Mapenzi si pesa ila pesa huleta mapenzi

Mtuache

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
251
636
Habari za muda wana JamiiForums

Leo nimeona nije na mada hii tubadilishane mawili matatu juu ya mahusiano.

NB: Nikisema pesa huleta mapenzi simaanishi mabillioni au mamilioni ya pesa.

Binafsi naamini kwa 100% kuwa mapenzi ya kweli sio pesa. Nikimaanisha kuwa Mwanamke/Mwanaume akikupenda kwa dhati kabisa hatoangalia ni kiasi gani cha pesa unacho.

Hii inathibitishwa kwa uwepo wa watu walio na hali ya chini ya kiuchumi (Masikini) lakini wanapenda tena kwa dhati kabisa. Sio hao tu, kuna matajiri kibao ambao wamekuwa na wenza wao tangu wakiwa hawana kitu wakapendana na mpaka leo wapo katika mapenzi ya dhati. Na wapo matajiri ambao ndoa zao zina migogoro mpaka kufikia hatua ya kuachana. Kama ingekuwa mapenzi ni pesa basi wasingeachana(mifano tunayo)

tukirudi kwenye mada. Mapenzi sio pesa lakini Pesa huleta mapenzi ni kwa namna gani basi? Tiririka nami hapo chini

Wanawake huzama penzini kwa kusikia, wanaume huzama penzini kwa kuona. Mwanaume atamuona mwanamke atavutiwa nae atamfata kumshawishi. Hapo kwenye ushawishi ndo kuna vitu vingi sana

Unaweza kumshawishi kwa zawadi aidha ndogo au kubwa. Asilimia kubwa sana ya wanawake wanapenda kupewa zawadi. Kama ukigundua mwanamke unayemtaka anapenda zawadi basi usiache kumletea hata mkishakuwa wapenzi, wanandoa mkazaa na watoto kamwe usiache.

Zawadi ni pesa. Nikimaanisha kama ni nguo utanunua, cheni sijui saa utanunua perfumes zinauzwa kwahiyo utatumia pesa kununua. Simu, vipodozi, matunda, viatu, kila kitu utanunua. Nadhani hapo tumeanza kuelewana kuwa pesa huleta mapenzi.

Chukua mfano unapigiwa simu na mpenzi wako anayekupenda sana akakwambia anaumwa. Na wewe huna hata mia nina uhakika jibu lako halitacheza mbali na "ugua polee mpenzi wangu nitakuombea upone haraka, usiache kunywa maji mengi". Chukua huo huo mfano ila sasa wakati huo unayo pesa alafu umjibu hivi "oh polee mpenzi, jiandae nakupitia twende hospitali" alafu muda unaenda kumpitia unambebea zawadi ambazo zinamfaa mgonjwa. Unampeleka hospitali nzuri, mnatoka hospitali mnapitia sokoni unamnunulia matunda, mkifika nyumbani unampikia chakula kizuri anachopenda alafu unamuachia na pesa kidogo ya kutumia.

Hizo situations mbili zinakupa picha kuwa mapenzi si pesa lakini pesa huleta mapenzi. Mgonjwa hakupiga simu kusema baby naumwa nitumie hela. Lakini pesa ilitumika kuonesha kiasi gani mgonjwa anajaliwa.

Situations ziko nyingi sana. Unaweza kuzifikiria au ulishawahi kuzipitia katika maisha ya kawaida.

Hakuna mwanaume ambae hapendi mwanamke wake asipendeze. Mwanamke anavyopendeza anazidi kumvutia mwanaume wake kumpenda zaidi. Dunia ya sasa ili mwanamke apendeze lazima utumie pesa.

Familia ambayo haina pesa haiishi migogoro, kugombana kwao ni jambo la kawaida, simaanishi matajiri hawagombani lakini masikini wamezidi. Ni kawaida sana kukuta Mama na Baba wanagombana adharani mbele ya watoto mbele ya watu wengi kwenye familia ya kimasikini tofauti kabisa na familia za kitajiri.

Fikiria huu mfano:- wewe ni mwanachuo na mwenza wako mwanachuo. Wote mnasoma na hamna kazi, hamna pesa mnategemea wazazi. Ikatokea bahati mbaya mwanamke akakosa ada. Wewe mwanaume huna pesa umetafuta umekosa kwahiyo huwezi fanya lolote. Mwenzako akaacha masomo wewe ukaendelea. Of course hawezi kukuchukia kwanini unaendelea kusoma na hawezi kuacha kukupenda kwanini umeshindwa kumlipia ada. Lakini kama ungekuwa na pesa au ungepata vyovyote vile ukaweza kumlipia naamini penzi lake kwako lingeongezeka.

Kuna watu watasema mbona wengine walilipiwa ada bado wakawa wasiliti. Penzi halijengwi na kitu kimoja. Pesa tu haileti mapenzi, ila ni kisababishi kikubwa sana kwenye kuleta mapenzi. Unaweza kuwa na pesa lakini huna muda na mwenza wako.

Kwa leo naomba niishie hapo. Karibuni kwa maoni, share your experience ni kwa namna gani pesa ni muhimu kwenye mapenzi. Situations zipi unaona kabisa kama pesa ingekuwepo ingesaidia jahazi lisizame.

KARIBUNI.
 
Back
Top Bottom