Mapenzi yanauma sana ndugu zangu, kamwe usimcheke mtu kama bado hayajakukuta


Myahudi Jr II

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
3,688
Points
2,000
Myahudi Jr II

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
3,688 2,000
Habari za kazi Ndugu zangu natumai mambo yanaenda salama Salimini

Yapita miezi sasa tangu niachane na mwanamke(girlfriend) niliyekua nampenda sana sana, nakiri wazi nilikua nampenda mno, naweza sema ndio alikua mwanamke wangu wa 1(first ever) kuwa nae kwenye mahusiano yaliyo siriazi ambayo ningejua yangezaa ndoa, sijawahi kua na “mahusiano na mwanamke” yeyote hapo kabla ”nieleweke hapa” yaliyo siriazi na kujihusisha na mapenzi kwangu hakikua kitu nilichokipa kipaumbele sana sikutaka kabisa kuchezea moyo wa mwanamke yoyote chini ya jua hili kwakua niliamini “what goes around, comes around” kama sio kwangu basi kwa watoto wangu hata kizazi cha nne, sikutaka hili litokee kabisaa.

Nakiri wazi, binti huyu nilimuhudumia chochote kilicho ndani ya uwezo wangu, daaaaaahhh mapenzi bwana yaache tu, nilifanya hilo kwa moyo wangu wootee, napenda kujali sana, sikutaka ajione yupo mpweke, I tried my best kwakweli, we had fun sehemu mbalimbali(hapa nikipita haya maeneo kumbukumbu zinarudi) mf. Tulikua tunaenda pale “lifepark” Mwenge kutembea na kupata juisi, na ndio njia yangu nayopita sasa,nikifika pale nayakumbuka yale nasema hakika upendo una nguvu.

Nakiri wazi tuu, sijui kama ndio kulia kwenyewe au vipi, machozi yalikua yanabubujika kama chemichemi asee, sijui yanatoka wapi, najitahidi hapa na pale lakini wapi, mapenzi yanauma ndugu zangu, nilikua napumua(exhale) ya moto balaa utadhani ndani nimewashwa jiko la mkaa (jiko la mkaa likiwaka Sanaa huwa linatoa kama miali flani hivi) ndiyo hali nilokua nayo(nashindwa kuielezea vizuri).

Mwanaume sikutamani hata kula, chakula hakipiti, nikiweka kijiko mdomoni naona kama umeniwekea mawe ya kg100, hata harufu ya chakula tu sikuitaka iwe karibu yangu, nilikaa siku 5 bila kutia chochote mdomoni, maana muda wote nilikua nimeshiba tu (hii hali sijui inakuaje wadau, yaani husikii njaa) nilikonda ndani ya wiki tuu, wasiojua walinishangaa sana, niliuchuna kama sijui, nakumbuka nilienda kumuomba ruhusa HR ni mgonjwa aisee aliponiona tu alisema “wewe nenda nitashughulikia kila kituu katibiwe mwanangu nendaaa” kumbe ni mapenzi.
Nisifiche, ilibidi nitundikiwe dripu za Sukari kwa kua sijala kitu chchote kile angalau mwili upate nguvu, japo nilipishana sana na wale watu wa afya, nilisema uongo wangu woote, nikawawin, japo najua walinipiga kwenye kuandikisha pesa ya dkumuona daktari, machupa ya madripu yale, sikujali.

Nilidumbukia mzima mzima, kichwa, kiwiliwili, miguu pamoja na moyo woote, wanawake bwanaa, hivi mpendwaje nyie watuu, unapata mtu aliye siriaz na wewe kwenye kila kitu lakini badooo tuu, yaani nimeshindwa kuwaelewa kabisaa, labda sikua najua ulimwengu wa mapenzi unavoenda.

Kwa umri wangu 27yrs nilikua sijawahi kuingia kwenye mahusiano, nilipoingia sikua na jua kuna kuumizwa, nakumbuka sana nilikua nasoma thread za watu humu nacheka sana, nasema haya mambo yanawezekanaje, nakumbuka kuna MwanaJF alijiua kwa kunywa sumu kule Mbeya mkewe alikua anafanya kazi idara ya maji aisee nilimshangaa sana yule baba nikadiriki kusema “dunia ina wanawake wote hawa anajiua kwa sababu ya mapenzi” Omba yasikukute, yaani mimi kipindi kile hata ungeniletea sijui UWOYA, WEMA, LULU aisee nisingeweza hata kuwataka ningewaona kama wanaume wenzangu, yaani nilikua namtaka yeye tuu, sikuona mwanamke mwingine Zaidi yake. Love is wicked kwakweli hapo ndipo nilipouelewa wimbo huu vizuri sana.

Siku zikapita miezi ikasogea maumivu yapungua nikaweza kula na kuinuka tena, ila alieumwa na nyoka hata jani huliogopa, sina Imani na hawa watu tenaa, moyo umekufa ganzi kwakweli, nguvu ya kuoa imepotea kabisaa, japo nahitaji kuoa kabla sijafika 30yrs, unajua siwezi kuwa “playboy” namaanisha siwezi kuhudumia wanawake wawili, SIWEZI…SIWEZI, bora niwe single tu.

Jana nilikua napitia thread zoote za walioumizwa, nilikua nacheka sana, unaweza ukaona kama yanafurahisha ila mtu unakuwa haupo vizuri mentally ndio maana unakuta mwanaume analalamika sana na anaonekana kama chizi maarifa flani hivi.

Kuna memba humu anaitwa lost id anatoa ushauri sana japo unaweza kumuona kama amechanganyikiwa ila jamaa anaongea facts sana juu ya mahusiano, anasema “mwanamke usimpe moyo wako, mpe pesa ila sio moyo” hapa mimi nilimpa vyote pesa na moyo, ile Burn niliokua naifeel aisee anajua Mungu tu nadhani.

Nawashukuru Wachangiaji woote wa thread mbalimbali za watu walioumizwa, japo zinasaidia 10% tu, zilizobaki ni MUDA tu ndio utakaoponya maumivu hayo.

Mapenzi yanauma, mapenzi yanaumiza, mapenzi yanarun dunia, usiombe yakukute.

gbwa-20190225074318-1-jpg.1099087
 
Extrovert

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Messages
15,428
Points
2,000
Extrovert

Extrovert

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2016
15,428 2,000
Hahah mkuu unahisi kweli sijawahi kupenda???

Tatizo alipenda akaingiza miguu,kichwa na kiwiliwili kwa pamoja...

Tena umemshauri vizuri sana huyu..Nafikiri kama wewe kuwa abadilishe approach mana inaonesha akipenda huwa anajali kupita maelezo...Ajikaze maisha yaendelee.
Ndio inavyokuwa mkuu, katika maisha tunajifunza kutokana na makosa. Mwanzoni kuteleza ni kawaida ila kuanzia paper 2 unakamua kwa uwezo
 
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Messages
35,114
Points
2,000
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2010
35,114 2,000
Kuumia kupo ila ukiwa na expectations, hii hutokea first time mwanaume anapopenda kweli na kutazama future na mwanamke husika. Ukipigwa za uso hapo lazma udate.

Ila kwa wale wa kusogezea siku hata kibuti siwazi kwanza ndio nauza match kila nikipata nafasi. Ntaumiaje wakati sina mpango nawewe. Works like that!
Kama mtu unampenda na unapanga future nae, akizingua shukuru Mungu wala usiumie. Shukuru kwasababu kazingua mapema, angezingua tayari mko ndoani hio ni changamoto maanake kosea hata kujenga ila sio kuoa. Mimi mwanamke nikimpenda akizingua namuacha immediately kwasababu huko mbele nitapata shida, lakini kama simpendi akizingua naenda nae hivyo hivyo namuweka sehemu yake tu.
 
E

Ekuweme

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2018
Messages
1,136
Points
2,000
E

Ekuweme

JF-Expert Member
Joined May 28, 2018
1,136 2,000
Mkuu ushawahi kunyofolewa ukucha wa kidole kikubwa cha mguuni? Unayafahamu maumivu yake? Utagundua hayo maumivu unayo yasema ya mapenzi si kitu.
 
Myahudi Jr II

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
3,688
Points
2,000
Myahudi Jr II

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
3,688 2,000
Kama mtu unampenda na unapanga future nae, akizingua shukuru Mungu wala usiumie. Shukuru kwasababu kazingua mapema, angezingua tayari mko ndoani hio ni changamoto maanake kosea hata kujenga ila sio kuoa. Mimi mwanamke nikimpenda akizingua namuacha immediately lakini kama simpendi akizingua naenda nae hivyo hivyo namuweka sehemu yake tu.
Nijaliwe moyo wako, afu mkuu umesema kweli, sema mwanadamu huwa hatuoni mbele kabisaa tunataka tuliyonayo hapa
 
Myahudi Jr II

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
3,688
Points
2,000
Myahudi Jr II

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
3,688 2,000
Mkuu ushawahi kunyofolewa ukucha wa kidole kikubwa cha mguuni? Unayafahamu maumivu yake? Utagundua hayo maumivu unayo yasema ya mapenzi si kitu.
Maumivu ya nerves ni tofauti kabisa na maumivu ya moyo

Ukininyofoa kucha nakula sana, tena nitataka vitamu zaidi
 
chuma cha reli

chuma cha reli

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2012
Messages
2,278
Points
2,000
chuma cha reli

chuma cha reli

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2012
2,278 2,000
Utakiwi kuwa weak epukana na hiyo hali maana itakucost katika maisha yako yote don't be to emotional

We tell people we love them when we need or want something because real love happens in movies only not in real life
Acha nikiri mimi ni weak, siwezi kupenda kwa kuingia mguu mmoja
 

Forum statistics

Threads 1,294,205
Members 497,843
Posts 31,168,260
Top