Mapenzi yanauma sana ndugu zangu, kamwe usimcheke mtu kama bado hayajakukuta

Habari za kazi Ndugu zangu natumai mambo yanaenda salama Salimini

Yapita miezi sasa tangu niachane na mwanamke(girlfriend) niliyekua nampenda sana sana, nakiri wazi nilikua nampenda mno, naweza sema ndio alikua mwanamke wangu wa 1(first ever) kuwa nae kwenye mahusiano yaliyo siriazi ambayo ningejua yangezaa ndoa, sijawahi kua na “mahusiano na mwanamke” yeyote hapo kabla ”nieleweke hapa” yaliyo siriazi na kujihusisha na mapenzi kwangu hakikua kitu nilichokipa kipaumbele sana sikutaka kabisa kuchezea moyo wa mwanamke yoyote chini ya jua hili kwakua niliamini “what goes around, comes around” kama sio kwangu basi kwa watoto wangu hata kizazi cha nne, sikutaka hili litokee kabisaa.

Nakiri wazi, binti huyu nilimuhudumia chochote kilicho ndani ya uwezo wangu, daaaaaahhh mapenzi bwana yaache tu, nilifanya hilo kwa moyo wangu wootee, napenda kujali sana, sikutaka ajione yupo mpweke, I tried my best kwakweli, we had fun sehemu mbalimbali(hapa nikipita haya maeneo kumbukumbu zinarudi) mf. Tulikua tunaenda pale “lifepark” Mwenge kutembea na kupata juisi, na ndio njia yangu nayopita sasa,nikifika pale nayakumbuka yale nasema hakika upendo una nguvu.

Nakiri wazi tuu, sijui kama ndio kulia kwenyewe au vipi, machozi yalikua yanabubujika kama chemichemi asee, sijui yanatoka wapi, najitahidi hapa na pale lakini wapi, mapenzi yanauma ndugu zangu, nilikua napumua(exhale) ya moto balaa utadhani ndani nimewashwa jiko la mkaa (jiko la mkaa likiwaka Sanaa huwa linatoa kama miali flani hivi) ndiyo hali nilokua nayo(nashindwa kuielezea vizuri).

Mwanaume sikutamani hata kula, chakula hakipiti, nikiweka kijiko mdomoni naona kama umeniwekea mawe ya kg100, hata harufu ya chakula tu sikuitaka iwe karibu yangu, nilikaa siku 5 bila kutia chochote mdomoni, maana muda wote nilikua nimeshiba tu (hii hali sijui inakuaje wadau, yaani husikii njaa) nilikonda ndani ya wiki tuu, wasiojua walinishangaa sana, niliuchuna kama sijui, nakumbuka nilienda kumuomba ruhusa HR ni mgonjwa aisee aliponiona tu alisema “wewe nenda nitashughulikia kila kituu katibiwe mwanangu nendaaa” kumbe ni mapenzi.
Nisifiche, ilibidi nitundikiwe dripu za Sukari kwa kua sijala kitu chchote kile angalau mwili upate nguvu, japo nilipishana sana na wale watu wa afya, nilisema uongo wangu woote, nikawawin, japo najua walinipiga kwenye kuandikisha pesa ya dkumuona daktari, machupa ya madripu yale, sikujali.

Nilidumbukia mzima mzima, kichwa, kiwiliwili, miguu pamoja na moyo woote, wanawake bwanaa, hivi mpendwaje nyie watuu, unapata mtu aliye siriaz na wewe kwenye kila kitu lakini badooo tuu, yaani nimeshindwa kuwaelewa kabisaa, labda sikua najua ulimwengu wa mapenzi unavoenda.

Kwa umri wangu 27yrs nilikua sijawahi kuingia kwenye mahusiano, nilipoingia sikua na jua kuna kuumizwa, nakumbuka sana nilikua nasoma thread za watu humu nacheka sana, nasema haya mambo yanawezekanaje, nakumbuka kuna MwanaJF alijiua kwa kunywa sumu kule Mbeya mkewe alikua anafanya kazi idara ya maji aisee nilimshangaa sana yule baba nikadiriki kusema “dunia ina wanawake wote hawa anajiua kwa sababu ya mapenzi” Omba yasikukute, yaani mimi kipindi kile hata ungeniletea sijui UWOYA, WEMA, LULU aisee nisingeweza hata kuwataka ningewaona kama wanaume wenzangu, yaani nilikua namtaka yeye tuu, sikuona mwanamke mwingine Zaidi yake. Love is wicked kwakweli hapo ndipo nilipouelewa wimbo huu vizuri sana.

Siku zikapita miezi ikasogea maumivu yapungua nikaweza kula na kuinuka tena, ila alieumwa na nyoka hata jani huliogopa, sina Imani na hawa watu tenaa, moyo umekufa ganzi kwakweli, nguvu ya kuoa imepotea kabisaa, japo nahitaji kuoa kabla sijafika 30yrs, unajua siwezi kuwa “playboy” namaanisha siwezi kuhudumia wanawake wawili, SIWEZI…SIWEZI, bora niwe single tu.

Jana nilikua napitia thread zoote za walioumizwa, nilikua nacheka sana, unaweza ukaona kama yanafurahisha ila mtu unakuwa haupo vizuri mentally ndio maana unakuta mwanaume analalamika sana na anaonekana kama chizi maarifa flani hivi.

Kuna memba humu anaitwa lost id anatoa ushauri sana japo unaweza kumuona kama amechanganyikiwa ila jamaa anaongea facts sana juu ya mahusiano, anasema “mwanamke usimpe moyo wako, mpe pesa ila sio moyo” hapa mimi nilimpa vyote pesa na moyo, ile Burn niliokua naifeel aisee anajua Mungu tu nadhani.

Nawashukuru Wachangiaji woote wa thread mbalimbali za watu walioumizwa, japo zinasaidia 10% tu, zilizobaki ni MUDA tu ndio utakaoponya maumivu hayo.

Mapenzi yanauma, mapenzi yanaumiza, mapenzi yanarun dunia, usiombe yakukute.

View attachment 1099087
Cheka sn na dem wko,furahi nae san,pga nae stor zote lkn tengeneza mazingira ya wew kutoumia kwa hali yeyote koz ucwe mtumwa wa mtu no matter upendo uko vp.
 
Huo nauita ubatizo wa moto, sasa sahivi umezaliwa upya katika maswala ya kimahusiano. Ukilizwa tena ujue umejitakia ila hivyo ndio gemu inavyokwenda. Kingine soma tabia za wanawake cheki makala mtandaoni. Zilinisaidia sana ikiwamo kufahamu kuwa the more you lurk around a woman the more he find you clingy.

Ukimuonesha kumjali sana KE anakuona uko weak sana it turns her off you should not be overnice.
The more you hurt yourfself pleasing her the more she feels insecure about you. Unatakiwa umjali kwa kiasi tu usijiumize kuonekana hero mbele yake maana mwisho atakuona kituko. Ndio walivyo hao.

Mwisho ujifunze kukaza, dont be a doormat sio kila unachoombwa unatoa tu. Vingine kataa, set standards zako mzee. Try to loose her at times analeta kwere, atajitudisha mwenyewe on track sio unafanyiwa vituko unang'ang'ania tu kama mamaako mzazi huyo. Let her loose akisepa ujue hakuwa wako
Mkuu hii ni kweli kabisa!binafsi nilikuwa namfanyia kila kitu hata nisivyopenda mimi ili tu kumfanya afurahi !yani niliogopa kumpoteza kwa kuogopa ntakosa mzuri kama yeye!alinitesa sana aisee yule binti!ila kuonyesha kutokujali na aone unaweza kumuacha mda wowote ndo dawa yao hawa viumbe anakuwa na heshima na anatulia
 
acha blaablaaa sema nini kilitokea.mthredi mreeefu huelezei kisa ndo nn sasa? uligongewa? au?ningekuwa moderator ningekunyuka ban akil ikukae sawa na ukajifunze jinsi y kusimulia mikasa
 
Sijawah penda from that time mpaka leo

Am just happy with my life

Playing games

Looking movies

Playing with my son theodore

Eating delicious food , tena hapa mi ni fundi teh !

Reading my books

Finaly doing many surgery as much as i can , and writing my scientific researches as many as i can

My life have been better without them am feeling blessed

And i doncha gona hate them !!

With time utaanza tena kuhisi upweke hautakaa
ivyo milele ni swala la muda tu
 
Mkuu hii ni kweli kabisa!binafsi nilikuwa namfanyia kila kitu hata nisivyopenda mimi ili tu kumfanya afurahi !yani niliogopa kumpoteza kwa kuogopa ntakosa mzuri kama yeye!alinitesa sana aisee yule binti!ila kuonyesha kutokujali na aone unaweza kumuacha mda wowote ndo dawa yao hawa viumbe anakuwa na heshima na anatulia
Amini kwamba ukifata hayo niliyosema hapo juu katika hio post hamna mwanamke atakujia juu ama kukusumbua hata akiwa mzuri kama Anjelina Jolie.

Wanawake kudeal nao ni trick ya kucheza na hormones zao tu 🤣🤣🤣. Hakika utawafaidi mkuu na utainjoy kuwa nao. They mostly need a man not a boy attitude. Just put her into place hata kama itarisk we kumpoteza na amini kwamba hataenda popote atazidi kukupenda tu.
 
With time utaanza tena kuhisi upweke hautakaa
ivyo milele ni swala la muda tu
Ni miaka sasa mingi sana

Wengi wamenipenda may be due to my position

Labda pia sababu ya upole wangu

Yaani wengine wametamka wazi wazi how they deeply love me

Aisee .... Mi siwaamini i just trust my son
 
Huo nauita ubatizo wa moto, sasa sahivi umezaliwa upya katika maswala ya kimahusiano. Ukilizwa tena ujue umejitakia ila hivyo ndio gemu inavyokwenda. Kingine soma tabia za wanawake cheki makala mtandaoni. Zilinisaidia sana ikiwamo kufahamu kuwa the more you lurk around a woman the more he find you clingy.

Ukimuonesha kumjali sana KE anakuona uko weak sana it turns her off you should not be overnice.
The more you hurt yourfself pleasing her the more she feels insecure about you. Unatakiwa umjali kwa kiasi tu usijiumize kuonekana hero mbele yake maana mwisho atakuona kituko. Ndio walivyo hao.

Mwisho ujifunze kukaza, dont be a doormat sio kila unachoombwa unatoa tu. Vingine kataa, set standards zako mzee. Try to loose her at times analeta kwere, atajitudisha mwenyewe on track sio unafanyiwa vituko unang'ang'ania tu kama mamaako mzazi huyo. Let her loose akisepa ujue hakuwa wako
Nimependa ushaur wako big up
 
Nimeamini ww ni mtoto na huyo mwanamama alikutenda kwa sababu ya utoto wako.

Ebu fikiria unajitokeza JF unazungumzia tu kuachana na mpenz waki bila kuelezea ilivyokua, mazingira gan na kwa nn ilitokea ivo.

Unatuletea tu habari juu juu. Vip na wengne wangekua wanatoa habari nusu nusu....JF ingekua kama ilivo? Ww ni mtoto wa Facebook.
 
Back
Top Bottom