Mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 - Nafurahia yanayotokea leo?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,943
3,818
Nani alipinduliwa 1964? Ni Mfalme ni Uhuru wa Zanzibar ni kitu gani haswa?

Waathirika wengi wa mapinduzi ya 1964 Zanzibar ni waZanzibari na sio Mfalme, kauli za leo kwa walio wengi zinasema yanayotokea Zanzibar ni dhulma iliyofanywa 1964 na waathirika wanasema waache wauwane au wauliwe au yawakute,haijalishi mtu yupo chama gani kwani ukiangalia haohao walikuwa CCM jana leo wapo upande wa upinzani na kuonekana watetezi wakubwa.kuna waathirka wa mapinduzi wanasema dua zao zinajibiwa baada ya kusubiri muda mrefu na majibu yanapita kwenye mikondo mbalimbali.

Leo inaonekana walio upinzani wakipata vipigo vikubwa vikubwa na hata walio ndani ya CCM nao huwakuta majanga ,wote hao ndugu au jamaa zao au wazazi wao walishiriki katika Mapinduzi Matukufu. Je, wamesahau kama wao wanajinasibu ni WAISLAMU kuwa ALLAH hasahau ni suala la mida tu,na yanayotokea leo unaweza kusema ni adhabu au mapigo mjarabu yanayowaathiri wote walioshinda na walioshindwa,tumeona Husein alivyoondoka kwenye kuapishwa hakucheka hakufurahi,kasibiwa na nini? Alikuwa anakimbilia kutoka akaambiwa bado hili akarudi kisha hakugeuka kwenye mlango mazima.

Tayari utawala aliokuwa akiugombania umeshaingia doa la mauaji yasiyofutika. Reconciliation haitasaidia kitu kwani, katika uislamu kunahitajika kulipwa fidiya juu ya mauaji yaliyotokea.

Mapinduzi matukufu sasa ndugu anamuuwa nduguye iwe iwavyo ,inasemwa wanauwana wenyewe kwa wenyewe wacha wauwane ndio majibu ya dhulma iliyotokea 1964.

Vizazi vya walioshiriki Mapinduzi matukufu leo vinasota na kusaga meno ,hakuna maendeleo,yajayo yanafurahisha au yanakirihisha ? Tayari pengo lisilo zibika limeshatokea.

Kubwa ni serikali ya Husein itayarishe uombaji msamaha kwa Mapinduzi yaliyotokea 1964 ,wapo baadhi hawajafariki au familia zao zipo hai na irudishe ile sherehe za uhuru na kufuta hizi sherehe za Mapinduzi, ambazo zinaibua hisia za kuilaani serikali ya Zanzibar lana ambayo tunaiona leo inaitafuna Zanzibar. Je, Zanzibar ni kisiwa kilicholaaniwa?

CCM waliopo madarakkani hapa Zanzibar wasijidanganye kuwa wapo salama ni wangapi walikuwemo CCM na je leo wangapi kimewakuta, wangapi wameondoka CCM lakini kuondoka kwao ndio wamekuwa salama? Lana inawafuata huko huko waliko,haikimbiliki uwe CCM uhamie upinzani.

Moja ya ushauri ni kuifuta siku ya Mapinduzi ili kufungua Zanzibar mpya na kufungwa kwa siku hii kufuateni na kuomba msamaha kwa kiujumla kwa waathirika wote wa Mapinduzi ya Zanzibar awe mweusi au mweupe.
 
Back
Top Bottom