Mapenzi ya jinsia moja yaota mizizi mkoani morogoro....maambukizi ya ukimwi nayo yaongezeka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080



HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro inakabiliwa na changamoto ya kukua kwa maambukizi ya Ukimwi, baada ya kushamiri kwa biashara ya mapenzi ya jinsia moja.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Naibu Meya Manispaa ya Morogoro, Lidya Mbiaji, alisema kuwa kumekuwa na tatizo kubwa la kushamiri kwa vichocheo vya ngono, hali inayochangia kukua kwa kiwango cha maambukizi ya Ukimwi katika mkoa huo.

Pia alisema ongezeko la nyumba za kulala wageni nalo limekuwa kichocheo kikubwa cha kushamiri kwa biashara ya ngono zembe.

Aliionya jamii kuepukana na mila na desturi zinazochangia kuleta vichocheo vya kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi, ikiwemo ngoma za unyago zijulikanazo kwa jina maarufu la kunemwa pamoja na mabanda ya kuonyesha video ambayo nje yamekuwa yakionyesha mechi za soka, lakini ndani ya mabanda hayo huonyesha picha za ngono na kusababisha kuleta hamasa ya watu kufanya ngono.

Pia aliviomba vyombo vya habari kusaidia kuelimisha jamii namna ya kujiepusha vitendo vinavyochangia maambukizi ya ukimwi, kwani hali si shwari kutokana na makundi ya watu wanaofanya biashara ya ngono kuvamia Manispaa ya Morogoro.

Alisema hata kwa wasomi wa vyuo vikuu, hali pia si shwari, kutokana na tafiti kuonyesha kuwa wana kiwango cha juu cha kufanya ngono zembe, hivyo kulitisha taifa kupoteza wasomi wake mara baada ya kumaliza masomo yao.

"Kumekuwa na makundi makubwa ya jamii yanayoingia katika hatari ya kupata maambukizi…ukiangalia kundi la wanafunzi, watu masikini na wanawake, hasa wajane changamoto hii inawagusa moja kwa moja," alisema Mbiaji.



MAPENZI YA JINSIA MOJA YAOTA MIZIZI MKOANI MOROGORO....MAAMBUKIZI YA UKIMWI NAYO YAONGEZEKA - MPEKUZI HURU
 
sasa hao wanafanya nini?
Eti na macho wamefumba wanadai eti wanasikilizia utamu
Aaaargh maruweruwe yamezidi kuongezeka.
 
Kizazi hiki kinahitaji kudra za Mwenyezi Mungu kukinusuru na hali mbaya ya mmonyoko wa maadili kwa kiwango hiki! Kama tabia ndiyo hizi, tunajieletea laana na sijui kama taifa letu litaendelea kama tunavyofikiria.
 
kuna takwimu zozote kuhusu hili ongezeko? hard data zitasaidia kupunguza maambukizi kuliko blah blah.

maoni yangu

  1. i hear gesti haziruhusu wanaume 2 in the same room, kwanini wasi-extend this to include watu wasiokwenye ndoa?
  2. wazazi na 'wasamaria wema' wawe wanatoa taarifa za hivyo vibanda vinavyoonesha p0rn videos. nashangaa wanakaa kimya na kuja kulaumu 'mmonyoko wa maadili' wakati hawachukui hatua zozote kusaidia
  3. watoto wafundishwe umalaya ni kujiabisha wao+family, hili nawalaumu wazazi kwa kushindwa wajibu wao. siamini kama hao machangu wameshindwa kabisa kufikiri njia mbadala ya kipato
 
Mengine yote inawezekana ila hilo la kunema wali sidhani kama analifahamu huyo kiongozi, labda anafikiri pia kunemwa maana yake ukeketaji, mie ninavyofahamu kunemwa hakuwezi sababisha maambukizi ya ukimwi.
 
mkuu papaa2015 Morogoro kasoro bahari una mambo makubwa kuliko Dares-Salaam kuna kila starehe hapo Morogoro mjini karibu ujionee mwenyewe walugulu kwa kupenda starehe mwisho.
Mkuu hakuna anayependa mateso katika dunia hii, kama kungekuwa na uwezo kila mtu angependa starehe. La maana Morogoro ni sehemu fikika kirahisi na watu wa mikoa ya Iringa, Dar na Dodoma, kumbe inawezekana kati ya hao wanaopenda starehe wanashirikiana na hao wa mikoa tajwa hapa.
 
Taarifa zilizozagaa pia ni kuwa miongon mwa makund yanayoongoza km wateja wa machangudoa (baada ya kuhojiwa) ni wafanyakazi wa serikali na biashara hunoga zaidi siku za kazi wanapochomoka makazini kwenda kujiburudisha
 
ARV zinasaidia sn..huwez kumtambua kwa kumuona
Ni vigumu hata kukubali maana kuna wengine wanaonyesha dalili zote lkn bado wanapata wateja sasa sijui wanaofanya hivyo nao wanakua tayari walishakua wahanga. Nakumbuka jirani kulikua na mgonjwa lkn wamama waliendelea kumfuatilia tu japokua alikua wakati mwingine anazimika . Akisha kua poa tu wanae.
 
Back
Top Bottom