Mapenzi yanauma sana ndugu zangu, kamwe usimcheke mtu kama bado hayajakukuta

Daaahh, bora ujitenge mapema usikutwe na bwana pepsi huyu, hakulipii afu anakuacha peke yako

Ila mkuu nitaumia kiasi maana huyi mamsi tumetoka mbali since naanza maisha ya kigeto geto , nalala chini, Sina mishe ya kueleweka , Tunagombana tunapatana , ila now mambo yamekuwa serious, nina 3 day ban, simu nlomnunulia na kaipasua mbele yangu na line kavunja dah so nimemute tuuu
 
Pole Sana...mapenzi yalishatiwa dosari toka enzi za bustani ya Edeni...sisi tunarudia tu.
 
uzoefu kazini nacho ni kitu cha msingi, ushakuwa mzoefu sasa kazi utaifanya vzuri. haya nikutakie kazi njema uendako huko
 
Huo nauita ubatizo wa moto, sasa sahivi umezaliwa upya katika maswala ya kimahusiano. Ukilizwa tena ujue umejitakia ila hivyo ndio gemu inavyokwenda. Kingine soma tabia za wanawake cheki makala mtandaoni. Zilinisaidia sana ikiwamo kufahamu kuwa the more you lurk around a woman the more he find you clingy.

Ukimuonesha kumjali sana KE anakuona uko weak sana it turns her off you should not be overnice.
The more you hurt yourfself pleasing her the more she feels insecure about you. Unatakiwa umjali kwa kiasi tu usijiumize kuonekana hero mbele yake maana mwisho atakuona kituko. Ndio walivyo hao.

Mwisho ujifunze kukaza, dont be a doormat sio kila unachoombwa unatoa tu. Vingine kataa, set standards zako mzee. Try to loose her at times analeta kwere, atajitudisha mwenyewe on track sio unafanyiwa vituko unang'ang'ania tu kama mamaako mzazi huyo. Let her loose akisepa ujue hakuwa wako
Experience is the best teacher hahaaaaa
 
Usikubali kuzama mzima mzima mkuu utakufa, wengi huwatokea katika first love lakin umejifunza sana ukiona hali kama hyo inaendelea kwa watakao kuja baada ya huyo utapata tabu sana maana utakua unajitakia mwenyewe...........kuumizwa kwenye mapenz huwa ni mara 1 tu, zaid ya mara 1 huko n kujitakia.
 
 
Mkuu tatizo ulikuw lena kwenye mapenz ndo ulikuw unaanza afu age 27yrs, hujawai pata kashikash za mapenz thats all. Ushaur wangu me tafuta wengine kama wa5 then date nao afu angalia anaejielewa, shida mnataka madem wa chuo hapa ndo shida
 
Habari za kazi Ndugu zangu natumai mambo yanaenda salama Salimini

Yapita miezi sasa tangu niachane na mwanamke(girlfriend) niliyekua nampenda sana sana, nakiri wazi nilikua nampenda mno, naweza sema ndio alikua mwanamke wangu wa 1(first ever) kuwa nae kwenye mahusiano yaliyo siriazi ambayo ningejua yangezaa ndoa, sijawahi kua na “mahusiano na mwanamke” yeyote hapo kabla ”nieleweke hapa” yaliyo siriazi na kujihusisha na mapenzi kwangu hakikua kitu nilichokipa kipaumbele sana sikutaka kabisa kuchezea moyo wa mwanamke yoyote chini ya jua hili kwakua niliamini “what goes around, comes around” kama sio kwangu basi kwa watoto wangu hata kizazi cha nne, sikutaka hili litokee kabisaa.

Nakiri wazi, binti huyu nilimuhudumia chochote kilicho ndani ya uwezo wangu, daaaaaahhh mapenzi bwana yaache tu, nilifanya hilo kwa moyo wangu wootee, napenda kujali sana, sikutaka ajione yupo mpweke, I tried my best kwakweli, we had fun sehemu mbalimbali(hapa nikipita haya maeneo kumbukumbu zinarudi) mf. Tulikua tunaenda pale “lifepark” Mwenge kutembea na kupata juisi, na ndio njia yangu nayopita sasa,nikifika pale nayakumbuka yale nasema hakika upendo una nguvu.

Nakiri wazi tuu, sijui kama ndio kulia kwenyewe au vipi, machozi yalikua yanabubujika kama chemichemi asee, sijui yanatoka wapi, najitahidi hapa na pale lakini wapi, mapenzi yanauma ndugu zangu, nilikua napumua(exhale) ya moto balaa utadhani ndani nimewashwa jiko la mkaa (jiko la mkaa likiwaka Sanaa huwa linatoa kama miali flani hivi) ndiyo hali nilokua nayo(nashindwa kuielezea vizuri).

Mwanaume sikutamani hata kula, chakula hakipiti, nikiweka kijiko mdomoni naona kama umeniwekea mawe ya kg100, hata harufu ya chakula tu sikuitaka iwe karibu yangu, nilikaa siku 5 bila kutia chochote mdomoni, maana muda wote nilikua nimeshiba tu (hii hali sijui inakuaje wadau, yaani husikii njaa) nilikonda ndani ya wiki tuu, wasiojua walinishangaa sana, niliuchuna kama sijui, nakumbuka nilienda kumuomba ruhusa HR ni mgonjwa aisee aliponiona tu alisema “wewe nenda nitashughulikia kila kituu katibiwe mwanangu nendaaa” kumbe ni mapenzi.
Nisifiche, ilibidi nitundikiwe dripu za Sukari kwa kua sijala kitu chchote kile angalau mwili upate nguvu, japo nilipishana sana na wale watu wa afya, nilisema uongo wangu woote, nikawawin, japo najua walinipiga kwenye kuandikisha pesa ya dkumuona daktari, machupa ya madripu yale, sikujali.

Nilidumbukia mzima mzima, kichwa, kiwiliwili, miguu pamoja na moyo woote, wanawake bwanaa, hivi mpendwaje nyie watuu, unapata mtu aliye siriaz na wewe kwenye kila kitu lakini badooo tuu, yaani nimeshindwa kuwaelewa kabisaa, labda sikua najua ulimwengu wa mapenzi unavoenda.

Kwa umri wangu 27yrs nilikua sijawahi kuingia kwenye mahusiano, nilipoingia sikua na jua kuna kuumizwa, nakumbuka sana nilikua nasoma thread za watu humu nacheka sana, nasema haya mambo yanawezekanaje, nakumbuka kuna MwanaJF alijiua kwa kunywa sumu kule Mbeya mkewe alikua anafanya kazi idara ya maji aisee nilimshangaa sana yule baba nikadiriki kusema “dunia ina wanawake wote hawa anajiua kwa sababu ya mapenzi” Omba yasikukute, yaani mimi kipindi kile hata ungeniletea sijui UWOYA, WEMA, LULU aisee nisingeweza hata kuwataka ningewaona kama wanaume wenzangu, yaani nilikua namtaka yeye tuu, sikuona mwanamke mwingine Zaidi yake. Love is wicked kwakweli hapo ndipo nilipouelewa wimbo huu vizuri sana.

Siku zikapita miezi ikasogea maumivu yapungua nikaweza kula na kuinuka tena, ila alieumwa na nyoka hata jani huliogopa, sina Imani na hawa watu tenaa, moyo umekufa ganzi kwakweli, nguvu ya kuoa imepotea kabisaa, japo nahitaji kuoa kabla sijafika 30yrs, unajua siwezi kuwa “playboy” namaanisha siwezi kuhudumia wanawake wawili, SIWEZI…SIWEZI, bora niwe single tu.

Jana nilikua napitia thread zoote za walioumizwa, nilikua nacheka sana, unaweza ukaona kama yanafurahisha ila mtu unakuwa haupo vizuri mentally ndio maana unakuta mwanaume analalamika sana na anaonekana kama chizi maarifa flani hivi.

Kuna memba humu anaitwa lost id anatoa ushauri sana japo unaweza kumuona kama amechanganyikiwa ila jamaa anaongea facts sana juu ya mahusiano, anasema “mwanamke usimpe moyo wako, mpe pesa ila sio moyo” hapa mimi nilimpa vyote pesa na moyo, ile Burn niliokua naifeel aisee anajua Mungu tu nadhani.

Nawashukuru Wachangiaji woote wa thread mbalimbali za watu walioumizwa, japo zinasaidia 10% tu, zilizobaki ni MUDA tu ndio utakaoponya maumivu hayo.

Mapenzi yanauma, mapenzi yanaumiza, mapenzi yanarun dunia, usiombe yakukute.

View attachment 1099087
Bora kuachana nayo!
 
Kama mtu unampenda na unapanga future nae, akizingua shukuru Mungu wala usiumie. Shukuru kwasababu kazingua mapema, angezingua tayari mko ndoani hio ni changamoto maanake kosea hata kujenga ila sio kuoa. Mimi mwanamke nikimpenda akizingua namuacha immediately kwasababu huko mbele nitapata shida, lakini kama simpendi akizingua naenda nae hivyo hivyo namuweka sehemu yake tu.
Nimekuelewa sana Kaka Mkubwa ,Maana kwa wanao amini katika Mungu tunaami hapo Mungu anakuwa amekuepusha na majanga makubwa mbeleni
 
Back
Top Bottom