Bishanga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2008
- 15,323
- 10,050
Yaani ukisikia stori za kinamama wanavyokwenda kwa Kalumanzila utachoka kabisa.Kusema kweli kinababa sijui huwa tunalishwa uchafu kiasi gani.Wengine nasikia wanawapikia waume zao kwa maji yanayoosha maiti mochware,wengine nasikia wanachukua vipande vya nyama wanavisokomeza kusikotamkika kisha wanawakaangizia waume zao,ili mradi ni waganga kutaka kuzidiana ufundi. Jamani jamani uuuuuuwwwwiiiii,huko kwa mahawara ndo usiseme,ndo hakufai kabisa maana hawara ndo anakuwa anahangaika umsahau mkeo.Inachosha kabisa!