thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Loud and clearBernard Membe amekuwa akipitia nyakati mbalimbali za machungu makubwa kwake katika harakati zake za muda mrefu za kuitafuta Ikulu ya Chamwino. Mapigo hayo yamezidi kufifisha ndoto yake hiyo ya mchana ambayo amekuwa akiiota kila uchao.
Pigo la Kwanza: Hili pigo alilipata mwaka 2015. Ni dhahiri kuwa mwaka ule alikuwa ameshaanza hata kufanya rehearsal ya kuapishwa, na alikuwa ameshaanza hata kutembea kimapozi kama Rais kwani alikuwa na uhakika kwa asilimia nyingi kuwa angeweza kuwa Rais wa Tanzania. Pigo kwake ilikuwa ni Kamati Kuu ya CCM kumkata jina, na hivyo kumuondoa kwenye orodha ya majina ya Wanachama Watatu ambao majina yao yalipelekwa kwenye Mkutano Mkuu ili kupigiwa kura na hivyo kumpata Mgombea kupitia chama hicho.
Pigo la Pili: Hili pigo alilipata baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM. Baada ya kukosa nafasi hiyo, Membe bado aliendelea kuwa na imani kuwa mwaka 2020 atagombea nafasi hiyo. Matokeo yake ni kuwa alikamia sana hata akawa anavunja misingi waliyojiwekea kama chama, na hata mara nyingine akaonekana kuwa ni mtovu wa nidhamu. Hali hiyo ilipelekea chama kumvua uanachama wake, na hivyo likawa ni pigo lake la pili.
Pigo la tatu: Upinzani nao wote wamemkataa mchana kweupe. CHADEMA wamekataa kuungana naye, na hivyo kila chama kimeendelea na mchakato wa uchaguzi kivyake. Membe amebaki na ACT yake ambayo alihamia baada ya CCM kumtema. ACT-Wazalendo walimuahidi kumpa nafasi ya kugombea Urais kupitia chama hicho. Membe kipindi fulani alisema atakuwa tayari kugombea iwapo upinzani wangeamua kuungana na kumsimamisha yeye kama Mgombea wao. Ni dhahiri kuwa alijipa “Face Value” kubwa sana wakati wapinzani aliotaka waungane wanamuona kuwa ana “Actual Value” ndogo sana. Membe alitamani sana Chadema wakubali kumuunga mkono yeye; hivyo kitendo cha Chadema kumtema na kumteua Lissu kuwa Mgombea wao na Salum Mwalimu kuwa mgombea mwenza limekuwa ni pigo jingine kwa ndugu yetu Membe.
Yajayo yanafurahisha, Uko Tayari?