Mapinduzi cup: Simba yaibamiza Jang'ombe magoli mawili bila majibu, kukutana na Yanga

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Kombe la Mapinduzi linaendelea mjini Zanzibar na mechi ya kwanza siku ya leo ni Simba anakabana koo na Jang'ombe Boys. Suluhu au ushindi kwa Simba vitamfanya aongoze kundi, ushindi kwa Jang'ombe utamfanya aongoze kundi. Mshindi wa kundi hili atakwaana na Yanga nusu fainali.

Mpaka sasa mpira umeanza na milango bado migumu kwa pande zote.

12' Simba anaongoza kwa goli moja kupitia kwa Laudit Mavugo.

45+' Mpira unaenda mapumziko, simba bado anaongoza goli moja.

Mpira umeisha na Simba imeshinda magoli mawili bila majibu yote yakifungwa na Laudit Mavugo. Simba watakwaana na Yanga kwenye nusu fainali siku ya Jumanne.
 
Dakika ya 54: Mavugo anaipatia Simba bao la pili shuti kali.

GOOOOOOOOOOOO!!!!!!
 
Back
Top Bottom