Mapinduzi makubwa duniani yameletwa na matumizi ya zana za madini ya chuma, ni heri uache vyote ili uchimbe chuma kama unayo

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Chuma ndio madini mama duniani, mapinduzi makubwa duniani yameletwa na matumizi ya zana za madini ya chuma, ni heri uache vyote ili uchimbe chuma kama unayo. Tena huna haja ya kutafuta mwekezaji kwenye madini ya chuma chimba mwenyewe.

Taifa lengo malengo litachimba chuma kwanza hata kabla ya dhahabu na nickel. Yaani kwa umuhimu itaanza chuma na kufuatiwa na makaa ya wawe, shaba, bati na dhahabu.

Chuma ndiyo itatumika kutengenezea zana kuchimbia madini mengine na njia za kusafirisha madini mengine.

Inaonekana uchimbaji wa chuma haupewi msukumo mkubwa kwakuwa hauna maslahi kwa viongozi mmojammoja, maana huwezi kuficha kipande cha madini ya chuma kwenye begi lako kama dhahabu na almasi.
 
Bora tungechimba chuma kuliko SGR,chuma haina hasara. SGR ni Kama ndege Hakuna masikini atakaemudu panda.Ni maalumu kwa ajili ya middle na upper income people.
kuzifahamu faida za SGR kwetu kunahitaji ubongo mkubwa sana. Huwezi kufahamu uwekezaji wa SGR utatuiingizia faida gani mpaka kwanza ufahamu hesabu zifuatazo:

1. Gharama halisi ya kuijenga SGR ni hela ngapi
2. Tutasafirisha nini kutoka na kurudi DSM kwa njia ya SGR
3. Hasara gani wafanyabiashara wa magari ya mizigo na abiria na wataingia wamiliki, wafanyakazi wa magari hayo, wafanyabishara kandokando ya barabara wanaotegemea uwepo wa magari hayo njiani kama vile mahoteli, wafanyabiashara ndogondogo wa vitunguu, nyanya, kuku, nk njiani yatakayopisha nafasi ya SGR kufanya kazi za malori na mabasi hayo na na serikali kukosa kodi ya malori na mabasi ya njia hiyo.
4. Wauza spea za malori na mabari
 
Sekta ya chuma huwa inaajiri watu wengi sana. Huyu anatengeneza nondo, huyu vijiko, huyu nut, huyu Bolt, huyu spoko za pikipiki, huyu kiti cha pikipiki, huyu iron sheets za mageti huyu steel beams za maghorofa. Chuma kinaweza ajiri hata mamilioni ya watu.
 
Hapana mkuu, hapa tunaongelea kile chuma halisi kinachotumika kujengea viwanda, magari, vifaa vizito vya uchimbani, makontena ya mizigo, matrekta, reli, mabehewa, nk
Sawa ila Alumas hutumika kukata vioo, kuchimba miamba, magari hawatumii vyuma tuu kutengeneza kuna Aluminium kwenye engine, gearbox, kuna madini ya bati ngumu zile body, chasis gari kubwa ndo chuma pure, koo kazi tunayo sana.
 
Hahahaaaa acha kuota mkuu, we are after money, hatuchimbichimbi, you can not extract minerals before doing an economical analysis. Is it economical?
Hakuna taifa linalochimba chuma ambalo ni maskini duniani, chuma kinavutia ujenzi na uwekezaji wa viwanda mama.
 
Sekta ya chuma huwa inaajiri watu wengi sana. Huyu anatengeneza nondo, huyu vijiko, huyu nut, huyu bolt, huyu spoko za pikipiki, huyu kiti cha pikipiki, huyu iron sheets za mageti huyu steel beams za maghorofa. Chuma kinaweza ajiri hata mamilioni ya watu.
exactly, hapo dhana ya kuwa taifa tajiri tungeitafsiri kwa vitendo. Hata wafugaji wangetengenezewa kengele bora za kufunga kwenye ng'ombe wao

Hata binadamu wa kale alipovumbua matumizi ya zana za chuma badala ya mawe maendeleo yao yalipiga hatua kubwa sana mbele.
 
Sawa ila Alumas hutumika kukata vioo, kuchimba miamba, magari hawatumii vyuma tuu kutengeneza kuna Aluminium kwenye engine, gearbox, kuna madini ya bati ngumu zile body, chasis gari kubwa ndo chuma pure, koo kazi tunayo sana
Kama ni vazi la mtu chuma ni sawa na kanzu na hayo madini mengine ni kama kilemba, kofia na skafu. Hayo madini mengine sio kwamba sio muhimu lakini ni lazima yatanguliwe na Iron kwanza na makaa ya mawe kama kipaumbele chetu namba moja kama taifa badala ya nickel, titanium, gold, diamond, germs etc.
 
Hapana mkuu, hapa tunaongelea kile chuma halisi kinachotumika kujengea viwanda, magari, vifaa vizito vya uchimbani, makontena ya mizigo, matrekta, reli, mabehewa, nk
Mkuu mbona unakoroga mambo sasa, mbona kama unachanganya idhaa? Magari yanatengenezwa na chuma? Makontena ni chuma kile?

Unaelewa tofauti kati ya bati, chuma na aluminium?
 
Mkuu mbona unakoroga mambo sasa, mbona kama unachanganya idhaa? Magari yanatengenezwa na chuma? Makontena ni chuma kile?

Unaelewa tofauti kati ya bati, chuma na aluminium?
We unafikiri contena ni nini?
 
Back
Top Bottom