Mapinduzi Madagascar: Lazima atakuwa amevuta bangi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapinduzi Madagascar: Lazima atakuwa amevuta bangi!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ZeMarcopolo, Mar 14, 2009.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hivi huyu kijana anayetaka kumtoa Rais wa Madagascar madarakani ni kitu gani kinampa kiburi? Na kwanini mataifa mengine yanaangalia tu kama sinema? Hivi hawajui kuwa hii tabia iko contageous? Hawajui kuwa wakilea huu ugonjwa unaweza kuamia kwa majirani very soon? Huyu kijana wa miaka 34 aliyekuwa DJ ni LAZIMA atakuwa amevuta sana bangi!
  Ni jukumu la jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kuwa huyu muhuni afanikishi kumtoa Rais aliyechaguliwa kidemokrasia madarakani. Kwanini jumuiya ya kimataifa inangoja mpaka ifikie point of no return ndio iingilie hili swala?
   
 2. K

  Kicheche Member

  #2
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ninayoona hapo katika maelezo yako ni lawama tu. toa sababu zinazokufanya kutoa lawama hizo kwanzo. uwezi kujua huenda naye amchoshwa na ufisadi na kumbuka kuwa huyo kijana hayuko peke yake .nakuwekwa madarakani kwa kupigiwa kura na wananchi sio kigezo pekee kuwa ni mtawala bora kwa maana hata Mugabe, hitler nao pia walipigiwa kura na wananchi kuwepo madarakani
   
 3. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huwezi kupata sapoti ya maelfu kwa sifa ya u-DJ au kuvuta bangi. Penye kufuka moshi pana moto.

  Lazima itakuwa huyo raisi Ravalomanana atakuwa amechemsha au huyo kijana ana ujumbe unaovutia zaidi ya matendo ya huyo mkuu wa nchi.

  I wish na sisi Bongo tungebadilisha mbinu na kuanza maandamano mpaka JK ang'atuke.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Hii ni Karma tu, alichofanya Ravalomanana kwa rais aliyemuangusha Bwana Ratsiraka ndicho Rajoelina anachomfanyia, you live by the sword you die by the sword, tena kutoka kiti kile kile cha meya wa Antananarivo.

  Ravalomanana alikuja kama bonge la mwanamapinduzi, lakini baadaye ikaonekana hamna chochote, sasa Rajoelina anasema huyu Rais ni mwizi tu.

  Tatizo ni kwamba hata Ravalomanana naye alisema hivyo hivyo, kwa hiyo hatuna njia ya kujua kwamba huyu Rajoelina naye ni mwanasiasa tu anayejifanya ana uchungu kumbe anataka urais tu, na akipata urais atasahau kila kitu, kama Ravalomanana.
   
 5. K

  Kicheche Member

  #5
  Mar 18, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15

  kutojua nia ya mtu anayeonakana kuwa ni mkombozi isiwe sababu ya kumwaachia mwizi aendelee kuhujumu. inabidi tumpongeze huyu kijana Rajoelina aliejitoa mhanga kukemea wizi na ndio maana hata majeshi yamemwachia nchi
  Raisi Ravalomanana ameliona kosa lake ndio maana ameachia ngazi!!
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Rajolina ana ujumbe kwa wana Madagaska,wizi umekidhiri kama kwetu,hatuna budi kuiga ili tuwaondoe wasanii na walinda mafisadi,tukishindwa tujiandae kwa kura 2010 bila kuruhusu vyombo vya dola kutumika kuwapitisha mafisadi.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Usipotoshe watu hapa.
  Rais wa Madagascar katolewa na nguvu za wananchi waliochoshwa na longo longo zake na janja janja zake za kuwa madarakani. Huyu kijana yeye alikuwa ni muongoza harakati tu na wao wameona anawafaa si kuwa rais tu bali kuwa kiongozi wao.
  Sasa subiri ikitokea tz ndipo tutaelewa nguvu za wananchi ni kitu gani maana watawala wetu wanadhani nguvu za wananchi zinazimwa kwa ffu au tpdf. Hapana wananchi wakikuchoka hata uje na mizinga nakwabia utakimbia mwenyewe.
  Nimemsikia Kikwete akilalama bbc nikamuonea huruma maana hakujua kuwa wanajeshi waliingilia kati kuinusuru nchi isichukuliwe na wananchi wenyewe bila mpangilio maana hilo lilionekana wazi.
  Huu ni mfano wa yajayo tu!
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  I think only time can help you understand what am talking about. Lets give this some time and see the result of haya mageuzi kwa maisha ya watu wa Madagascar.
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kuna watu na viatu.
  Watu wengine wanaamini damu yao ni kijani kwa sababu tu kwa muda mrefu sana wameshurutishwa kukubali hivyo.Ni rahisi kwetu kuwashauri kujinyonga kuliko Kuwashawishi watu hao kwamba damu yao ni nyekundu,pia kwamba waliowaambia damu yao ni ya kijani waliwachota akili.
  Pilipili iko shambani, walioko majumbani mwao wanapiga miluzi kwa ukali wake. Toba!!
   
 10. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ila sisi TZ tusije tukalogwa kumpa nchi kijana mwenzetu Zitto maana RA ataendelea kuinyonya hii nchi kama atakavyo. Maana kwa sasa Zitto yuko mfukoni mwa RA. Lakini huyu RA kwa nini atatuchezea waTZ kiasi hiki na sisi tunamwangalia tu! Itabidi tuji-organize tubebe hata mapanga tumtimue arudi kwao India. Tumechoshwa na huu wizi wa kupindukia wa mali za waTZ. Jamaa ni trionea lakini halidhiki. Vodacom ana hisa 19% ambazo kwa maana nyingine pato lake si chini ya milioni 190 kwa siku kwani pato la Vodacomu kwa sasa ni zaidi ya bilioni 1 kwa siku. Bado ana mitambo kwenye machimbo ya madini ambako nako anapata bilions of money, lakini bado tu yuko Kagoda, Richmond, Dowans etc. Enough is enough, tumechoka nawe RA dawa yako iko jikoni.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  AT least wao wame-take risk na kubadili hali kwa sauti ya umma... sijui wewe mwenzangu na mie uko comfortable na business as usual life au vipi

  Wahenga wanasema kipendacho roho.... they are ready and i believe wao si wajinga kupambania mabadiliko kwa kumwaga damu ya zaidi ya ndugu zao 150

  way to go for greedy african leaders
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,272
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu kijana anayetaka kumtoa Rais wa Madagascar madarakani ni kitu gani kinampa kiburi? Na kwanini mataifa mengine yanaangalia tu kama sinema? Hivi hawajui kuwa hii tabia iko contageous? Hawajui kuwa wakilea huu ugonjwa unaweza kuamia kwa majirani very soon? Huyu kijana wa miaka 34 aliyekuwa DJ ni LAZIMA atakuwa amevuta sana bangi!
  Ni jukumu la jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kuwa huyu muhuni afanikishi kumtoa Rais aliyechaguliwa kidemokrasia madarakani. Kwanini jumuiya ya kimataifa inangoja mpaka ifikie point of no return ndio iingilie hili swala?

  KWANI MWAKYEMBE ANAPENDA KUFANYA YALIYOFANYKA JANA
  WAMECHOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOKA
   
 13. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kitu walichokifanya wananchi wa Madagasca ni cha ujasiri sana na kinafaa kisambae Africa nzima ikiwemo Tanzania...

  Kwa nini kisambae? Maana watawala wanajua kwamba madaraka ni mali yao na si mali ya wananchi waliowaweka pale...

  Viongozi wamekuwa watawala (KINGS) na sio viona mbali (Leaders)... Watawala wa Africa wanajisahau sana na wamejitungia sherai mbalimbali zinazohakikisha ni wale tu wenye vision kama yao ndo wanachaguliwa, kwa mfano, mtu ana haki ya kupiga kura akiwa na miaka 18, ni kwanini basi waweke au kupitisha sheria kumtaka yeyote autakaye Uraisi lazima awe na miaka 40... huoni hii ni age discrimination? Kama unaweza kutambua uwezo wa mtu mwenye miaka 18 kupiga kura basi pia uwezo wake wa kuongoza akiwa miaka 18 na kuendelea lazima pia utambulike... Hili wana Madagasca wamelielewa na ndo maana hawakujali kama huyo kijana ana miaka 34 au 35 au 30... wamemuona tangu akiwa mayor wa Antananarivo na kazi yake waliiependa sio wananchi bali mapolisi na walinda usalama wa nchi-Wanajeshi...

  Nani asiyefahamu kwamba kupa support ya majeshi katika nchi zetu za kiafrika ni jambo humu sana? Hebu anagalieni wanajeshi wanavyooangaliwa hakuna hata mtu mmoja atakayediriki kuulizia Ufisadi ndani ya jeshi la wananchi kwa kisingizio cha usalama wa taifa ili hali wana usalama wa taifa wao wamekaa kimya...

  Ni jambo la ajabu kwa wana-jeshi wa Madagasca pia kutosa Rais wao na kumuunga mkono huyo kijana...

  Hizi ni nyakati za kijufunza toka Democrasia ya Madagasca na si kuwabeza au kuwakejeli kwa namna moja au yeyote ile...

  Sisi ndo wajinga tuliwao na akina RA na EL bila kuamka na kumkemea Muungwana kwamba kwa nini nchi inaliwa na yeye akiwa macho akisingizia acha sheria ichuke mkono wake? saa nyingine sheria inabidi zikae kando mpaka wenye nchi wananchi wakae chini na kukubaliana upya...

  siku moja haya ya Madagasca yatakuja Tanzania tutake tusitake maana watu wetu wakiaamuka katika lindo la usingizi totoro, watawala hawatataka tena kufanya madudu yao kama hayo wanayofanya huo Dowans na kutushia kuiweka nchi kwenye Giza ili hali wakijua hiyo ni kutomimiza majukumu yao waliyokuwa wanayatafuta kwa udi na Uvumba mpaka kwa akina kalumanzila...

  Ni hayo tu wakuu...
   
 14. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huu utaratibu tungeutumia TZ tungeweza kuokoa rasilimali zetu kwani kwa jinsi mafisadi wanavyolindwa 2010 ni mbali kwa kuokoa kilichobaki.
   
 15. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Zitto amelambishwa kidogo tu na mitambo ya DOWANS je ukimpa nchi si ndio ataipiga mnada!! Kijana huyu kama mbunge mwenzie toka Kigoma Kaborou ameonyesha udhaifu wake juu ya faranga!!
   
Loading...