Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari

Ni lazima wakimbie kwa sababu ,Ilikua ni kutumikia jela,Ama kuolewa kwa lazima(warabu wa kik) ,Adhabu ilio kali hidhran na pili pili juu.Fuatilia youtube mahojiano sheikh muhamad barwan
 
Wanabodi,

Nafuatia makala maalum kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 1964, zinazorushwa mfululizo na Idhaa ya KIswahili ya BBC kila siku kuanzia 1:00-1:30.

Katika kipindi cha leo, Mmoja wa askari aliyekuwa zamu ikulu ya Sultani, kwa jina maarufu la Mzee Sukari, anasimulia first hand information kuhusu mapinduzi hayo! akihojiwa na Baruan Muhuza wa BBC. Amekiri kuwa Sultani hakufukuzwa Zanzibar, alikuwa akitafutwa hivyo alitoroka mwenyewe!, na baada ya Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar, waarabu hawakufukuzwa Zanzibar, bali walijiondokea wenyewe!.

Kesho kutafanyika mjadala maalum kuhusu Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar utakaoanza saa 12:45-1:30.
Baada ya mapinduzi Zanzibar - BBC Swahili - BBC.com
Zanzibar na miaka 51 ya Mapinduzi - BBC Swahili

Siku ya kilele, kutatolewa nishani maalum za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, sijui kama yule shujaa halisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Field Marshal John Okello, atakumbukwa!.

Paskali
Kuelekea kumbukumbu ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Paskali
 
Wengi wanadhani ubaguzi ni pale tu mwafrika anapobaguliwa na wazungu/waarabu wanasahau kuwa ubaguzi ni tabia na sio kabila,unapomchukia na kumdharau mwarabu/muhindi/mzungu/mtu wa kabila tafauti na lako na wewe pia unakuwa mbaguzi,watu weusi pia hatujasalimika na dhambi ya ubaguzi.
 
Pasco,

Kumbe hivi ndivyo unavyofanya research au ndio umepanga na kina Salim Kikeke muyatkufushe hayo Mauwaji thru BBC na. wewe ndie field corespondent mpaka 13/1/2014. Teh teh. Poor Pasco
Natuma salamu za pongezi ya miaka 54 ya Mapinduzi, matukufu ya Zanzibar kwa Wanzibari wote, Wazanzibara na Wapemba, japo hawakushiriki Mapinduzi.

Mapinduzi Daima.

P
 
Moja katika hotuba za karume alisema tutawamaliza waarabu wote mpaka akitokea mwarabu basi awe tunu na watu waseme ...mwaraaaaaaabu yuuuuuuuuuule
Yaan awe tunu kama dawa.
Lakini Mungu mkubwa akaondoka yeye warabu wanangara znz
Maadam hili lilisemwa tuu lakini halikutekelezwa, na sasa waarabu wanang'ara sio Zanzibar tuu, bali hadi huku kwetu bara, kwa hili tuu la Mwarabu kung'ara, nalo halistahili shukrani?, tena sio tuu anang'ara, bali hadi kutaka kurejeshewa Zanzibar kwa kipande cha karatasi!, huu ni Wema ulioje?.

P.
 
Natuma salamu za pongezi ya miaka 54 ya Mapinduzi, matukufu ya Zanzibar kwa Wanzibari wote, Wazanzibara na Wapemba, japo hawakushiriki Mapinduzi.

Mapinduzi Daima.

P

Utukufu wa mapinduzi ni kitu gani???

Kuvamiwa Zanzibar na jeshi la Nyerere likisaidiwa na baadhi ya vibaraka wapenda madaraka kutoka ASP na Umma Party ???

Kuuliwa watu bila makosa na kunajisiwa wasichana na wake za watu??

kukamatwa kwa waziri mkuu Muhammed Shamte pamoja na baraza lake la mawaziri na kupelekwa magereza ya Tanganyika na kufungwa kwa zaidi ya miaka 10 bila kufikishwa mahakamani ??

Kuwekwa kwa Muhammed Shamte magereza ya Nyerere hata kabla huo uitwao muungano haujafikiwa ???

Kuendelea kuwanyima watu wa Zanzibar haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka ???

Kuweka vikosi vya jeshi na usalama kila mtaa ???

Kuingiza madawa ya kulevya , malaya na kila aina ya uchafu ???

kuwaweka masheikh ndani ya magereza ya Tanganyika na kuwabqambikizia kesi za ugaidi kwa kutumia haki yao ya katiba kupinga muungano ???
 
Sultan Seyyid Said amekuja Zanzibar mwaka 1832, naamini unakijua fika alichowafanya watu aliowakuta Zanzibar kwa miaka yote zaidi ya 130, na hakuna yoyote aliyehadithiwa kilichotokea na aliyeandika kilichokuwa kinatokea, hivyo hakuna anayesikitika!, labda nikukumbushe tuu kidogo
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa, -hasiwa, -bakwa, na kuuawa kinyama!

Lakini kwa kilichotokea ile 1964, kwa vile mmehadithiwa, na wengi wengi mmeathirika ndio maana mnasikitika mnaponisoma, kitu pekee ninachoweza kusema ni poleni sana!.

Na ili kuukata mzizi wa fitna kama Mapinduzi yale yalikuwa matukufu au mauaji, ifanywe research kupima pros na cons za mapinduzi yale, pros zikizidi, then ni haki na halali kuyaita Mapinduzi Matukufu, na cons zikizidi, then tuyaite mauaji ya Zanzibar ya mwaka 1964, lakini katika mapinduzi yote ya umagwaji damu yanapotokea popote duniani, siku zote huwa kuna casualities na heroes, ukiandika chochote kwa kuwatumia wahanga wa casualties tegemea machungu, na kuyaita mauaji ya kimbari, mauaji ya halaiki etc, lakini ukiandika kuhusu the heroes, tegemea watasifu utukufu wa mapinduzi hayo na kuyaita Mapinduzi Matukufu na vibwagizo vya Mapinduzi Daima!.

Mimi bado nasisitiza Zanzibar wanahitaji the truth and reconciliation commission kuponya makovu ya Mapinduzi.

Pole tena.

Umeanza kutuletea propaganda za kanisa katoliki ??? labda na mimi nikukumbushe kidogo Biashara Ya Watumwa Ya Afrika Ya Mashariki

Hebu niambie mtu mmoja tu kutoka Zanzibar ambaye mzee wake alidhulumiwa na huyo Sultan Said kwa kuuzwa kama mtumwa , au mtu mmoja tu ambaye alibambikizwa kesi au kuuliwa na mfalme.

Yale hayakuwa ni mapinduzi ulikuwa ni uvamizi kutoka Tanganyika ulioratibiwa na Laanatullahi Nyerere chini ya uongozi wa kanisa katoliki

Inakuwaje mapinduzi yafanywe zanzibar , waziri mkuu wake na mawaziri wengine wapelekwe kwenye jela za Tanganyika bila hata kufikishwa mahakamani??

tena kabla ya hata huo uitwao muungano haujafikiriwa ???

Hebu niambie ni mtu gani upande wa hao waliopindua ambaye alifariki kwenye haya Mavamizi???

Wote walioathirika na wanaoathirika mpaka leo na huu Uvamizi ni wazanzibari , huku mkituletea hizo propaganda za CCM zinazopangwa na kanisa katoliki

Mwisho nauliza tena

Utukufu wa mapinduzi ni kitu gani???

Kuvamiwa Zanzibar na jeshi la Nyerere likisaidiwa na baadhi ya vibaraka wenye uchu wa madaraka kutoka ASP na Umma Party ???

Kuuliwa watu bila makosa na kunajisiwa wasichana na wake za watu??

Kukamatwa kwa waziri mkuu Muhammed Shamte pamoja na baraza lake la mawaziri na kupelekwa magereza ya Tanganyika na kufungwa kwa zaidi ya miaka 10 bila kufikishwa mahakamani ??

Kuwekwa kwa Muhammed Shamte magereza ya Nyerere hata kabla huo uitwao muungano haujafikiwa ???

Kuendelea kuwanyima watu wa Zanzibar haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka ???

Kuweka vikosi vya jeshi na usalama kila mtaa ???

Kuingiza madawa ya kulevya , malaya na kila aina ya uchafu ???

kuwaweka masheikh ndani ya magereza ya Tanganyika na kuwabqambikizia kesi za ugaidi kwa kutumia haki yao ya katiba kupinga muungano ???
 
Nawatakia kumbukumbu njema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyovikomboa visiwa hivi.
P
 
Moja ya Hotuba za Karume wakati huo wa Mapinduzi alikua akisema tuna taka Waraabu tuwaondoe kwa visa na kuwa fukuza mpaka abaki mwarabu wa dawa.
Yaani ukimuona basi utasema mwaraaaaaaaabu yuleeeeeeee kama mtu wa ajabu

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Back
Top Bottom