Mapinduzi ya viwanda na dhana ya 'mwaka wa yubile' tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapinduzi ya viwanda na dhana ya 'mwaka wa yubile' tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunago, Feb 28, 2011.

 1. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Nampongeza Mh. L.Nyalandu katika kueleza (kupitia television kipindi cha dakika 45 cha kijana Selemani) mambo mengi ya makusudi na mikakati ya kuelekea Mapinduzi ya Viwanda. Aidha nampa big up pia kuongelea vyema waziwazi juu ya familia yake jambo hadimu kwa baadhi ya viongozi wetu. Jambo moja la kumshauri.

  Asichanganye makusudi yaliyopo na dhana halisi ya Mwaka wa Yubile (the Year of Jubelee). Bado Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2010-2015) ibara ya 48 (d) inalenga kuondoa udhaifu wa Menejiment na kuongeza Stadi za biashara na masoko na pia kuendelea kuimarisha sekta binafsi katika uwekezaji na biashara na pia katika kukuza soko la ushindani hivyo bado Viwanda na Mashirika kadhaa yataendelea kubinafsishwa na au kuuza hisa zake kwa umma na pia Wawekezaji wa ndani na nje. Sera ya Soko huria na ubinafsishwaji hatujaikana!

  Ni bayana kuwa kulikuwa na udhaifu mkubwa sana katika kuendesha na hata utoaji wa huduma wa Viwanda na Mashirika mengi yaliyokuwa yanamilikiwa na Serikali (Umma). Hivyo leo huwezi kuongelea kuyarejesha kwa waliokuwa wanayaendesha kupitia dhana ya mwaka wa yubile!

  Inatosha kusema kuwa utachukuwa hatua muafaka kutathmini njinsi hivyo viwanda & mashirika yanayofanya kazi leo na kama hali hairidhishi, basi mikakati mbadala ya mabadiliko au maboresho itachukuliwa ikiwa ni pamoja na kubadilisha menejiment, mbinu za uzalishaji, masoko na hata umilikaji wa kiwanda au shirika.

  Kutumia dhana ya ‘mwaka wa yubile’ katika shughuli ya kujitathmini na kufanya maboresho ni kusema kuwa Ilani ya CCM iliyopita ilikuwa kandamizi na sasa wewe unatutangazia mwaka wa kufunguliwa (year of liberation); sidhani kwamba hakika hii ndiyo nia yake.
   
Loading...