Mapenzi haya! Nimeenda kwetu kujifungua kurudi namkuta na mwanamke mwingine

jane26

Member
Nov 9, 2016
27
18
Samahanini wana JF,

Naomba ushauri,

Nina mume nipo naye mwaka wa nne na tumepata mtoto mmoja wa kiume, lakini cha kushangaza nilipojifungua nimeenda kwetu kurudi nakuta anamwanamke mwingine na bila kujua kumbe kabla yangu anamtoto mwingine.

Nilipomuuliza alisema walishindwana kisa dini, baada ya hapo ndo kanipata mimi lakini baada ya kurudi nyumbani naona anamwanamke mwingine tena kamzidi umri, nikimuuliza ananipiga, kumbe yule mwanamke anamimba na ninavyoongea sasahivi ameshajifungua mtoto.

Nilipojua inauma sana na kumpeleka kwa ndugu zake akatubu kweli mtoto wake akasema alipitiwa lakini cha ajabu bado anaendelea na huyo mwanamke
ukimuuliza anasema mtoto anaumwa nilienda kumwona.

Huwa ananiaga anaenda kanisani kumbe anaenda kwa huyo mwanamke alafu anataka mtoto akikuwa aniletee mimi wote nyumbani. Jamani naumia sana na sijawahi kumsaliti na natimiza kazi zangu zote kama mke.

Naombeni ushauri jamani maana hali tete.
 
Samahanin wana jr,naomba ushaur nina mme nipo naye mwaka wa nne na tumepata mtoto mmoja wa kiume,lakin cha kushangaza nilipojifungua nimeenda kwetu kurud nakuta anamwanamke mwingine,na bila kujua kumbe kabla yangu anamtoto mwingine.
Nilipomuuliza alisema walishindwana kisa dini,baada ya hapo ndo kanipata mm,lakin baada ya kurud nyumban naona anamwanamke mwingine tena kamzid umr,nikimuuliza ananipiga kumbe yule mwanamke anamimba na navoongea sahv ameshajifungua mtoto.
Nilipojua inauma sana,na kumpeleka kwa ndugu zake akatubu kweli mtoto wake.akasema alipitiwa lakin chaajabu bado anaendelea na huyo mwanamke
Ukimuuliza anasema mtoto anaumwa nilienda kumwona.huwa ananiaga anaenda kanisan kumbe anaenda kwa huyo mwanamke alafu anataka mtoto akikuwa aniletee mm wote nyumban.
Jaman naumia sana,na cjawah kumsalit na natimiza kaz zangu zote kama mke.
Naomben ushaur jaman maana hali tete.

Dah!

Sasa sisi tukupe ushauri gani?

Ingependeza kama naye ungemleta humu ili walau naye tumsikilize ana nini cha kusema kabla ya kutoa ushauri.

Hapa ukipewa ushauri utakuwa ni ushauri ulioegemea taarifa za upande mmoja tu, jambo ambalo si la kibusara sana.
 
Vitu vingine ni mitihani nyie acheni tu
Kuna watu hatupendi kusema ukweli mapema ili kuseto mambo mapema . wengi tunaficha suala la kuwa tayari tulishazaa tukihofia kutokukubaliwa mwisho wa siku inaleta mushkeli kama hivo
Mi kama nimemmpenda mwanaume akanieleza ukweli mapema kuwa alishazaa walaa sina tatizo tena namwambia amlete mtoto nitamlea vizuri raha mustarehe kama navowalea wanangu
Kimbembe kinakuja ikiwa too late alishanificha lol
It hurts.
 
Samahanini wana JF,

Naomba ushauri,

Nina mume nipo naye mwaka wa nne na tumepata mtoto mmoja wa kiume, lakini cha kushangaza nilipojifungua nimeenda kwetu kurudi nakuta anamwanamke mwingine na bila kujua kumbe kabla yangu anamtoto mwingine.

Nilipomuuliza alisema walishindwana kisa dini, baada ya hapo ndo kanipata mimi lakini baada ya kurudi nyumbani naona anamwanamke mwingine tena kamzidi umri, nikimuuliza ananipiga, kumbe yule mwanamke anamimba na ninavyoongea sasahivi ameshajifungua mtoto.

Nilipojua inauma sana na kumpeleka kwa ndugu zake akatubu kweli mtoto wake akasema alipitiwa lakini cha ajabu bado anaendelea na huyo mwanamke
ukimuuliza anasema mtoto anaumwa nilienda kumwona.

Huwa ananiaga anaenda kanisani kumbe anaenda kwa huyo mwanamke alafu anataka mtoto akikuwa aniletee mimi wote nyumbani. Jamani naumia sana na sijawahi kumsaliti na natimiza kazi zangu zote kama mke.

Naombeni ushauri jamani maana hali tete.
Usiende kwenu kujifungua tena!
 
Hata nicpoenda c ameshaanzisha mahusiano na huyo ana mtoto wake,lin wataachana?
 
Pole sasa dada kama ulivyosema mapenzi yanauma, najuwa maumivu uliyonayoo,kwa vyovyote sasa hivi huna maamuzi ya kuondoka kirahisi maaana ni jambo ambalo hukupanga!!!!!! haya hutukuta wote wanaume kwa wanaume na kwa hali ilivyo naamini lazima binadamu apitie mauumivu haya maishani. Nakushauri vumilia lea watoto mwache aruke ruke hayo yana mwisho kwake.Pole sana bi dada
 
Back
Top Bottom