Naombeni ushauri kuhusu mpenzi wangu

Dasca

New Member
Apr 13, 2021
3
8
Ndugu zangu naomba ushauri

Mimi ni kijana ambaye nina miaka 23 naishi Canada.

Kuna kipindi nilikutana na dada fulani FB huyo dada tuliwai kusoma wote shule kabla sijaenda Canada.

Sasa tulivyo kutana na huyo mwanamke ilikuwa 2019 tukaanza mahusiano naye tukapendana sana akanipenda sana na mimi nikampenda sana.

Mpaka ilifikia hatua pesa zangu za mwaka nilizo pokea huku Canada milioni 34 nikanunua nyumba Dar es salam, nikawahamisha kutoka kijijini kwao nikawapeleka Dar yeye na ndugu zake, nikamfungulia saloni ya kike pamoja na restaurant na nikawa namsaidia kwenye mahitaji mengine kila mwezi nikawa namtumia laki 4 za kitanzania.

Sasa ikafika kipindi 2020 nikasema niende kumuona mwanamke wangu. Mimi kufika tu familia yake wakanikatalia eti hauja weka Mahari kwa hiyo haurusiwi kuwa na mtoto wetu.

Nikapiga simu Canada wazazi wangu wakanitumia shilling milioni 5 nikaenda kuweka kwao wakakataa eti izo ndogo mtoto wetu bila dolar 15000 hatoki hapa.

Nikawaambia wazazi wangu wakasema hapa tuna dollar 7000 nikaomba msaada kwa marafiki zangu wakanisaidia nikapata dollar 12000.

Nikaenda kuweka Mahari nikawaambia nataka kumchukuwa mke wangu wakakataa eti huwezi mchukua mpaka hizo zingine umalize nikakubali masharti yao.

Sasa cha ajabu huyo mwanamke nilivyoonana naye mara ya kwanza akaanza kunitukana kuniambia mimi niko sawasawa na mtoto wao wa mwisho yaani ana nizidi kimo kidogo tu. Nikamwambia kwanini una sema hivyo nikamshauri akanisikiliza.

Sasa akabaki kunidharau pale nitakapo mkasirisha ananitukana
kuna kipindi aliniambia eti mimi ni kamwanaume gani hawezi eti kunitambulisha kwa marafiki zake eti mimi ndio mume wake yote hayo nilisikia nikamsamahe kipindi kingine alinikosea kuniambia nilivyo mfupi ndivyo akili yangu ilivyo fupi nikmsamehe.

Sasa nilivyo rudi nyumbani nikaja na wazo la kumleta huku sasa na nilikuwa nafanya kila nikikumbuka dharau zake pesa nilizo andaa kupambania kuja kwake huku nanununua pombe yangu.

Nilimwambia tuachane na ndani ya nyumba yangu watoke na biashara zangu nafunga akanijibu kwa jeuri eti yeye ni mrembo hawezi kosa wa kumuoa sasa cha ajabu siku hizi ananiandama ananiambia nimsamehe ule ulikuwa utoto sasa hivi amekua kwa hiyo hatorudia kosa lake.

Sasa swali anayekupenda kweli anaweza kukuonyesha dharau na kiburi?
 
Hapana mkuu, toka hapo....huyo msichana na ndugu zake ni wezi....inaelekea hujiamini, huamini unaweza kupata mpenzi tena ndio maana uko desperate kujenga uhusiano hewa, jiamini mkuu, kila pipa na mfuniko wake,utapata anayekupenda na ufupi wako....ukiendelea na huu uhusiano jua utakaribisha shari katika ndoa yako, haitakua na amani ooohhhhoooo atakuletea hadi wanaume ndani..
 
Uandishi wako mkuu umenitatiza sana ila hivyo hivyo hatimaye nimeelewa.

Miaka 23 bado uko mdogo sana. Bado upo kwenye kipindi cha kujifunza na kuyaelewa maisha pamoja na hekaheka zake yakiwemo mapenzi. Na huyu binti nadhani naye bado mtoto kama wewe na hivyo mmekutana wote wachanga si ajabu hata hamuelewi mnachokitaka bado. Binti bado hajafika kwenye umri wa kutulia na ataendelea kukusumbua tu.

Pengine atakuja kuanza kutulia akifikia 26+ huko baada ya kufaidi ujana wake sawasawa japo pia wapo ambao huwa hawatulii. Na anakudharau sana na huo ufupi wako.

Umewekeza sana katika mahusiano haya na kama unaona huwezi kuachilia basi pambana. Kufa hutakufa ila cha moto utakiona. Ningekuwa wewe ningeanza upya japo hili ni jambo gumu ajabu. Pole sana
 
Hapana mkuu, toka hapo....huyo msichana na ndugu zake ni wezi....inaelekea hujiamini, huamini unaweza kupata mpenzi tena ndio maana uko desperate kujenga uhusiano hewa, jiamini mkuu,kila pipa na mfuniko wake,utapata anayekupenda na ufupi wako....ukiendelea na huu uhusiano jua utakaribisha shari katika ndoa yako, haitakua na amani ooohhhhoooo atakuletea hadi wanaume ndani..
Na akicheza wanaweza hata kumrestisha in peace akizubaa.
 
Asante ndugu yangu dah
Ila mbona anaonesha dalili kama ananipenda hivi.

Na cha ajabu uo ufupi anao ni tukana yeye si mrefu kwangu sema kako kembamba mimi Nina mwili kidogo.
In short huyo hakupendi, chukua mali zako fukuzia mbali huyo acha mazoea naye. Tafuta mwingine, huyo anakuigizia.
 
Kimbia tena na kimbia kabsaaa huyo ni shetan hapo anataka kukuteka ili akuangamize kabsa
 
ndugu zangu naomba ushauri

Mimi ni kijana ambaye nina miaka 23 na ishi Canada

Kuna kipindi nili kutana na dada fulani fb uyo dada tuliwai kusoma wote shnyesha dharau na kiburi?
Wewe exposure yako ya huko mbele bado haujafuta upumbavu wako
 
Sijui ni sababu gani haswa inanifanya niiamini hii stori... Na nataka niendlee hivi hivi kutokuiamini


MIMI NI KAKA YAKO UKINIZINGUA TUNAZINGUANA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom