Mapenzi yanauma sana, niliwaza mpaka kujiua kisa kupenda

KALINZI NYUMBANI

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
1,658
1,157
Wakuu salama!.

Nilikuwa siku zote nikimuona mtu analia kwa sababu ya mapenzi nilimcheka na kumdharau.Lakini kwa haya yameyonikuta sihitaji kusikia neno mapenzi katika masikio yangu maana niliwaza kujiua kisa haya mapenzi.

Mnamo mwaka 2008 nilitokea kumpenda binti tulie kuwa nae na utofauti wa kidini.Kiukweli nisime ukweli nilimpenda huyu binti kiasi kuwa nilikuwa siambiwi wala sisikilizi lolote lile nililoambiwa na mtu mwingine.Nilimtongoza zaidi ya mwaka ndipo akakubali kuwa na mie.

Hakika mwanzo wa mapenzi yetu tulipendana sana,tena tulipendana zaidi ya neno lenyewe kupendana.Mie kipindi hicho nilikuwa nipo naenda advance ye alikuwa yupo form four.Kwa bahati nzuri nae alipomaliza form four alifauru akachaguliwa shule moja huko Tanga.Kipindi hicho tulikubaliana tuwe tunawasiliana siku za mapumziko jumamosi na juma pili tu.Hakika tuliendelea na mahusiano yetu.Na nikikili kuwa nilimpenda sana huyu binti kiasi kuwa nilikuwa muaminifu kwa kila kitu juu yake.

Alipofika form six 2011 kipindi hicho mimi nipo mwaka wa kwanza katika chuo kimoja wapo hapa Dar,alinipigia simu nakudai anaomba tuachane hakika niliumia sana zaidi ya sana maana nilikuwa naona yeye ndio mwanamke wa ndoto yangu.Nilimbembeleza sana asiniache lakini aligoma.Akidai kuwa haoni future ya mapenzi yetu kulingana na utofauti wa dini zetu.Baadae nilikubaliana nae lakini baada ya miezi kama mitatu akanitafta nakuomba turudiane.

Hapo ndipo nilipofanya makosa kwa kukubali kurudiana nae.Kiukweli alilia sana mpaka jamaa zangu wakinisihi nimsamehe ili tuendelee na uhusiano wetu.Kiukweli nilikubali kumbe mwenzangu alikuwa na agenda ambayo ilimsukuma kurudiana na mie lakini mie sikuifahamu.

Baada ya yeye kuja chuo hapa hapa Dar lakini chuo tofauti na mie.Alinionyesha upendo wa hali ya juu kiasi kwamba nilianza kumuamini tena nikisukumwa na upofu wa upendo nilio kuwa nao juu yake.Tulirudia kulizungumza suala la dini na akakubali kuwa atabadili dini awe dini moja na mie na hapo tukuanza kuwa tunaenda sali nae mara moja moja.

Kulingana na uchumi alio kuwa nao kwao na kulingana na course aliyokuwa anasoma alipokuja chuo hakubahatika kupata mkopo.Nyumbani kwao walikuwa wanamlipia ada tu mambo mengine yote juu yake niliyabeba mie.Nakiukweli kipindi hicho nilifight sana nikaanza kufanya bisness ili mchumba wangu asome kwa amani.Of course mishe zangu zilienda vizuri nikawa napata faida nzuri tu.Maana nilikuwa natoa mchele kyela nauleta dar nawauzia mama ntilie.Mchele mwingine nilikuwa nautoa kahama na iliniradhimu kuajili vijana wawili walio kuwa wanafanya hio kazi dhen tunalipana.

Kiukweli binti wawatu alisoma kwa amani na mwaka jana tulibahatika maliza chuo.kwakuwa yeye alikuwa anachukua course ya miaka mitatu mie minne tulimalizia pamoja.Baada ya kumaliza kwakuwa mie nilikuwa nimeshajipanga ndani alikuja tukawa tunaishi nae gheto kwangu na mimi sikutafta ajira niliona bora niendelea na biashara zangu tu.

Baada ya kukaa nae gheto miezi miwili kuna jamaa yangu alinipigia simu ikidai kuna private sector fulani wanatafta wafanyakazi,Ikabidi nimwambie na yeye aombe lakini alikosa baada ya hapo nikaanza kufatilia katka hio kampuni HR wapale akadai kuna nafasi moja imebaki lakini nimpe chochote ndio huyo binti aingie.Kiukweli nililipa 1.5M ili huyu niliekuwa nafikili nimke wangu mtarajiwa apate kazi na kiukweli alipata kazi nzuri tu.Yenye malipo ya laki tano kwa mwezi.

Sasa baada ya kupata kazi alinibadilikia sana mpaka nikaanza kuduwaa kuwa ni yeye au ni mwingine.Tulikuwa ndani tunasaidizana baadhi ya kazi kama kufua,kupika,kwenda some time kuchota maji.Nikijua kuwa namuomyesha upendo wa dhati mwenzangu ili ajue nikias gani nampenda na kumjali.Lakini alianza badilika nikimwambia usiku apike hataki kupika,afue hataki wekend ikifika nikimwambia tukachote maji hataki niliendelea kumvumilia kama mwezi hivi.

Na tulikuwa tumepanga mwaka huu mwezi wa sita twende kwao ili tufanye mpango wakufunga nae ndo,ingawa kwao walikuwa wanajua kama tayali anaishi na mtu nakashabadili dini.Baada ya kufika mwezi wapili mwishoni mwaka huu,niliondoka kufata biashara zangu mkoani niliporudi nikamkuta hayupo nikimpigia simu hapokei.Ikanibidi niende kazini kwao nikamkuta nikaongea nae akaniambiwa kuwa ameamua tuachane hawezi olewa na mimi.

Kiukweli moyo wangu uliniuma sana nilihisi dunia yote kama ipo juu ya kichwa changu.Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana,hamu yakula sikuipata mawazo namie,mie na mawazo.kiukweli niliangalia nikiasi gani nimeinverst kwa huyu binti ili aje kuwa mke wangu nilichoka.Usiku nikilala nilikuwa nabubujikwa na machozi siamini kama kweli huyu binti kaniacha ,muda mwingine mpaka niliwaza sijui nijiue lakini nilishindwa kiukweli mapenzi yanauma asikwambie mtu.

Sasa mwezi kama nawiki mbili tangu aniache ndio naanza kuhisi akili yangu inarudi normal.Nakiukweli sasa ivi nmeanza kuwachukia wanawake wote mpaka baadhi ya ndugu zangu wakike.Hili tatizo ndio linanisumbua na sijui naliondowaje kichwani mwangu.Muda mwingine nawakasirikia watu bila sababu hii hali kiukweli inanisumbua na sipendi iendelee.

Nikiusikia wimbo wa DIAMOND-nalia na mengi nahisi kama nimeimbiwa mie vile.Nahitaji msaada wenu hii hali niiondoaje.

Nawasilisisha kwa unyonge.
 
Sasa mwezi kama nawiki mbili tangu aniache ndio naanza kuhisi akili yangu inarudi normal.Nakiukweli sasa ivi nmeanza kuwachukia wanawake wote mpaka baadhi ya ndugu zangu wakike.Hili tatizo ndio linanisumbua na sijui naliondowaje kichwani mwangu.Muda mwingine nawakasirikia watu bila sababu hii hali kiukweli inanisumbua na sipendi iendelee.
You are not allone the friend of mine, mie hapa sijajua tu wapi nitapata wanasaikolojia ningeenda walau nipate counselling.
 
Mkuu tatizo linalokusumbua ni moja Hutaki kuiruhusu akili yako kumuacha huyo mwanamke kama ungeweza kuruhusu akili yako kufikilia kuwa duniani mwanamke sie yeye pekee na wewe sio wa kwanza kufanyiwa hivyo bila shaka ungemsahau na ungehamishia hizo hasira/mawazo kwenye kuwekeza zaidi katika biashara zako.
Pole sana chukulia umeteleza tu,maisha yaendelee tena kwa umakini wa kuangalia pale ulipoteleza na sio ulipoangukia.
 
Pole sana mkuu... Kisicho rizki hakiliki. Maumivu ya mapenzi yanapita msiba. Tunaumizwa na kuumizana ila sio mwisho wa ndoto zako

Ndoto ulizokua nazo juu yake utampata anaestahili na kuhamishia ndoto kwake,na utafurahia maisha tena...

Amini mwanamke wa maisha yako yupo,kazi yako ni kuomba Mungu akukutanishe nae na uwe mvumilivu kusubiri majibu....
 
kipindi hiki cha maumivu afanye nini sasa?maana hata tumbo ukihara hospitali unapewa dawa ya maumivu na yakuponyesha
 
Mwenewachu Kalinzi kwetu, mshukuru Mungu kwa hilo, tena una bahati sana. Yaani vituko alivyokuwa anakufanyia ulikuwa bado hupati akili ya kujiuliza kuhusu mabadiliko ya tabia zake?

Kama ungekuwa umeshamuoa kabisa ingejuwaje? Mshukuru Mungu pia kuwa umeweza kumsaidia kimaisha hadi hapo alipofika, sasa muhesabu kama umemsaidia nduguyo, usijutie kamwe msaada wako kwake, huo ni muhuri muhimu kuwa uliwahi kuhangaikia maisha yake na kuwa ktk mafanikio yake kuna nguvu zako.

Vv
 
Asante ndugu yangu.
 
Pole sana mkuu... Kisicho rizki hakiliki. Maumivu ya mapenzi yanapita msiba. Tunaumizwa na kuumizana ila sio mwisho wa ndoto zako

Ndoto ulizokua nazo juu yake utampata anaestahili na kuhamishia ndoto kwake,na utafurahia maisha tena...

Amini mwanamke wa maisha yako yupo,kazi yako ni kuomba Mungu akukutanishe nae na uwe mvumilivu kusubiri majibu....
Asante sana Mkuu.
 
kipindi hiki cha maumivu afanye nini sasa?maana hata tumbo ukihara hospitali unapewa dawa ya maumivu na yakuponyesha
Ahamishie mawazo yake kwenye mengine,awe bize na kazi,afungue miradi/biashara mbalimbali ajikip bze kuisimamia.

Kifupi aelekeze mtazamo wake kwenye maendeleo yake,aweke mikakati miaka miwili ijayo angependa kua position gani.

Ajichanganye na watu mbalimbali wenye mtazamo negative bila kusahau ibada. Na akaonane na wanasaikolojia pia
 
Back
Top Bottom