Mapenzi mapenzi jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi mapenzi jamani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by dave80, May 14, 2010.

 1. d

  dave80 Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walienda Kwenye Daraja Kujiua Lakini...
  [​IMG]
  Ivanov na Maria mbele ya daraja walilotaka kujiuaThursday, May 13, 2010 8:32 PM
  Walienda kwenye daraja kwa nia ya kujirusha kila mmoja akiwa na sababu zake mwenyewe za kuhitimisha maisha yake lakini bila kutarajia badala ya kujiua waliangukia kwenye mapenzi na hivi sasa wanategemea kuoana.Andriej Ivanov, 26, wa nchini Urusi alienda kwenye daraja la mji wa Ufa katikati mwa Urusi kwa nia ya kujirusha ili afariki.

  Ivanov aliamua kujiua baada ya mchumba wake kufariki siku moja kabla ya harusi.

  Lakini Ivanov alipofika kwenye daraja hilo alimkuta mwanamke aliyejulikana kwa jina la Maria Petrova, 21, akiwa anang'inia kwenye machuma ya daraja akiwa tayari kujirusha ili ajiue.

  Maria kwa upande wake aliamua kujiua baada ya wazazi wake kumfukuza nyumbani kwao alipopata ujauzito kabla ya kuolewa.

  Ivanov alipomuona Maria anajiandaa kujirusha darajani, aliamua kuingilia kati na kuanza kumsihi asijiue.

  "Kuna hisia zilinijia na sikutaka kumwachia Maria ajiue ingawa mimi mwenyewe nilikuwa na masaibu yangu yaliyonivunja moyo", alisema.

  "Alibadili uamuzi wake wa kujiua, alilala mikononi mwangu huku akilia sana, nami ndipo nilipoanza kulia pia".

  Ivanov aliezea jinsi walivyotumia siku hiyo pamoja wakipiga stori mpaka asubuhi na kuahidiana kusaidiana kupeana moyo baada ya masaibu yaliyowakuta.

  Ivanov na Maria waligeuka kuwa wapenzi baada ya siku hiyo na hivi sasa wanapanga kufunga ndoa.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  Walikuwa wana beep kifo.
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kweli mipango ya Mungu ni ya ajabu.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Duuuuhhhh! Hii story imenigusa kishenzi. Ahsante sana kwa kuiweka hapa.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. T

  Tall JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  mtu aaetajataja kujiua kuna siku tu ataja jiua. SIJUI HIYO FAMILIA ITAKUWAJE?
  WANA JF KUJIUA SI SOLUTION. UNAACHA UGALI,JF.......NA MWISHO NI MOTO WA MILELE.
   
Loading...