Mapinduzi ya Misri ni pigo kwa Mfalme wa Saudi Arabia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapinduzi ya Misri ni pigo kwa Mfalme wa Saudi Arabia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by abdulahsaf, Feb 13, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Hali ya afya ya Mfalme Abdullah ibn Abdulazizi wa Saudi Arabia imeripotiwa kuzorota zaidi kutokana na juhudi zake za kuzuia kutimuliwa madarakani dikteta wa zamani wa Misri Husni Mubarak.
  Duru zinaarifu kuwa Mfalme wa Saudia alijaribu kuishawishi Marekani iendelee kuunga mkono kubakia madarakani Mubarak pamoja na kuwa Wamisri waliowengi walikuwa wameshaanza mapinduzi ya kumtimua Mubarak aliyetawala Misri kwa miaka 30.
  Gazeti la World Tribune la Marekani limenukulu duru za kijasusi nchini humo zikisema kuwa harakati hizo za kuzuia ushindi wa mapinduzi ya Misri zimepelekea hali ya mfalme Abdullah kuzorota zaidi.
  Mtawala huyo wa Saudia alifanyiwa oparesheni Novemba 24 na Desemba 3 mwaka jana nchini Marekani na sasa anaripotiwa kuwa mapumzikoni nchini Morocco. Alhamisi iliyopita Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Saud al Faisal alikanusha uvumi kuwa Mfalme Abdullah alikuwa ameaga dunia. Alisema hali yake kiafya ni nzuri na ana hamu ya kurejea nyumbani kuendelea na kazi zake.
   

  Attached Files:

 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wasi wasi kama huo umewakumba watawala wote wanaoendesha nchi kiubabe kwa maslahi ya wachache. Jambo linalowapa wasi wasi hasa wale vibaraka wa nchi za mag'haribi ni kuona kuwa Marekani iko tayari kuwatosa ikishaona hawana manufaa nayo tena.
   
Loading...