Mapigano ccm na chadema yatia dosari kampeni maswa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapigano ccm na chadema yatia dosari kampeni maswa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by SpK, Oct 26, 2010.

 1. S

  SpK Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  MAPIGANO CCM NA CHADEMA YATIA DOSARI KAMPENI MASWA


  Kampeni za Ubunge katika majimbo ya Maswa Magharibi na Maswa Mashariki ambazo ziliingia dosari na kusimama kwa muda tangu Jumatano iliyopita, kufuatia vurugu, uhasama na mapambano kati ya washabiki wa Chama cha Mapinduzi [CCM] na Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA], zilizosababisha kifo cha mtu mmoja na wengine watano kujeruhiwa vibaya kwenye Mkutano wa CHADEMA katika kijiji cha Kizungu, Jimbo la Maswa Magharibi zimeanza tena baada ya hali ya uhasama uliozuka kati ya vyama hivyo viwili Wilayani hapo kudhibitiwa.

  Aliyefariki kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali katika mtafaruku huo, ametambuliwa kuwa ni Steven Kwilasa [26], dreva wa mgombea wa Jimbo kwa tiketi ya CCM, Bw. Robert Kisena.

  Kufuatia mtafaruku huo, uhasama wa wanachama wa vyama hivyo ulienea Wilaya nzima, huku kila upande ukilaumu upande mwingine kwa vurugu hizo, na kuahidi kulipiza kisasi, na hivyo kufanya Jeshi la Polisi Wilayani humo kuimarisha ulinzi katika mji wa Maswa [Maswa Mashariki] na mji mdogo wa Malampaka [Maswa Magharibi] ili kuzuia mapambano mengine kuibuka katika maeneo hayo.

  Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Daudi Siyasi, amesema, kufuatia ghasia hizo, mgombea Ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. John Magalle Shibuda, ambaye alikuwa akihutubia siku ya tukio, alikamatwa na kushikiliwa kwa siku tatu na Polisi kwa mahojiano ili kujua kama anahusika na ghasia hizo au la; na kwamba ya awali inaonyesha kuwa hahusiki na ghasia hizo, na hivyo ameachiwa kwa dhamana wakati upelelezi zaidi ukiendelea.

  Vivyo hivyo, Polisi Wilayani Maswa, ilimwita kumhoji, Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia tiketi ya CCM, Bw. Robert Kisena, sababu ya wafuasi wake kuvamia eneo la Mkutano wa CHADEMA siku hiyo; lakini katika hatua ya kushangaza, wakati Kisena akiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Maswa, Mrakibu wa Polisi, Peter Ndunguru, Mgombea huyo alimpiga ngwara na mateke na kumwangusha chini Afisa huyo Polisi na kuondoka bila kukamatwa wala kuhojiwa na hakukuwa na juhudi zozote za Polisi kufuatilia matukio hayo mawili dhidi ya Mgombea huyo, hadi siku tatu kupita alipoitwa tena Polisi na kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana.

  Na katika hali inayoonyesha vyombo vya dola kutoa hukumu mapema ya upande mmoja, kwa njia ya kukomoa juu ya ghasia zilizotokea, Jeshi la Polisi na vijana wa CCM Wilayani hapa, Alhamisi na Ijumaa iliyopita, lilianzisha Kampeni kabambe ya kung’oa mabango, kuchana picha, bendera na matangazo ya Wagombea wa Ubunge na Udiwani kwa tiketi ya CHADEMA katika maeneo ya mji wa Maswa [Maswa Mashariki] na mji mdogo wa Malampaka [Maswa Magharibi] kwa kile kinachotafsiriwa na wananchi wengi kuwa ni ushawishi wa CCM kwa Walinzi hao wa usalama na amani kuihujumu CHADEMA.

  Wakiongea kwa sharti la kutoandikwa majina, wananchi hao wamelalamikia ukandamizaji huo, na kitendo cha mgombea wa CCM kumpiga Mkuu wa Polisi Wilayani humo lakini bila kuchukuliwa hatua mara moja kuwa ni upendeleo maalumu kwa CCM dhidi ya kambi ya upinzani.

  Akisimulia juu ya ghasia zilizotokea kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini, kwa hofu ya kufuatiliwa na vyombo vya Usalama, mmoja wa wakazi wa kijiji cha Kizungu ulipofanyika mkutano wa CHADEMA siku ya tukio alisema, CCM ndio wa kulaumiwa kwa uchokozi dhidi ya wenzao wa CHADEMA. Alidai kuwa, siku hiyo, wakati Shibuda wa CHADEMA akiwa katika hatua za mwisho mwisho kumaliza mkutano wake, alituma washabiki wake kwa gari la matangazo kwenda Kata ya jirani ya Shishiyu kuandaa mkutano mwingine. Wakiwa mita 300 tu toka Shibuda alipokuwa akihutubia, huku wakiondoka, waliona gari la mgombea wa CCM likija mkutanoni kwa kasi ya kutisha; na katika kujaribu kulikwepa, gari la CHADEMA liliingia kwenye tuta. Ndipo washabidi wa CCM waliposhuka na kuanza kuwashambulia kabla ya wao nao kujibu mapigo huku wakipiga kelele na kuomba msaada kutoka kwa wananchi, jambo lililomfanya Shibuda asitishe hotuba na kwenda kwenye tukio akiwa na Polisi.

  Inaelezwa kuwa, wakati haya yakiendelea, gari lingine la Bw. Robert Kisena wa CCM lilionekana likija kwa kasi kubwa kwenye uwanja wa mapambano kutoka upande wa pili, likiwa limebeba mashabiki wengine wenye silaha za uvamizi na nondo kuashiria kwamba uvamizi huo ulikuwa umepangwa. Hata hivyo, vijana wa CHADEMA wakisaidiana na Wananchi, waliweza kuwadhibiti vijana wa CCM wakatimua mbio, lakini mmoja wao, hayati Steven Masele alikuwa ameumizwa vibaya na kufariki alipofikishwa hospitali ya Wilaya ya Maswa.

  Wiki mbili kabla ya tukio hili, mfuasi mmoja wa CHADEMA mkazi wa mji mdogo wa Malampaka, aliyefahamika kwa jina moja tu la Ngolo, alijeruhiwa vibaya na wafuasi wa CCM kwa kukatwa mapanga baada ya kukaidi kushusha bendera ya CHADEMA aliyopeperusha juu ya paa la duka lake, sakata linalioelezewa kuwa na baraka za Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Maswa. Na katika tukio la juzi la uhasama huo wa kisiasa, mwananchi huyo amechomewa duka lake na nyumba kulipiza kisasi cha tukio la Kizungu.

  Kwa wiki tatu mfululizo za Kampeni za uchaguzi, Makada Vijana wa CCM, maarufu kama “Green Guards” wametunga na kueneza wimbo wa ukakamavu, wakipita sehemu mbali mbali wakiimba “Wapinzani wako wapi; waje tuwapige, tuwachanechane”, hali inayoashiria dalili za kuvunjika kwa amani iwapo Viongozi wa ngazi za juu wa vyama hivi hawataingilia kati.

  Wachunguzi wa siasa Wilayani hapa wanahusisha ghasia zinazotokea na siasa chafu za “maji-taka”, zikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, ambaye pia ni mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Maswa Mashariki, Peter Bunyongoli; na Katibu Mwenezi wa Wilaya wa Chama hicho, Jeremiah Mange Shighala, maarufu kwa jina la “Makondeko”, ambapo watu wengi wanaona, “uropokaji” na tabia yao isiyoonyesha utu uzima, ustaarabu wala matarajio ya jamii, umeipa nguvu mpya na turufu kambi ya upinzani na uwezekano mkubwa kwa CCM kupoteza majimbo yote mawili.

  Wakati wa ziara yake Wilayani hapa Ijumaa iliyopita kufuatia ghasia hizi, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Yusufu Makamba, alielezwa na WanaCCM, hali halisi ya siasa Wilayani Maswa na chanzo cha CCM kukosa ushawishi kwa wananchi, ambapo naye alisikika akitamka hadharani akiwaelekea Shigala na Bunyongoli, akisema: “Wewe [Shigala] ndiye chanzo cha vurugu, migogoro na fujo zote katika Wilaya hii, tunajua; punguza maneno na uropokaji”.

  Na kwa Bunyongoli, katika hali na aina fulani ya kumnadi kwa utani, Makamba alisema: “Mchagueni huyu, licha ya kuwa na sura mbaya [kichama?] lakini ni kada wetu”.

  Marehemu Steven Kwilasa alizikwa Jumapili iliyopita katika kijiji cha Badabada, nje kidogo ya mji wa Maswa. Waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Yohane Balele; Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, Katibu wa CCM Mkoa, Mohamed Mbonde na mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete, ambaye ni rafiki mkubwa wa Mgombea wa Jimbo la Maswa Magharibi, Robert Simon Kisena pia ni mnunuzi, mchambuaji na mfanyabiashara wa pamba Mkoani Shinyanga ambako inadaiwa baadhi ya vigogo wa kitaifa ni wabia katika Viwanda vya kuchambua pamba.

  Katika hili iliyoonyesha Uongozi wa CCM Maswa kujali zaidi ujio wa Ridhiwani kilioni hapo, kwa nia ya kutumika kama kete katika Kampeni za uchaguzi kuliko Uongozi wa CCM Mkoa na uwepo wa Mkuu wa Mkoa, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Maswa, ambaye pia ni mgombea Udiwani wa Kata ya Zanzui, Jeremiah Mange Shighala, alimtambulisha kwanza na kumkaribisha kuongea kabla ya Viongozi wa Mkoa na Wilaya, lakini Ridhiwani alibakia kimya huku amekaa, kwa kubaini kuwa protokali ilikuwa imekiukwa.

  Na alipopewa nafasi ya kuongea baadaye, mwana huyo wa Rais aliwataka Makada wa CCM Wilayani humo kuwa watulivu kwa kuendesha Kampeni za kistaarabu na kuyaona yaliyotokea kuwa ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu ambaye ndiye anayepanga namna kila mtu atakavyopita hapa duniani.

  Katika hatua nyingine, taarifa za uhakika toka Kikao cha ndani kati ya Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba na Viongozi wa CCM Wilaya ya Maswa, zimeeleza kwamba Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya hiyo Mary Kitundu, aliitwa kikaoni na kuelekezwa kuitisha Kikao cha Kamati ya Maadili ya Uchaguzi kujadili tabia ya CHADEMA ili ikiwezekana, ipendekeze kwenye Tume ya Uchaguzi ya Taifa [NEC] kienguliwe katika uchaguzi Wilayani humo. Imeelezwa pia kwamba, katika Kikao hicho, Makamba aliwahamasisha vijana wa CCM wafuatilie na kushinikiza Shibuda abakie rumande mpaka uchaguzi utakapomalizika, na vijana hao walikwenda kituo cha Polisi wakitaka kuthibitishiwa kuwekwa ndani kwa Shibuda.

  Akihutubia wananchi kwenye Uwanja wa CCM wa Kambarage mjini Shinyanga, Ijumaa iliyopita baada ya kutoka Maswa, Makamba alisema, CHADEMA hakiwezi kukwepa lawama kwa vurugu na mauaji ya Mwana-CCM, yaliyotokea Maswa, kauli iliyofanya wananchi wagune na kupiga kelele kuashiria kwamba haikuwa kweli.

  Katika hali inayoendelea kushangaza wengi katika uchaguzi huu, nguvu ya dumuzi wa vyama vya upinzani imezidi kutikisa katika Mkoa huu ambao hapo mwanzo ulijulikana kama “treni ya ushindi” kwa CCM kitaifa. Ukiondoa wagombea wa majimbo ya Kahama, Msalala, Kishapu, Solwa, Kisesa na Bariadi Magharibi, Wagombea wa majimbo yaliyobaki kwa tiketi ya CCM, watatakiwa kutumia nguvu ya ziada ili kuyaokoa majimbo hayo yasinyakuliwe na upinzani.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wakome CCM natamani kipigo hicho angepata makamba na kuuwawa na wananchi wenye hasira kali
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Dah, Kigogo bana! Taratibu mkuu. Naona hukopeshi kabisa.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yote haya yanatokana na kutokuwapo kwa haki kunakofanywa na vyombo vya dola. Nimepata habari sasa hivi kutoka Arusha kwamba ingekuwa Takukuru inatumia haki, saa hizi yule Mama Burian angekuwa anajibi kesi mahakamani za kugawa fedha anazoletewa na Lowassa kila siku. Takukuru wanapuuza kila tukio wanalopelekewa kutoka kwa wananchi walikouwa macho. Pamoja na hayo yote, wana-Arusha wameamua kumpa mama huyo buriani ya kuwania ubunge.

  Katika hali ya namna hii, vurugu zinaweza kukosekana?
   
Loading...