Mapenzi ya kizazi hiki na heshima mbele ya wazazi yamenichosha. Oooops!!

Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
4,368
2,608
Nina bint yangu yuko form two. Nilikuwa najaribu kufuatia mwenendo wake nikagundua vijana wameshaanza kumchakachua,nilipofuatilia kwa karibu zaidi nikagundua ana kaboyfriend shulen na kijana mmoja mitaa ninayoishi naye ni mwanafunzi ila anasoma shule nyingine. Nilimweleza mama yake akae naye ampe darasa, hvyo mama yake alichua jukumu hilo ambapo jana alikaa naye na kumweleza impact ya kujihusisha na mambo ya mapenzi wakati anasoma, na moja ya mambo aliyomweleza kuwa wanaume ni wabaya sana, si watu wazuri na watamwaribia maisha yake. Lakini binti naye akamwuliza mama yake kama anasema wanaume ni wabaya mbona weweunaishi na baba,kwani yeye sio mwanaume na si mbaya? Huogopi atakuharibia maisha yako?,wife akashindwa kuendelea kukapa councelling akaja kunieleza. Nimechoka nashindwa hata nimfanye nini huyu mtoto manake hasikii na siku zinavyokwenda nako kanazid kuchanganyikiwa na malavidavi. Jaman hebu nisaidien dawa/njia ya kumpunguza spindi huyu mtoto. Au nikapeleke kwa bibi akakakekete kukapunguza speed?.

Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
4,368
2,608
ukikakeketa ndo unaongeza speed,angalia warangi na wanyaturu......

mbona nasikia kukeketa kunapunguza? Warangi na wanyaturu si sababu ya maisha magumu ya kule wanakotoka?

Chauro

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
2,968
1,471
Pamoja na nguvu zetu katika malezi naamini sala ina nguvu kubwa sana ya kurekibisha mambo..................

Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,182
408
Nina bint yangu yuko form two. Nilikuwa najaribu kufuatia mwenendo wake nikagundua vijana wameshaanza kumchakachua,nilipofuatilia kwa karibu zaidi nikagundua ana kaboyfriend shulen na kijana mmoja mitaa ninayoishi naye ni mwanafunzi ila anasoma shule nyingine. Nilimweleza mama yake akae naye ampe darasa, hvyo mama yake alichua jukumu hilo ambapo jana alikaa naye na kumweleza impact ya kujihusisha na mambo ya mapenzi wakati anasoma, na moja ya mambo aliyomweleza kuwa wanaume ni wabaya sana, si watu wazuri na watamwaribia maisha yake. Lakini binti naye akamwuliza mama yake kama anasema wanaume ni wabaya mbona unaishi na baba? Huogopi atakuharibia maisha yak?. Nimechoka nashindwa hata nimfanye nini huyu mtoto manake hasikii na siku zinavyokwenda nako kanazid kuchanganyikiwa na malavidavi. Jaman hebu nisaidien dawa/njia ya kumpunguza spindi huyu mtoto. Au nikapeleke kwa bibi akakakekete kukapunguza speed?.

Duuh mkuu huyo mtoto ni wako wakumzaa au ni nduguyo wakufikia?? Maana ulivoandika inaonesha hauko siriaz na maamuzi yako mbele ya familia yako,

okey jambo lamuhmu inabidi ufanye maamuzi kama mzazi, sidhani kama utashindwa endapo utaamua kufanya hvo, jaribu kufatilia maendeleo yake shuleni, akirudi nyumbani atumie muda mwingi kufanya kazi za shule(home work) na apunguze au umkataze kabisa safari zisizo na umuhimu kwake(kuzurura)..

Lakini pia kama baba unaweza kukaa nae na kumueleza madhara yakujihusisha na mapenz wakati bado student, ongea naye juu ya mimba na magonjwa ya ngono pia..

BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
572
ndugu, kwanza huyo mtoto ni wako au wenu??? je mabadiliko umeanza kuytaona muda gani?/ je huamini na wewe una nafasi ya kuongea na huyu mtoto???

ni wangu. kichwan yupo fresh.si kuwa sichukui jukumu kama mzazi i tried at my best level kumweka sawa, ila si unajua watoto hawa wa sasa wa facebook wanasumbua sana

NYENJENKURU

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
1,036
247
ndugu, kwanza huyo mtoto ni wako au wenu??? je mabadiliko umeanza kuytaona muda gani?/ je huamini na wewe una nafasi ya kuongea na huyu mtoto???
Ni kweli na wewe unanafasi kwa hilo siyo mama pekee yake

Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
4,368
2,608
ndugu, kwanza huyo mtoto ni wako au wenu??? je mabadiliko umeanza kuytaona muda gani?/ je huamini na wewe una nafasi ya kuongea na huyu mtoto???

mabadiliko nilianza kuyaona taratibu na ndio maana nikaanza ku trace wapi tatizo, ndio nikagundua hayo mambo yanayomfanya awe hivyo, muda wa kukaa nae upo na ninajitahidi sana kumwelimisha. Tatizo ni kuwa unamweleza ila alkikupa mgongo ndo imetoka hvyo,yote unayomweleza anayaacha hapohapo.

Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
4,368
2,608
Makuzi bila kumtanguliza Mungu ni kumuharibu mtoto

bujibuji hebu toa ushauri kaka nifanyeje. Hv unafikiri watu wote wanaoharibikiwa watoto wanakuwa hawamshirikishi Mungu katika malezi?

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,735
9,119
Jaribu kutafuta mtu mwingine wa kumshauri. Watoto wa hivyo wengi huwa hawapendi kusikia wanachoambiwa na wazazi.

BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
572

mabadiliko nilianza kuyaona taratibu na ndio maana nikaanza ku trace wapi tatizo, ndio nikagundua hayo mambo yanayomfanya awe hivyo, muda wa kukaa nae upo na ninajitahidi sana kumwelimisha. Tatizo ni kuwa unamweleza ila alkikupa mgongo ndo imetoka hvyo,yote unayomweleza anayaacha hapohapo.

je huwa unaongea na mtoto wako arudipo toka shule au huna hiiyo tabia??? pia inaonyesha una weekness fulani ambayo huyo mwanao anaitumia na wewe unashindwa kuchukua hatua

Vin Diesel

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
9,083
6,334
Kwa jinsi ulivyoleta hii thread naona mtoto hana makosa kabisa kwani amerithi tabia yako ya kuchukulia mzaha kila jambo.

IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,375
6,995
Kwa jinsi ulivyoleta hii thread naona mtoto hana makosa kabisa kwani amerithi tabia yako ya kuchukulia mzaha kila jambo.

mimi hiyo avatar yake sijui imekaaje,..nilifikiri ni 'she'....kumbe ni mwenzetu bana,.......ushauri wangu ubadili avatar utaona mabadiliko ya mtoto wako

lolyz

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
339
197
. Lakini binti naye akamwuliza mama yake kama anasema wanaume ni wabaya mbona weweunaishi na baba,kwani yeye sio mwanaume na si mbaya? Huogopi atakuharibia maisha yako?,wife akashindwa kuendelea kukapa councelling akaja kunieleza.

Kwanza poleni sana kwa huo mtihani wa malezi,
Kwani nyie kama wazazi wa binti mnaishi kwa wazazi wenu? mama anapaswa amweleze huyu binti kuwa nyie mmeoana na hata umri wenu hawezikujilinganisha nanyie,inampasa atumie muda wake kwenye masomo na sio ufuska,pia anatakiwa ajue kuwa yeye hapo alipo atakuwa anavunja amri ya Mungu na ambayo hakuna dini inayoruhusu,ila anatakiwa ajue wazi kuwa baada ya kumaliza masomo yake atapata muda wa kutosha kwa yeye kujiingiza kwenye hayo mambo na hakuna atakayemuingilia.

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,180
14,319
Una nafasi kubwa sana ya kukaa nae na kumweleza hatari iliyoko mbele yake na kumwambia tuu kuwa wanaume ni wabaya wakati yeye anaona mama na baba wanakaa pamoja na wanapendana sio suluhisho
Mweleze hatari ya mampenzi kama kupata magonjwa ya zinaa na ukimwi na mimba zisizotarajiwa
Tena kwako wewe baba ni afadhali zaidi kuliko mama maana wanasemaga watoto wa kike wako karibu sana na watoto wao wa kike
Una nafasi na wewe itumie kama mzazi kumweleza hatari iliyoko mbele yake na ondoa hilo la kumwambia kuwa wanaume ni wabaya

Vaislay

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
4,532
1,814
Shida ya watoto wa sikuhz ukiweka get ataruka,usimbane mpaka akagundua unambana,ila anahtaj kuongea nae mara kwa mara na kupewa mifano iliyo hai.

bombu

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,127
542
Siku zote huwa nasikitishwa na kauli za wazazi "mtoto huyu kashindikana". Huwa naamini usemi usemao, sikio haliwezi kuzidi kichwa, na maneno huumba. Siku zote mtoto hapaswi kumshinda mzazi, Ongea naye taratibu, na pengine aweza kukusikiliza wewe kuliko mama yake, ukiongea nawe kama baba na kumpa ushauri, usioneshe kama umeugundua mchezo aufanyao, bali mshauri in a general way. Mpe madhara ya kujihusisha na mapenzi ktk umri mdogo na faida ya ku"concetrate" kwenye masomo. Mie nilipokuwa Secondary babangu alikuwa mshauri wangu mkuu, aliponishauri nilimsikiliza kuliko ambavyo ningeshauriwa na mama. So take responsibility na usimwachie mama pekee.

0 Reactions
Reply
Top Bottom