Mapenzi kazini ni sawa na kujifunga bomu kichwani!

Annina

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
437
57
Jamani ukitaka kujua ubaya wa mapenzi, anzisha mahusiano ofisini maana ni sawa na kujifunga bomu kichwani ukisubiri likulipukie wakati wowote!

Mahusiano kazini yasipoathiri utendaji wako (kama vile kutoa upendeleo maalum kwa mpenzi, kutumia muda wa kazi kwa ajili ya mambo binafsi na mpenzi nk) na kukusababishia matatizo kazini, basi mahusiano yakivunjika pia ni balaa jingine, visa, visasi, chuki vinatawala na kufanya mazingira ya kazi kuwa magumu.

Tuchukue tahadhari...
 
From business point of you sijui huko kazini...kwenye biashara ni hasara na inakula kwako, inakula mtaji lazima utarudi kukopa benki, never entartain..
 
ni kweli kabsa. nilishuhudia watu walikuwa wapenzi wakaachana. Baada mbaya kipindi fulani wakawa wote kwenye project moja mwanaume akiwa project manager na dada akiwa assistant, ilikuwa vituko na video. Hata tuliokuwa hatujuhi kuwa walihi kuwa wapenzi tulijua na kuwa walitofautiana. na kazi zilikuwa haziendi vizuri kwa sabb ya tofauti zao hizo.
 
Sasa ikitokea nimemzimikia msichana na tuko nae ofisi moja inabidi nife na tai shingoni kwa kuogopa kuharibu mambo kazini?

Mimi ninadhani kwamba inategemeana na wahusika wenyewe na wana-draw mipaka ya kazi na mahusiano kwa kiasi gani. Unaweza kuwa na gf/bf ambaye anafanya kazi ofisi/kampuni tofauti, lakini kila siku yuko ofisini na kasheshe kibao. Hapa ninaona ni swala la hulka, na siyo kwamba watu wakiwa ofisi moja basi watashindwa kutenda haki.

Ninakubaliana kunaweza kuwa na conflict of interest na hasa kama ofisi inaendeshwa kiswahili bila kufuata kanuni/taratibu/sheria za kazi. Hapo mtu anaweza kupendelea wazi na asifanywe chochote. Lakini kama sheria zipo, ikitokea jamaa kapendelea basi sheria zitafanya kazi.
 
Ni hatari sana hii mchezo! Kuwa na mpenzi eneo lolote unalotafutia rizki ni shida tupu. Hata mwenye genge la nyanya atamhonga bi Chausiku wee, hadi afilisike. But to your surprise, lots of employees do run this errand in office. Unashangaa jioni bosi yupo ofisini, na dada Mwatano anasema anabaki, kisa, eti ana kazi anaimalizia, kumbe mmmhh!...haya!
 
jamani ukitaka kujua ubaya wa mapenzi, anzisha mahusiano ofisini maana ni sawa na kujifunga bomu kichwani ukisubiri likulipukie wakati wowote!

mahusiano kazini yasipoathiri utendaji wako (kama vile kutoa upendeleo maalum kwa mpenzi, kutumia muda wa kazi kwa ajili ya mambo binafsi na mpenzi nk) na kukusababishia matatizo kazini, basi mahusiano yakivunjika pia ni balaa jingine, visa, visasi, chuki vinatawala na kufanya mazingira ya kazi kuwa magumu.

tuchukue tahadhari...


kuna binti hapa ofisini yupo idara tofauti kabisa na yangu,
niko ghorofa ya nne yeye ya kwanza,
je kuna ubaya nikizamisha kwenye dimbwi la mapenzi na binti huyu?
 
kuna binti hapa ofisini yupo idara tofauti kabisa na yangu,
niko ghorofa ya nne yeye ya kwanza,
je kuna ubaya nikizamisha kwenye dimbwi la mapenzi na binti huyu?

hahaha bujibuji anzisha tu hakuna tatizo
 
Mapenzi kazini ni sumu na haitakiwi imagine unaweza kuwa PS wa boss na mkawa katika malav davi inatokea wageni wa kike wakiingia unanuna Presha inapanda presha inashuka na kazi inakushinda
mahusiano hayo si mazuri hata kidogo ..mnakosa uhuru ,pia utendaji wa kazi unaweza kuwa sio mzuri ...kula nanasi kunahitaji nafasi
 
Pengine muwe wawazi zaidi,mngesema uasherati na uzinzi kazini ni sumu.Lakini ukisema mapenzi sidhani kama ni sahihi,vp kama ukiwa na mke au mme hata mchumba hapo kazini,sumu inatoka wapi?
 
Pengine muwe wawazi zaidi,mngesema uasherati na uzinzi kazini ni sumu.Lakini ukisema mapenzi sidhani kama ni sahihi,vp kama ukiwa na mke au mme hata mchumba hapo kazini,sumu inatoka wapi?
ha ha haaa, naona ZD umetoa from bible's point of view.
Hata mimi naona ni hatari kuwa na mahusiano sememu ya kazi, its too uncomfortable i guess.
 
Keil kama ulikuwa kichwani kwangu!

Si wanasema mapenzi ni maua popote huchanua? na mara nyingi mtu hupenda pale anapopaona na kuwa karibu napo mara kwa mara kwa maana ya kwamba maofisini ndio mahali panapokutanisha watu na kuwafanya wakae kwa muda mrefu kiasi cha kujuana tabia na kuwa attracted sasa mtu akijikuta anampenda mwenzi wake afanyeje? Na hii ndio huwa ninaiquestion kwenye yale mashirika yanayokataza watu wawili kufall in love. Nway pengine wanao uelewa tofauti na wangu mie!
 
Vimada kazini ndio soo. Kuna mtu alibwagiwa watoto kazini na mkewe.Na hilo lilitokea baada ya mama kuja moja kwa moja kupambana na mtuhumiwa wake na kuleta vurugu kubwa.Ilikuwa aibu kweli.
 
Jamani ukitaka kujua ubaya wa mapenzi, anzisha mahusiano ofisini maana ni sawa na kujifunga bomu kichwani ukisubiri likulipukie wakati wowote!

Mahusiano kazini yasipoathiri utendaji wako (kama vile kutoa upendeleo maalum kwa mpenzi, kutumia muda wa kazi kwa ajili ya mambo binafsi na mpenzi nk) na kukusababishia matatizo kazini, basi mahusiano yakivunjika pia ni balaa jingine, visa, visasi, chuki vinatawala na kufanya mazingira ya kazi kuwa magumu.

Tuchukue tahadhari...




Hilo nakubaliana na wewe kabisa, maana hata kwenye maamuzi unakuta yule mwanamke ndiye anatoa badala ya boss mwenyewe. Hata katika kupandishwa vyeo anasikilizwa mwanamke aseme ndiyo unapandishwa kwa hiyo kama huna uhusiano mzuri na huyo mwanamke wa boss imekula kwako.

Na hasa katika mashirika ya umma na Serikali ndiyo wamezidi kuwa na wapenzi maofisini matokeo yake hatuendelei wala hakuna mabadiliko.kazi ni kungonoka tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu! inasikitisha kwa kweli.
 
Mapenzi kazini ni sumu na haitakiwi imagine unaweza kuwa PS wa boss na mkawa katika malav davi inatokea wageni wa kike wakiingia unanuna Presha inapanda presha inashuka na kazi inakushinda
mahusiano hayo si mazuri hata kidogo ..mnakosa uhuru ,pia utendaji wa kazi unaweza kuwa sio mzuri ...kula nanasi kunahitaji nafasi

haswa!!!!!!!! afu tena kushinda na mtu all the time aaah, unakinai kabisaaa!!! siwezi hata kutumia neno 'hun nimekumis'... mda wote tuko pamoja!

Boring!! plus hayo nlo yakoti hapo ya FL!!
 
Ngoja niwape mchapo mmoja, wangu binafsi. Mume wangu tulianza mapenzi kiutani tukiwa ofisi moja, yeye kama Supply officer nikiwa Administrative assistant. Tumeenda vizuri akanikandamizia engagement, baada ya miezi sita akanioa kabisa tukaendelea vizuri tu. hakuna fujo wala kuoneana wivu wa kipumbavu.

Tumekaa waingereza wakaichukulia tofauti, wakatupa option kati yetu mmoja aache kazi, ikaonekana mimi ndiyo niache maana tayari nilikuwa mjamzito na kiwango cha msharaha haikukuwa kikubwa kama cha mume.

Kasheshe ikaja, pale wanapotakiwa kuniachisha kwa manufaa ya kampuni, kupiga hesabu ya kunilipa wakagundua nitakuwa tajiri wakaniacha wenyewe maana hatukuwa na tatizo lolote sema.

Kuwa na mpenzi sehemu ya kazi lazima muwe displined na muwe mnapendana sana na malengo juu. siyo kukandamizana tu au kula good time then kila mtu kivyake.

Sioni tatizo la kufanya na mwenza wako au la.
 
Bomu la mapenzi kazi linakufuata hata na nyumbani, linaweza kulipuka na kuangamiza nyumba yako, mpenzi wako na watoto. Kwa wale wasio na wenzi, kazini si vema kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Kama itatokea ukawa na mtu unayehisi anaweza kuwa mwenzi wa maisha hapo kazi kwako, ni vema kutafuta muda mwingine nje ya kazi na kuongelea juu ya mapenzi na mstakabali wa maisha yenu. Vile vile mahusiano yenu hata na maandalizi yenu ya maisha ya ndoa yasiingiliane na majukumu yenu ya kikazi
 
Bomu la mapenzi kazini linakufuata hata na nyumbani, linaweza kulipuka na kuangamiza nyumba yako, mpenzi wako na watoto. Kwa wale wasio na wenzi, kazini si vema kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Kama itatokea ukawa na mtu unayehisi anaweza kuwa mwenzi wa maisha hapo kazi kwako, ni vema kutafuta muda mwingine nje ya kazi na kuongelea juu ya mapenzi na mstakabali wa maisha yenu. Vile vile mahusiano yenu hata na maandalizi yenu ya maisha ya ndoa yasiingiliane na majukumu yenu ya kikazi
 
Inakuwa ngumu kiasi kujizuia 100% kutoonyesha signs za mapenzi muwapo kazini. Hii inaweza hata kuwaboa staff wenzenu na wale wenye wivu wakaanza kuchonga.
 
Back
Top Bottom