoandaliwa na mwandishi Felix Ocen inayomtambulisha John Okello akiwa na miaka 25 akiongoza kikosi cha watu 600 kwa muda wa masaa tisa tu na kufanikisha kumpindua Sultani.

John Okello aliyeingia Zanzibar miaka minne kabla ya mapinduzi, alikuwa mzaliwa wa familia ya kawaida katika wilaya ya Alebtong kaskazini mwa Uganda.

Okello, baada ya harakati zake za mapinduzi aliandika kitabu alichokipa jina The Revolution in Zanzibar, lakini kilipigwa marufuku kuchapishwa na serikali zote za Afrika Mashariki.

Gazeti linasema kuwa Okello aliongoza D-Day na wafuasi wake bila uwepo wa watu tunaoambiwa waliongoza mapinduzi hayo yaani Abeid Karume na Abdurahman Babu. Hawa wawili walikuwa wamefukuzwa visiwani na utawala wa Sultan, na walishangazwa sana kusikia kuna mapinduzi Zanzibar.

Okello alifanya siri mpango wake wa D-Day mpaka ilipofika usiku wa tarehe 11 January 1964, alipowakusanya wafuasi wake na kuwaamuru kuivamia kambi ya silaha ya Ziwani wakiwa na silaha za jadi.

Baada ya kufanikiwa kuiteka kambi ya silaha huku walinzi wa kambi wakitoroka, Okello na wafuadi wake walielekea mji mkongwe wakiwa wamejiimarisha kwa silaha kali. Kwa masaa machache walifanikiwa kuuteka mji mkongwe huku Sultan akikimbilia Dar es salaam kuomba hifadhi kwa Nyerere, lakini Nyerere alikataa na ikamlazimu Sultani kuelekea Mombasa kisha Uingereza.

Mpaka kufika asubuhi, Okello na wafuasi wake walikuwa wameshikilia vituo vyote vya muhimu huku akiwaamsha wazanzibari kwa tangazo "This is John Okello, the Field Marshall of Pemba and Zanzibar. Wake up you imperialists, there is no more imperialist government. Wake up you Blacks, pick the weapons and clear out the remnants of the imperialist government.... I am giving the Sultan 20 minutes to kill his children and wives and later himself, or else Okello will do it."

Mpaka kufika jioni watu takribani 13,000 walikuwa wameuliwa, huku zaidi ya 12,000 wakiwa waarabu. Viongozi wote ambao hawakufanikiwa kutoroka zahama ya Okello walitangaza kujisalimisha na kumuunga mkono Okello.

Okello aliunda kikosi cha wapiganaji wa mapinduzi kilichoitwa "Freedom Military Force" au Jeshi la Uhuru. Pia aliunda baraza la kwanza la mapinduzi, lakini walipompendekeza kuwa rais wa baraza alikataa. Badala yake aliwaita akina Karume kutokea Tanganyika, akampendekeza Karume kuwa Rais na Babu kuwa waziri mkuu.

Mengine fungua link usome wenyewe.

How Ugandan led revolution that ended Arabs reign over Zanzibar



Hapa kuna maswali kadhaa.

1. Kwanini CCM wanatudanganya watanzania na kuidanganya dunia?

2. Kuna faida gani tunazopata kwa kukataa kumtambua Okello kama kiongozi na baba wa taifa la Zanzibar?

3. Kwanini viongozi wa Afrika Mashariki walimwogopa Okello?

4. Inaonekana Okello alitekwa na watu wasiojulikana wakati wa utawala wa Iddi Amini na hajulikani alipopotelea mpaka leo. Serikali ya Zanzibar imefanya juhudi zipi ili haki za huyu Field Marshall zipatikane zikiwepo za kupewa heshima anayostahili?

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom