Mapenzi yanagharimu kama si kuchukua kabisa maisha ya watu

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,791
8,743
Habari za wakati huu mabibi na mabwana, heshima kwenu.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, leo katika kutafakàri mambo mengi nimekumbukà mkasa uliompata kaka yangu hata kuepelekeà kifo chake yapata miezi 8 sasa. Kaka yangu alitokea kumpenda huyu dada, na dada nae alimpenda kaka, niliwashuhudia wakifurahia mapendo yao, kweli Eliza alimpenda kaka, kaka nae alimpenda Eliza, ndugu, jamaa na marafiki walijua kuwa hawa ni wapendanao. Huko na kule kaka akatujuza wanafamilia kuwa ataka afunge ndoa na Eliza, kama familia hatukuwa na shaka bali tulifurahia kwani ndiye aliyekuwa kaka yetu mkubwa, familia tulimtakia kheri.

Harakati za kupeleka posa zikaanza, na hapo ndipo matatizo yalipoanza, wazazi wa Eliza hawakutaka mtoto wao aolewe na kaka kwa kisingio cha uchumi mdogo, na kumtaka binti yao atafute rubani wa ndege, kaka yangu alikuwa mhasibu kampuni moja maarufu jijini Arusha, kabla ya hapo alikuwa akifanya kazi Nakuru, Kenya, kama mhasibu, alikuwa na maisha ya kawaida tu.

Posa ilikataliwa lakini wao kama wapendanao walikubaliana waishi, waliishi kwa muda baadae Eliza nadhani alishindwa kutokana na kutoelewana na wazazi wake, siku moja kaka yangu akiwa safarini Kenya kwenda kuchukua mizigo yake siku anarudi alimkuta Eliza yuko na njemba katika kitanda chake, hakika kaka alihuzunika sana.

Baada ya tukio lile la kuktwa na njemba ndani nyumba, Eliza aliondoka kwa aibu kusikojulikana, baadae tulisikia yupo Dar es Salaam anaishi na yule yule njemba aliyekutwa nae. Kaka yangu hakuwa mnywaji wa pombe alianza kunywa pombe, hata kuchanganyikiwa na kufikia kufungukiwa ndani, hapo ndo ikawa mwanzo wa maisha ya kaka kuharibika.

Aliishi hivyo na ile hali, japo familia na wapendwa kanisani walijaribu kumsaidia lakini haikuwezekana alikuwa akiacha baadae kurudia tena, na tangu aachane na Eliza hakutaka mwanamke mwingine. Binafsi nilikuwa nikiumia nakumuhurumia kwani malengo yake yote yalipotea na alikuwa mtu mwenye kukata tamaa, kazi aliacha akawa yupo yupo tu, alikuwa ni mwenye msongo wa mawazo,

Siku moja alinipigia simu usiku tuliongea sana kama SAA moja na zaidi hivi, katika kuongea huko nilimsihi mambo mengi mwisho akanambia sister nimekuelewa nitafanya ulivyosema, nilifurahi sana, kesho yake majira ya mchana nilimpigia kumjulia hali akanambia sister kuhusu Eliza tena sahau naanza maisha mapya, nilimpongeza, siku inayofuata nilipata simu toka kwa rafiki yake kuwa amefariki usiku akiwa amelala, tulimzika jamaa na marafiki waliungana nasi kutufariji, pia familia ya Eliza walihudhuria maziko. Na huo ndo ukawa mwisho wake.

Naweza kusema mapenzi yamegharimu maisha ya kaka
 
Inaonekana kuwa huyo Eliza ndo hakuwa na mapenz ya kweli kwa kaka yako, aka alimpenda kwa 54%... yani ni rahisi zaidi kuwa billionea kuliko kumpata anaekupenda 100% na ww umpende 100%. Mm mapenz huwa siyaendekezi..
 
Sasa hamkuchunguza hata nini kimemuuwa kweli???, inawezekana alikuwa keshasamehe kweli kama alivyokwambia ila akafa kwa pressure.
 
Dahhh.......
Umenikumbusha mbali sana aiseee...
Hiyo siku natoka likizo kurudi kazi na tulikua tuliishi camp. Ndipo nikatakiwa wazi na mdada nilie mpenda kwamba hanitaki tena na yupo na tu mwingine.
Lohh.... Kumbe Rafiki wangu w karibu ndie alie anzisha mahusiano na mpenzi wangu aiseeee.....
To make it long shot, niligeuka na nikakuamlevi wa kutupwa na hata kazi nikawa siendi.
Mwisho nilifukuzwa kazi, ingawa meneja w kitengo changu alijua sababu na akaniambia niende kisha nikiwa sawa nisemeshe kwa sim then anifanyie mpango wa ajira tena.
Agghhhh.....
Haya mambo magumu sana aiseee
 
Wazazi Wa Eliza walitaka aolewe na Rubani!
Hii kali hawa ma rubani wa tanzania?maana wanajua marubani ndio wenye pesa nyingi,?
Ahahaaa
 
Life without wife is not life but a wife can act as a knife to cut off your life
 
Hayo ndo madhara ya wanaume bikra kamuona eliza ndo mwanamke pekeee anampenda kuliko hata mama yake kweli huu ni ujinga kwa ambao mnatarajia kupenda kiivyo loh!
 
Back
Top Bottom