Mapinduzi Cup: Nusu fainali & fainali, na huyu ndiye Bingwa wa Visiwani na Bara

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,288
15,238
Bila shaka hakuna anayeweza kubisha kuwa Group B la Mapinduzi Cup litaongozwa na Yanga SC.
By tha way! Kama unabishana na hilo ,huenda ukawa unadhani kuwa Azam FC anaweza kuongoza hilo kundi. Assume mechi zote za Azam na Yanga wameshinda .....wao kwa wao wametoka sare. Hapo yanga atakaa juu kwa idadi ya mabao. (Ikumbukwe kuwa Wachezaji wa Yanga SC wamepewa mzigo wa kuhakikisha wanafunga zaidi ya mabao 4 kila mechi ya hatua ya makundi) na wamedhihirisha hilo katika mtanange wake wa kwanza wa michuano hiyo.

1. Yanga
2. Azam
3. Mwingine
4. Mwingine

Kundi B hakuna atakayebisha kuwa Matopeni FC mtaongoza kundi licha ya kuwa mmepangiwa kundi jepesi mno , URA wamepoteza mechi yao 1. sina hakika kama kupoteza kwenu point kutakuwa kwa kufungwa, Bali kwa kutoa sare. nadhani mtatoa sare na URA (kwa kuwa wanaonekana ni wagonjwa pia)...Hapo mtakaa nafasi ya juu kwenye group.

1. Matopeni FC
2. URA
3. Mwingine
4. Mwingine

Nusu fainali:- Msindi kwa kwanza wa Group B atacheza na mshindi wa pili wa group A

Yanga SC vs URA

Nusu fainali:- Msindi kwa kwanza wa Group A atacheza na mshindi wa pili wa group B

Azam FC vs Matopeni FC

(Hapa ndipo utakuwa ukomo wa Matopeni FC, hasa ukitia maanani kiwango chao huko Zanzibar ,na walipo cheza na baadhi ya vilabu vya zenji ambavyo Yanga SC hujipigiaga mengi mengi)





FAINALI:-

AZAM FC VS DAR ES SALAAM YOUNG AFRICANS SC.

Ukiuweka ushabiki pembeni na ukaulizwa nani atakuwa mshindi wa huu mtanange kwa kuzingatia ubora na perfomance ya hizi klabu mbili katika michuanno ya Mapinduzi Cup...Bila shaka chaguo lako litakuwa ni yule aliyeweza kutupia tupia mabao mengi mengi tangu mwanzo wa michuano.

YANGA BINGWA WA MICHUANO YA MAPINDUZI CUP 2017.

Baada ya hapo wenzetu wa Matopeni FC .....watarudi Dar kuendelea na Ligi .


wakiwa na Mawazo,Huzuni,Hofu, zilizozaliwa kwa kukosa Ubingwa wa Mapinduzi Cup watajikuta wwakipokea vipigo ambavyo vyenye kufanana na vile vya African Lyon na Prisons....

Huku wakitazama nyuma (wamuonapo Yanga SC) wanajazwa tena wasiwasi inayowapelekea kusarenda Usukani wa LigiKuu bara na kunyoosha mikono juu na kusema `Tumeshindwa, Nendeni nyinyi`.

Hapo ndipo Mabingwa watetezi na wa kihistoria wa Ligikuu Tanzania Bara watatwazwa Mabingwa kwa mara ya 3 mfululizo.

NB:- muendelezo wa huu uzi wa nini kitatokea upande wa Matopeni FC baada ya Yanga SC kutwaa ndoo utaendelea baada ya uhitimisho wa Kombe la Mapinduzi.
 
Mimi Simba lakini kwa kweli huu uzi unaninyong'onyesha haswa!jamaa mnazu wa yanga lakini katathmini vyema!wanasimba tusibishe tugombane na benchi la ufundi ili tuwe na matokeo ya kujiamini!wenzetu wantupua mibao kama hawana akili nzuri bwana!
 
Mimi Simba lakini kwa kweli huu uzi unaninyong'onyesha haswa!jamaa mnazu wa yanga lakini katathmini vyema!wanasimba tusibishe tugombane na benchi la ufundi ili tuwe na matokeo ya kujiamini!wenzetu wantupua mibao kama hawana akili nzuri bwana!

Vyema sana! Ila kwa sasa wamechelewa sana. labda wajiandae kwa ajili ya msimu ujao wa mwaka 2017/18
 
ha ha ha ha naina sasa mmeanza kuhangaikia la mapinduzi baada ya kuona ubingwa mwaka huu sio wa kwenu si mlisusa kipind fulan kushirk hili kombe
 
ha ha ha ha naina sasa mmeanza kuhangaikia la mapinduzi baada ya kuona ubingwa mwaka huu sio wa kwenu si mlisusa kipind fulan kushirk hili kombe
Mpaka ifikapo mwezi wa 5 kitu pekee ambacho mtakuwa mnajivunia nacho ni ubingwa wa vijana tu.

michuano ambayo sijui kama ina tija na manufaa mno kwenye vilabu vyetu.
 
Mpaka ifikapo mwezi wa 5 kitu pekee ambacho mtakuwa mnajivunia nacho ni ubingwa wa vijana tu.

michuano ambayo sijui kama ina tija na manufaa mno kwenye vilabu vyetu.
endeleen kufunga na kusali mbadilishiwe kile kifurush chenu cha siku ambacho kimegoma kuungwa mpaka leo
 
Haya mkuu subiri uaibike nafikiri utashindwa hata kujibu comments zetu

Eti wa Matopeni.. ....
Sawa subirini tuwaone wa kimataifa
 
Tathimini yako nzuri ila unasahau kua kila timu iliyocheza na simba tayari ilishajeruhiwa ivyo inakua na nafasi ya kujirekebisha ndo mana ata simba ushindi wake umekua wa tabu.juzi yanga alipata goli sita kwa jamhuri ila leo hawezi kuzipata kwa zimamoto ambao juzi walipoteza mbele ya azam.Mpira hauchezwi kwa hisia kaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom