Mapenzi yanauma sana ndugu zangu, kamwe usimcheke mtu kama bado hayajakukuta

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
4,798
2,000
Habari za kazi Ndugu zangu natumai mambo yanaenda salama Salimini

Yapita miezi sasa tangu niachane na mwanamke(girlfriend) niliyekua nampenda sana sana, nakiri wazi nilikua nampenda mno, naweza sema ndio alikua mwanamke wangu wa 1(first ever) kuwa nae kwenye mahusiano yaliyo siriazi ambayo ningejua yangezaa ndoa, sijawahi kua na “mahusiano na mwanamke” yeyote hapo kabla ”nieleweke hapa” yaliyo siriazi na kujihusisha na mapenzi kwangu hakikua kitu nilichokipa kipaumbele sana sikutaka kabisa kuchezea moyo wa mwanamke yoyote chini ya jua hili kwakua niliamini “what goes around, comes around” kama sio kwangu basi kwa watoto wangu hata kizazi cha nne, sikutaka hili litokee kabisaa.

Nakiri wazi, binti huyu nilimuhudumia chochote kilicho ndani ya uwezo wangu, daaaaaahhh mapenzi bwana yaache tu, nilifanya hilo kwa moyo wangu wootee, napenda kujali sana, sikutaka ajione yupo mpweke, I tried my best kwakweli, we had fun sehemu mbalimbali(hapa nikipita haya maeneo kumbukumbu zinarudi) mf. Tulikua tunaenda pale “lifepark” Mwenge kutembea na kupata juisi, na ndio njia yangu nayopita sasa,nikifika pale nayakumbuka yale nasema hakika upendo una nguvu.

Nakiri wazi tuu, sijui kama ndio kulia kwenyewe au vipi, machozi yalikua yanabubujika kama chemichemi asee, sijui yanatoka wapi, najitahidi hapa na pale lakini wapi, mapenzi yanauma ndugu zangu, nilikua napumua(exhale) ya moto balaa utadhani ndani nimewashwa jiko la mkaa (jiko la mkaa likiwaka Sanaa huwa linatoa kama miali flani hivi) ndiyo hali nilokua nayo(nashindwa kuielezea vizuri).

Mwanaume sikutamani hata kula, chakula hakipiti, nikiweka kijiko mdomoni naona kama umeniwekea mawe ya kg100, hata harufu ya chakula tu sikuitaka iwe karibu yangu, nilikaa siku 5 bila kutia chochote mdomoni, maana muda wote nilikua nimeshiba tu (hii hali sijui inakuaje wadau, yaani husikii njaa) nilikonda ndani ya wiki tuu, wasiojua walinishangaa sana, niliuchuna kama sijui, nakumbuka nilienda kumuomba ruhusa HR ni mgonjwa aisee aliponiona tu alisema “wewe nenda nitashughulikia kila kituu katibiwe mwanangu nendaaa” kumbe ni mapenzi.
Nisifiche, ilibidi nitundikiwe dripu za Sukari kwa kua sijala kitu chchote kile angalau mwili upate nguvu, japo nilipishana sana na wale watu wa afya, nilisema uongo wangu woote, nikawawin, japo najua walinipiga kwenye kuandikisha pesa ya dkumuona daktari, machupa ya madripu yale, sikujali.

Nilidumbukia mzima mzima, kichwa, kiwiliwili, miguu pamoja na moyo woote, wanawake bwanaa, hivi mpendwaje nyie watuu, unapata mtu aliye siriaz na wewe kwenye kila kitu lakini badooo tuu, yaani nimeshindwa kuwaelewa kabisaa, labda sikua najua ulimwengu wa mapenzi unavoenda.

Kwa umri wangu 27yrs nilikua sijawahi kuingia kwenye mahusiano, nilipoingia sikua na jua kuna kuumizwa, nakumbuka sana nilikua nasoma thread za watu humu nacheka sana, nasema haya mambo yanawezekanaje, nakumbuka kuna MwanaJF alijiua kwa kunywa sumu kule Mbeya mkewe alikua anafanya kazi idara ya maji aisee nilimshangaa sana yule baba nikadiriki kusema “dunia ina wanawake wote hawa anajiua kwa sababu ya mapenzi” Omba yasikukute, yaani mimi kipindi kile hata ungeniletea sijui UWOYA, WEMA, LULU aisee nisingeweza hata kuwataka ningewaona kama wanaume wenzangu, yaani nilikua namtaka yeye tuu, sikuona mwanamke mwingine Zaidi yake. Love is wicked kwakweli hapo ndipo nilipouelewa wimbo huu vizuri sana.

Siku zikapita miezi ikasogea maumivu yapungua nikaweza kula na kuinuka tena, ila alieumwa na nyoka hata jani huliogopa, sina Imani na hawa watu tenaa, moyo umekufa ganzi kwakweli, nguvu ya kuoa imepotea kabisaa, japo nahitaji kuoa kabla sijafika 30yrs, unajua siwezi kuwa “playboy” namaanisha siwezi kuhudumia wanawake wawili, SIWEZI…SIWEZI, bora niwe single tu.

Jana nilikua napitia thread zoote za walioumizwa, nilikua nacheka sana, unaweza ukaona kama yanafurahisha ila mtu unakuwa haupo vizuri mentally ndio maana unakuta mwanaume analalamika sana na anaonekana kama chizi maarifa flani hivi.

Kuna memba humu anaitwa lost id anatoa ushauri sana japo unaweza kumuona kama amechanganyikiwa ila jamaa anaongea facts sana juu ya mahusiano, anasema “mwanamke usimpe moyo wako, mpe pesa ila sio moyo” hapa mimi nilimpa vyote pesa na moyo, ile Burn niliokua naifeel aisee anajua Mungu tu nadhani.

Nawashukuru Wachangiaji woote wa thread mbalimbali za watu walioumizwa, japo zinasaidia 10% tu, zilizobaki ni MUDA tu ndio utakaoponya maumivu hayo.

Mapenzi yanauma, mapenzi yanaumiza, mapenzi yanarun dunia, usiombe yakukute.

GBWA-20190225074318[1].jpg
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
22,638
2,000
Hakika, ukishakinywea hiki kikombe lazima ubadilike
Huo nauita ubatizo wa moto, sasa sahivi umezaliwa upya katika maswala ya kimahusiano. Ukilizwa tena ujue umejitakia ila hivyo ndio gemu inavyokwenda. Kingine soma tabia za wanawake cheki makala mtandaoni. Zilinisaidia sana ikiwamo kufahamu kuwa the more you lurk around a woman the more he find you clingy.

Ukimuonesha kumjali sana KE anakuona uko weak sana it turns her off you should not be overnice.
The more you hurt yourfself pleasing her the more she feels insecure about you. Unatakiwa umjali kwa kiasi tu usijiumize kuonekana hero mbele yake maana mwisho atakuona kituko. Ndio walivyo hao.

Mwisho ujifunze kukaza, dont be a doormat sio kila unachoombwa unatoa tu. Vingine kataa, set standards zako mzee. Try to loose her at times analeta kwere, atajitudisha mwenyewe on track sio unafanyiwa vituko unang'ang'ania tu kama mamaako mzazi huyo. Let her loose akisepa ujue hakuwa wako
 

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
4,798
2,000
Kupenda hadi kushindwa kula,kutundikiwa drip dah mie naona ulijiendekeza sana...

Wewe sio wa kwanza Kupenda wala hautakuwa wa mwisho hebu jikaze na upunguze kulialia.
Sijalia tenaa na sitegemei sanaaa, ila ujue kuna wanaume wanapenda balaa sema ndio hivyo chanhamoto hazikosi
 

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
4,798
2,000
Jibu zuri sanaa hili Mkuu, tatizo kuna watu wanajifanya wana roho za Kimungu kwamba wanajiaminia sanaa kana kwamba wanahisi ni Udhaifu Kumpenda mwanamke unayetarajia awe mke wako mama yako wa uzeeni mwako
Na mimi ndivyo nilivyo, nikipenda nazama mzimaaa mzimaa, nashindwa kujizuia kabisaaaa, inanibidi niwe na mmoja ambae nauhakika nae
 
Top Bottom