Mapinduzi ya 1964 yaliwaunganisha Wazanzibari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapinduzi ya 1964 yaliwaunganisha Wazanzibari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Averos, Jan 12, 2011.

 1. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  NA KHATIB SULEIMAN, ZANZBAR

  MAPINDUZI Matukufu ya zanziba ya Januari 12, 1964 yalihitimisha utawala wa Sultan uliodumu kwa takriban karne moja.
  Ni mapinduzi ambayo yalikuwa na lengo la kuwaunganisha wananchi wa Unguja na Pemba kuwa kitu kimoja.
  Utawala wa Sultani wa Oman uliwagawa wananchi wa Zanzibar kwa kuwatawala katika nchi yao na kuwa watumwa. Wananchi wa visiwa hivi walikosa haki zao za msingi kama vile kumiliki ardhi ya makazi na kilimo, elimu, matibabu na huduma mbalimbali za kijamii.
  Uonevu huo uliwafanya viongozi wa chama cha Afro Shiraz (ASP) kufanya Mapinduzi Januari 12, 1964 chini ya jemedari wake mkuu, Hayati Abeid Amani Karume.
  Baada ya Mapinduzi matukufu, ASP ilikuwa na kazi kubwa ya kuleta maendeleo na kuwaunganisha wananchi wote kuwa kitu kimoja.
  Kuanzia hapo, Septemba 25, 1964, serikali ilitangaza elimu bure pamoja na wazalendo kupewa ardhi kwa shunguli za kilimo. Katika uamuzi wa kutoa ardhi, mwaka 1966 iliamriwa kila mwananchi kupewa ekari tatu.
  Ujenzi wa nyumba za kisasa za maendeleo ulitekelezwa ikiwa ni ilani ya ASP. Lengo lilikuwa kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora ambapo ujenzi wa nyumba hizo ulifanyika maeneo ya Michenzani, Kilimani na Kikwajuni.
  Vijijini, ujenzi huo uliendelea katika maeneo ya Gamba, Mpapa kwa upande wa Unguja na Chake Chake, Mkoani, Vitongoji na Micheweni kisiwani Pemba.
  Wazee wasiojiweza walijengewa makazi yao Sebleni mwaka 1967 ambapo Hayati Karume alisikika akisema: “kila mtu baadaye atafikia umri wa mtu mzima hivyo ipo haja ya kujenga mazingira mazuri kwao.”
  Kwa jumla, Wazanzibari walikuwa kitu kimoja wakiwa na upendo na kuchanganyika bila ya kujali dini au sehemu anayotoka mtu.
  Hali ya kisiasa ilianza kubadilika katika mwaka 1992 kufuatia kuingia kwa mfumo wa vyama vingi na baadaye kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 ambapo nyufa za kisiasa zilijitokeza.
  Uchaguzi mkuu uliwagawa Wazanzibari kutokana na itikadi za kisiasa baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na CUF.
  Ufa wa kisiasa ulizidi kujitokeza zaidi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 kwanimapema mwaka 2001, maafa makubwa yalitokea Pemba ambapo polisi walipambana na wananchi walioandamana na kusababisha vifo vya watu kadhaa.
  Hali ya kisiasa ilivurugika ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania ilizalisha wakimbizi wa kisiasa kwa wananchi wa Pemba kukimbilia huko Shimoni, Mombasa nchini Kenya.
  Mazungumzo ya kuleta muafaka wa kisiasa Zanzibar yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1998 kwa msaada wa Umoja wa Ulaya chini ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Chifu Emeka Anyauko.
  Hata hivyo, utekelezaji wa muafaka huo ulikosa nguvu za kisheria na kushindwa kutekelezeka ambapo joto la kisiasa kwa CCM na CUF liliendelea tena.
  Mwaka 2001, mazungumzo ya muafaka wa pili yalianza tena na safari hii kwa kiasi kikubwa kulitokea mabadiliko ya kisiasa ikiwemo marekebisho ya nane ya katiba ambayo yaliruhusu kuanzishwa kwa Tume ya Pamoja ya Muafaka.
  Marekebisho hayo yalibadilisha muundo wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ambayo ilikuwa ikilalamikiwa na CUF. Katika muundo mpya, tume hiyo ilijumuisha wajumbe kutoka CCM na CUF.
  Uchaguzi wa mwaka 2005 nao uligubikwa na matatizo ambapo CUF ilikataa kutambua ushindi wa CCM pamoja na aliyekuwa ameshinda kiti cha urais, Amani Abeid Karume.
  Mazungumzo ya kuleta muafaka na maridhiano ya kisiasa yalifanyika kwa mara ya kwanza Ikulu ya Zanzibar kati ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad.
  Hamad alimtambua rasmi Karume kuwa Rais halali wa Zanzibar.
  Kuanzia hapo, joto la kisiasa lilishuka kwa kiasi kikubwa na mazungumzo ya kisiasa yaliingia katika hatua kubwa na kuanzia Januari, mwaka jana, viongozi hao walikutana mara kwa mara.
  Baraza la Wawakilishi lilipitisha azimio la kuunga mkono mazungumzo hayo na kuwasilishwa mapendekezo ya kura ya maoni ambayo ingeamua muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
  Hatimaye, Julai 31, mwaka jana, Wazanzibari walipiga kura na kuamua kwa asilimia 66.4 kukubali kuwepo kwa muundo wa mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa.
  Maridhiano ya kisiasa yalifungua milango ya heri na kuleta amani na utulivu Zanzibar huku wananchi wakiamini kwa kiasi kikubwa kwamba serikali ya umoja wa kitaifa ndiyo muafaka wa kumaliza matatizo ya kisiasa Zanzibar.
  Akihutubia wananchi kwa mara ya kwanza baada ya kula kiapo cha utii na uaminifu kwa wananchi wa Zanzibar katika uwanja wa Amaan mjini hapa, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni, aliahidi kulinda maridhiano ya kisiasa ambayo yamewaunganisha wananchi wa Zanzibar.
  Alisema serikali ya umoja wa kitaifa imekuja kulinda na kutetea malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwa kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar kuwa kitu kimoja na kusahau tofauti zao za kisiasa.
   
Loading...