Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

This is Fake!.
P

IMG-20220112-WA0062.jpg

IMG-20220112-WA0065.jpg

IMG-20220112-WA0063.jpg
IMG-20220112-WA0062.jpg
 
Yaani watu wa Nobel prize waonyeshe fake video wakati wa kupewa zawadi Gurnah, kazi kweli
Labda tuelimishane tuu, hiyo 1964 fine color Video na zitoke wapi?!.
who was the producer?, unaujua ukubwa wa color video camera enzi hizo ni 16mm Film Camera, nani ailete Zanzibar?. Uwanja wa ndege ulikuwa umefungwa hicho kipepeo kimerukia wapi?.

Kwa hivyo hawa watu wa Nobel hawaelewi Na wanadanganya watu?
Hivi aliyefunga Airport ni nani ? Hivi hizi film Za zamani zinazokuwa updated kumbe hujaziona au Lumumba hamna taarifa?
Tatizo wewe kwako waliokufa ni ganda la usufi kwani hamna jamaa yako wala ndugu yako
 
Mwaka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.

Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.

Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.

Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]

Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?

Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?

View attachment 1923156

==============

Video ikimwonesha Okello,Karume na Babu masaa machache baada ya Mapinduzi

Kuna kile kitabi kinaitwa KWAHERI UKOLONI,KWAHERI UHURU kimeongelea mambo yote
 
Kuna kile kitabi kinaitwa KWAHERI UKOLONI,KWAHERI UHURU kimeongelea mambo yote
Kibosilee,
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' kilichoandikwa na Dr. Harith Ghassany ndicho kitabu kilichofichua mengi yaliyofichwa katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

John Okello hakupata kuwa kiongozi wa mapinduzi.
Atakuwaje Okello awe kiongozi wa mapinduzi na asiwe Abdallah Kassim Hanga?

Kulikuwa na kambi ya Kipumbwi, Tanga walipokusanywa Wamakonde wakavushwa na kuingizwa Zanzibar kuipigia kura ASP 1961 na mwaka wa 1964 kushiriki katika mapinduzi.

Hawa Wamakonde waliua Wazanzibari wengi sana.
Katika hali kama hii Okello unamtumbukiza wapi?

Kwenye kupanga mapinduzi au kwenye mauaji?

Kambi ya Kipumbwi kulikuwa na watu wawili muhimu katika kuandikisha watu na kuwaweka hapo kambini kwa mafunzo - Victor Mkello na Mohamed Omari Mkwawa.

Umepata kusikia majina haya yakitajwa katika historia ya mapinduzi?
Ali Mwinyi Tambwe na Jumanne Abdallah je?

Hawa wawili walikuwa Area na Regional Commissioner wa Tanga wakati ule.
Umepata kusikia majina haya katika historia ya mapinduzi?

Katika kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi Ali Mwinyi Tambwe alipewa medali kwa mchango wake katika mapinduzi.

Unajua kuwa wakati wa ukoloni Ali Mwinyi Tambwe alikuwa kachero wa Special Branch?

Jiulize mchango wa Ali Mwinyi katika mapinduzi ni upi?
Jiulize mwenyewe na ishughulishe akili yako.

Okello anaingia vipi katika watu hawa?
Okello alikuwa na nguvu gani ya kuweza kuwaamrisha hawa wote niliokutajia hapo juu?

Kweli huyu anaweza kuwa kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar?
Huyo hapo chini ndiyo Mohamed Omari Mkwawa.

Ana historia kubwa kushinda ya John Okello.

1647060767537.png
 
View attachment 2147590
Inasikitisha mambo mengi sana yamefichwa
 
Baada ya Mapinduzi Z'bar (1964), Saleh Sadalla Akida alipewa dhamana ya kuwa waziri wa Ulinzi. Akapitisha sheria kuwa wafungwa wawe wanakula mhongo na majani ya mhogo (suti). Alipofungwa, baada ya kutishiana bastola na Karume, akapewa mhogo na majani ya mhogo. Hakula. Mpishi Akamkumbusha "Mhe, chakula hiki ndicho ulichokitungia sheria wewe mwenyewe ukiwa waziri. Sasa vipi hauli?

Saleh Sadalla Akida alilia.
 
Maprofessa mahiri wetu mko wapi kwa historia ya kweli,upo wapi haroub othman,proffesa mazrui, baregu na wengine tele wasomi..wanazuoni.

Historia ya mataifa yetu hapa afrika mashariki imepindishwa, andikeni upya.
kwa nini tunawafundisha watoto uwongo?
Hivi ii!!? huko shule mnasomaga nini?? wajameni!! ujinga au....Mshindiii wa vita yeyote ilee!! ndiyo huwa anaandika Historia ya nchi hiyo ni sheria ya Historia Duniani... na

wale wooote walioshindwa vita ya kuijenga Tanganyika huru, huwa wanawekwa ktk sehemu au kundi lao la Historia inayo wastahili yaani lile la kushindwa lenye harufu ya ''usaliti'' uhasi uzandiki, Unafiki, urafi wa madaraka!

Mkuu watu hawa wameandikwa huko ktk mtizamo wa matatizo na changa moto za kuijenga Tanganyika huru! kitafute hicho kitabu utawakuta huko wamesheheni! walivo shiriki mpaka usaliti wao! hilo

La usaliti kwa maana ya matokeo ya vita ya ndani kwa ndani hasa ya kugombea Madaraka! hii ni vita mbaya sana!!...na inahitaji umakini wa hali ya juu Km Nyerere alivo kuwa makini!.....

Julius Alisema mapambano ya kuijenga Tanganyika huru bado yanaendelea! aluta continuor! ina maana vita ya ndani kwa ndani sasa weye haya hukuyajua kijana?

Marehemu Julius aliwahi sema haya mapemaa baada tu ya uhuru!! akilinganisha na Historia ya Mama Miti......na shoka la kukatia miti! itafute imo humu!

Mfano Kambona alikimbia mwenyewe bila kuguswa baada ya kutaka kumpindua/kumuua Nyerere lkn janja yake ikajulikana mapema toka kwa wana usalama watiifu wa upande wa Nyerere!! ......

nyerere alitumia mbinu moja kubwa baada ya kujua Kambona na Bibi titi na wenzake wengi tuu! walitaka kumpindua Nyerere.... so julius aka torokea na kujificha Kigamboni faster na kimyaaaa!!..

wakt wa seke seke la mapinduzi walijua Julius atatimkia UK! Lkn hakufanya ivo!! akabaki humu humu tena na wao wakajua fika Julius hakutimka bado yuko Ikulu!! lkn wapiiii.... tafuta weee!..holaa

hali hii iliwachanganya sana hao maadui zake Nyerere! yaani huyo Kambona na kundi lake!! ivo kambona akashindwa kujitangazia u rais! mAPema, baada ya kuhamasisha uhasi ule wa jeshi! sababu hakujua alipo julius!

Kumbuka hili la waasi likuwa kundi la wakubwa wengi hasa.... wakiwemo baadhi ya hao ulowataja hapo juu!....hii ilienda sambamba na historia ya shetani alivotaka kumpingua Mungu!! akashindwa!

shetani ameandikwa km aliyeshindwa....na Mungu ndo mshindi!! Hebu piga picha km shetani angemshinda Mungu je shetani ange muandika Mungu kwa mazuri? ,,,,

ivoivo na Historia ya nchi yetu!! Mshindi ndo huandika Historia ya ushindi!...walio shindwa huwekwa ktk kapu la kushindwa! na ushetani wa kila aina umesikiaaaa!! tatizo....... st kayumba mbaya sana!
 
Wanabodi,

Japo Shujaa wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni Sheikh Abedi Amani Karume, Kiongozi halisi wa Mapinduzi yale ni Field Marshal John Okelo.

Uthibitisho ni hii press conference ya Karume, Okelo na Babu, na wote wanamuelezea Okello kama ndie kiongozi wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

[h=1]Press Conference ya John Okello. [/h]

Kuona ni kuamini.

Tuacheni ubishi!. Karume hakuwepo Zanzibar, siku ya Mapinduzi!. Alikuja bara kuwapeleka shule wanaye Amani na Ali waliokuwa wakisoma kwenye nchini babu yao mzaa Baba!.

Nawatakia Mapumziko Memsa ya kusherehekea Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Pasco.

Mkuu JokaKuu kwanza hongera kwa bandiko zuri .
.
Niko Interested kujua ukweli juu ya mapinduzi ya Zanzibar na maisha ya John Okello baada ya mapinduzi.
Karibu mitaa hii Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?
P
 
Baada ya Mapinduzi Z'bar (1964), Saleh Sadalla Akida alipewa dhamana ya kuwa waziri wa Ulinzi. Akapitisha sheria kuwa wafungwa wawe wanakula mhongo na majani ya mhogo (suti). Alipofungwa, baada ya kutishiana bastola na Karume, akapewa mhogo na majani ya mhogo. Hakula. Mpishi Akamkumbusha "Mhe, chakula hiki ndicho ulichokitungia sheria wewe mwenyewe ukiwa waziri. Sasa vipi hauli?

Saleh Sadalla Akida alilia.
Niliiona hii kwenye maelezo ya Amani Thani Ferooz (Al marhum)
 
Nilishawahi kuuliza katika mwanzo wa mada hii: nini ilikuwa role ya Karume? Sasa naongezea: kwa nini Karume anastahili kuheshimiwa kwa mapinduzi ya Zanzibar il hali hatujui akuliwa na role gani?
Alikuwa kiongozi wa ASP na mwanaharakati wa kuleta utawala wa Waafrika dhidi ya udhalimu wa waarabu na wazungu walio wachache
 
Back
Top Bottom