Mapenzi yanaota kwa kasi kwa huyu mlimbwende wa JF.

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,373
54,755
Mnakumbuka tumeacha utoto wa Dura na Subila?

Yapata miaka 6 naishi humu ndani kwa michango ya tofautitofauti na nilikaa pasi ya kuwa na ukaribu na mwanachama yoyote humu kwa muda wa miaka 4 ila mwaka wa 5 nilipata kuanza PM na mlimbwende mmoja humu hakika sikudhani kama naweza kutana na binti wa aina hii ambayo kwa sasa ninayo.

Tulianza kuchat PM na baadae mawasiliano ya kawaida, akazidi kuuteka moyo wangu kwa namna alivyo tayari muda wowote kuwa nami. Siandiki kwa sababu ya kutaka attention ila najaribu kumsifia mlimbwende huyu ambaye siku si nyingi akikubali kuachana na mtu wake basi tunaweza kuoana.

August mwaka huu aliwahi kuja eneo ninalokaa wakati akitoka Mbeya kwenye mambo yake ya kazi. Hakika ilikuwa ni siku ya kukumbukwa kwetu sote wawili.

Na siku tuliyoonana mara ya kwanza nilijikuta nakunywa pombe kwa sababu yake.

"Bby unajua sipendi pombe ila kwa vile umeamua nitakunywa sina pingamizi"

Pembe za Panzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom