Mapinduzi baridi ndani ya chama kongwe, iliyokuwa CCM Mpya ya mwendazake yafukiwa rasmi
Hakika sasa chama kikongwe chama dola kimefanya mabadiliko na kurudisha safu, makada na itikadi iliyokuwa imefukiwa na mwenyekiti mwendazake (revered) hayati (late) John Pombe Joseph Magufuli.
Yanayoendelea kimya kimya ndani ya CCM ni hatua ya kuondokana na wale walioonekana kama 'wageni ' na sasa wale waliokulia ndani ya chama sasa wamerudi na kuchukua hatamu.
Nini tutegemee kwa taifa kuhusu mabadiliko haya ya ndani kwa ndani ya chama kongwe ambacho kilikuwa na uvumilivu wa vyama vingine vingi vya siasa Tanzania tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Historia inaonesha mwalimu Nyerere aliyechagiza mfumo huo wa vyama vingi viwepo ingawa wahafidhina wachache ndani ya CCM waliuogopa.
Ali Hassan Mwinyi aliulea mfumo huo na kupokewa na Benjamin Mkapa na kisha jukumu hilo la kitaifa likamwendea Jakaya Kikwete. Mambo yalienda kwa kiasi mazuri baina ya mwaka 1992 mpaka 2015 ambapo ghafla kukatokea mkakati wa kuua vyama na mfumo mzima wa vyama vingi.
Mwaka 2015 aliposhinda urais kuoitia chama cha CCM na kisha baadaye kama desturi ya CCM mwrndazake hayati rais John Pombe Joseph Magufuli kujizatiti kwa kuwa pia meenyekiti wa CCM alianza harakati za kufuta mfumo wa vyama vingi na pia kuwaweka pembeni wenye CCM yao.
Mbali ya kuiathiri CCM na pia kwa kiwango kikubwa vyama vingine vya siasa kugandamizwa, chaguzi kuchafuliwa na wageni kukaribishwa katika iliyoitwa CCM Mpya ya Magufuli, kelele na mayowe yakaanza kusikika ndani ya chama dola kongwe cha CCM vipi waliokipigania, waliokulia ndani ya chama tangu jumuiya ya chipukizi ya CCM, UVCCM vyuoni na kisha kuwa watu wa makamo ndani ya CCM wakatupwa nje ya shughuli za chama na nafasi zao kupewa wasio wanasiasa na pia ni mamluki toka vyama vingine walionunuliwa kwa fedha wakawa sasa wanaendesha chama na serikali chini ya John Pombe Joseph Magufuli.