Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mbunge wa CCM, Dec 21, 2009.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  1.
  Ndugu nipeni kilinge, ninalo la kuwaliza,
  Lazima sasa niringe, kwalo ninalouliza,
  wambea nao wachonge, beti zote kumaliza
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  2.
  Ni wazi yanapoanza, shurti wawili kughani,
  Wa kwanza akiwa mwanza, mwenziwe akiwa pwani,
  mapenzi hayataanza, hadi wawe kizioni,
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  3.
  Zamani mi nilidhani, mapenzi ni kitandani,
  Kumbe sikuwa makini, mapenzi kuyabaini,
  Sasa nimeamini, yaweza kuwa penuni,
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  4.
  Kama hawa wawili, bado kutana bayana,
  Nini kitawabadili, kama mmoja atakana,
  Kwamba hakumdahili, mwenzie bali hiyana,
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  5.
  Na hisia zi wapi, pale penye kuwadi,
  Kitanda kina makapi, raha nayo si zaidi,
  Hata itafunwe pipi, jivu halina uudi
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  6.
  penzi lisilo la ndani, baya kuliko kuzini
  Maungo yahisi nini, moyo u-kizuizini,
  Akili iko mtegoni, hisi zi mtandaoni,
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  7.
  Wa-tatu awapo kati, hapo hapakosi shaka,
  Hata uwe mkakati, mapenzi hutayataka,
  Tena yaliyo thabiti, si yale yenye mashaka,
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  8.
  Najua nimekukwaza, wewe uliye kuwadi,
  Sifazo nimeziviza, sasa wataka kunadi,
  Hata bila ya viza, nchi ukaifaidi,
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  9.
  Uzalendo u wapi, enyi wenye makuwadi,
  Nchi mwaipelekapi, huku mwadai waridi,
  Sie tulitoe wapi, kila kitu mmenadi,
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?

  10.
  Mwasema hamrejei, mwataka heshima mbele,
  Heri tuikose bei, nyie muishi milele,
  Mwisho tutoke nishai, kama sie misukule,
  Mapenzi yenye kuwadi, kwa vipi yawe ya moyo?
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  loh,

  shairi safi sana mkuu, embu baelezee hao makuwadi, kina lyautwanga!
   
Loading...