Mapenzi Yanataabu

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,236
Points
0

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,236 0
Nimekupata mpenzi , Mpenzi wangu wa ndani
Mi mwenzio sijiwezi Sina raha duniani
Nataka yako mapenzi Uliyonipa zamani

Mapenzi ni kikohozi Kuyaficha huwa kazi
Nina kiu ya mapenzi Tokea enzi na enzi
Nimekupata mpenzi Nakuomba unienzi

Ulinionjesha raha Raha zako za ajabu
Imekua ni karaha Moyoni napata tabu
Mapenzi sio karaha Nitoe hii aibu

Ni macho yaonapo Moyo huwa mashakani
Yasingelionapo Moyo usingetamani
Moyoni bado upo Japo kua huamini
 

Palloma

Member
Joined
Apr 8, 2008
Messages
8
Points
0

Palloma

Member
Joined Apr 8, 2008
8 0

Mpenzi njoo kwa haraka,
Sijamaliza mapenzi bado nakutaka!

Mbona ulipoondoka hukuniaga mpenzi,
Mwenzako nakukukumbuka yananitoka machozi,
Rudi wangu muhibaka unifutie simanzi!

Tangu ulipoondoka moyoni sina tabasamu,
Kuwaza na kukumbuka mapenzi yako matamu,
Na iwapo hutafika ninahiari kunywa sumu!

Toka ulipoondoka sina furaha moyoni,
Kuwaza na kukumbuka la kutenda silioni,
Rudi wangu nyonda nami niwe furahani!
Njoo kwa haraka!!!

 

Mbu

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2007
Messages
12,746
Points
1,500

Mbu

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2007
12,746 1,500
"hakuna mwingine kuliko wewe,
nakonda kwa maradhi ya mapenzi nilokuwa nayo!"
 

Mwazange

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2007
Messages
1,054
Points
1,195

Mwazange

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2007
1,054 1,195
Sabalkheri mpenzi waonaje hali yako....
Sabal'Ain habibi, hali yangu kama yako.....
Wawaonaje wazazi nyumbani utokeako.....


Haya na mtu apokee hapo jamani....
 

Forum statistics

Threads 1,366,252
Members 521,422
Posts 33,365,410
Top