Uchaguzi 2020 Mapinduzi makubwa kwenye sekta ya afya: Uchambuzi wa ilani ya CCM 2020-25

Bekiri

Member
Jun 30, 2013
14
75
Ili kujenga Taifa makini lenye ustawi na maendeleo, huduma za afya ni muhimu sana ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za maendeleo ya nchi. *Sura ya tatu ya Ilani ya CCM, kipengele cha 81 kwenye huduma za Jamii* imeeleza kwa kina mafanikio makubwa yaliyopatikana katika maeneo mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitano na namna miaka mitano ijayo itavyoendelea kufanya mapinduzi na maajabu kwenye sekta ya afya. Mafanikio hayo ni:-

Ujenzi na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za afya ambapo idadi ya vituo vya kutolea huduma ya afya imeongezeka kutoka 7,014 mwaka 2015 hadi 8,783 ambapo zahanati zimeongezeka kutoka 6,044 mwaka 2015 hadi 7242, vituo vya afya kutoka 718 mwaka 2015 hadi 1,205, hospitali za halmashauri zimeongezeka kutoka 77 mwaka 2015 hadi 148 ikiwemo na hospitali mpya 71 zilizojengwa na kuanza kujenga Hospitali kubwa ya Uhuru inayojengwa Chamwino Mkoani Dodoma.

Aidha, Serikali kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita imekarabati hospitali 23 za rufaa za mikoa, ujenzi wa hospitali za rufaa katika mikoa 5, kuendelea na ukarabati wa Hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (MOI), ununuzi wa mtambo wa upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu, uboreshaji wa Hospitali za rufaa na kanda ya juu Kusini Mbeya, Bugando, KCMC, na hospitali ya Kanda ya Kusini-Mtwara.

Zaidi Serikali iliendelea kuongeza upatikanaji wa dawa kwa kupandisha bajeti ya madawa kutoka bilioni 31 mwaka 2015 hadi bilioni 270, kuongezeka kwa watumishi wa sekta ya afya kutoka 86,152 mwaka 2015 hadi 100,631 hivi sasa, kuhakikisha kila kituo cha afya na zahanati inayojengwa inakuwa na nyumba za watumishi ambapo kwa miaka 5 nyumba 784 zimejengwa pamoja na kuboresha matibabu ya Kibingwa kwa kuwezesha wananchi wa Tanzania kupata huduma hizo hapahapa nchini na kuokoa fedha za wananchi na serikali zilizokuwa zinatumika kugharamia huduma hizo nje ya nchi.

Serikali imeendelea kuboresha kwa kiwango cha juu sana huduma za kibingwa kwenye hospitali ya Taifa-Muhimbili, Taasisi ya MOI, Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Benjamin Mkapa ambapo huduma za kupandikiza figo na nyingine nyingi zilizokuwa zinafanyika nje kwa miaka mingi toka uhuru sasa zinafanyika hapahapa nchini.

Ilani ya CCM ya mwaka huu kwenye Sura ya Pili, kipengele cha 83 (a) hadi (z) kutoka ukurasa wa 136 hadi 138,* katika kipindi cha miaka 5 ijayo itaendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya afya kwa kuwa inagusa maisha ya Watanzania na ustawi wa Taifa letu kwa kuendelea kuiboresha zaidi. Katika kipindi hicho, Chama kitasimamia Serikali katika kutekeleza yafuatayo:-

(a) Kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto na kuzitoa bila malipo ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

(b) Kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa saidizi na vitendanishi kulingana na mahitaji kwa ngazi zote.

(c) Kuweka mazingira kwa wawekezaji na sekta binafsi kujenga viwanda vya kuzalisha dawa, vifaa, vifaa tiba na vifaa saidizi.

(d) Kujenga na kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya ili viweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi. Hadi kufikia 2025 Serikali itaongeza vituo vya kutolea vituo vya afya kwa asilimia 20 ya vituo 8,446 vilivyopo sasa.

(e) Kuimarisha mfuko wa bima ya afya nchini ikiwemo mifuko ya bima za afya ya NHIF na CHF ili kufikia lengo LA Serikali kuwa na bima ya afya kwa wananchi wote.

(f) Kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa hospitali 98 za halmashauri na kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika hospitali 28 za rufaa ngazi za mkoa na hospitali za halmashauri za wilaya 125

(g) Kuongeza udahili wa wanafunzi wa kada mbalimbali ya afya kufikia 25,000 na kuajiri wataalam wa kutosha wenye ujuzi na kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi wa sekta ya afya.

TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA.
 

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
1,135
2,000
Miaka yote 60 tangu uhuru CCM walikuwa wapi??

CCM imepoteza uhalali wa kushika Dola.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom