Mapenzi haya, hebu tumshauri huyu mwanaume karudisha mabegi

LadyAJ

JF-Expert Member
Oct 21, 2015
7,173
9,631
Juzi nimepata mtihani kwa kweli sina cha kumshauri huyu ndugu yangu ni mwanamke ana miaka 29 ana mtoto mmoja aliyezaa na mwanaume wa Tanga nimpe jina la X mwenye miaka 40 (Mimi humuita kaka) na kutokana na sababu zao za kikazi mwanaume anaishi Dar mwanamke anaishi Tanga (wote ni waajiliwa).

Kwa nilivyoona mimi mwanzo wa mapenzi yao walipendana japo kwa muda mchache wa likizo (mwanamke ni Mwalimu) mwanamke alikua akiutumia Dar kwa wenziwake,yaonyesha alipokua akiondoka basi huku nyuma mwanaume alikua akifungulia wanawake wengine mpaka kufikia kumpa mimba mdada mmoja anayesemekana aliishi kwenye ndoa miaka 10 bila mtoto ndipo jamaa (X) akamtungisha mimba awali alifanya siri kwa Girlfriend wake ambae watoto wao kwenye kuzaliwa walipishana miezi 7.

Baadae mwanaume akaona amueleze huyu Mwl wa Tanga kua amezaa na mwanamke mwingine lakini kwa madai yake ya wakati ule alidai hana mpango na huyo mwanamke, ila huyu dada Mwl yeye ilimuuma kuona mwanaume wake kam cheat mpaka kuzaa na mwanamke mwingine matokeo yake ikawa ni maugomvi kila wakati na bwana wake mwisho waliachana wakati mtoto akiwa na miezi mi 3 tu'

Mwanamke alikua akija ananililia sana kulalamika kwann X alimtenda hivyo na kumpotezea muda ila Mimi kama mzazi nilikua nikimtia moyo tu kua ipo siku wataelewana kama Mungu alimpangia awe wake wakwe wa Tanga wanafiki tunajuana wenyewe kwetu kule ukimleta mwanamke huyu ukimleta yule wao wanapokea tu wala hawamuhoji kijana wao, Mwl. Akaamua ajiweke pembeni mbali na wakwe zake na hata jamaa.

Sasa Bi Dada kanijia ananiambia baba mtoto wake kamtafuta kamuomba msamaha anamuomba warudiane baada ya kuachana tangu 2015 mtoto akiwa na miezi mi 3 sasa ana miaka mi 3 kasoro miezi mi 2 ameenda Deep na kusema ukweli ana mpenda baba mtoto wake sana na tangu hapo yeye hajawahi kua na mwanaume mwingine Kwani anawaona hawa fit kwenye moyo wake hivyo kurudi kwa jamaa anakufurahia japo kunamtia wasiwasi na kutokua na imani nae hivyo amemuitikia tu japo moyo unamsita sita.

Mimi nimemwambia asikilize moyo wake,japo awe makini nae lakini pia ni wakati sasa waache kuzini Kama kweli huyo bwana amerejea mazima basi aanze kurasimisha mahusiano yao yawe ya heshima kwa M/Mungu na hata kwa binadamu,jibu alilopewa ni kwamba mwanaume ameomba wapeane miezi mi 4 waangaliane kama wanaweza kwenda kwenye hatua ya ndoa.

Binafsi yangu sifurahii huyu dada kurudiana na mbondei yule ila najua huyu dada anampenda sana mwanaume wake na kwa miaka yote hii mwanaume amekua mbali amekua akiishi kwa masikitiko sana
 
Haya mambo hatari tupu,


Wengine wanasema "Moyo sukuma damu na si vingine" lakini wengine mnasema ausikilize moyo.....!

Miaka mitatu ni mingi mno alitakiwa kuwa alishafanya maamzi tayari bt ajiandae kuumia zaidi na zaidi lakini ajue akili ni kitu mhimu ktk mapenzi ikistack ni hatari tupu.
 
Lady Naona rafiki yako kashafanya maamuzi....


Ingekuwa hajafanya ningemshauri asirudiane na huyo jamaa ila kwa ndoa tu. Wachunguzane tena nini wakati walishaishi na kuzaa wote?

Angemwambia Kama unataka turudiane Tangaza ndoa kwanza.


Je mtoto alikuwa anahudumia????
 
Tangu nimshauri rafiki yangu wa karibu ambaye alikuja home kuniomba ushauri baada ya kumfumania guest mpenzi wake ambaye miezi michache ilibaki wange ndoa na jamaa kuapa kuwa amefuta kila kitu cha yule mdada nami kumpongeza kwa maamuzi aliyoyafikia,... Lakini cha ajabu asubuhi yake nilienda mapema nyumbani kwa jamaa kuingia ndani nikamkuta akiwa na yule mdada. Tangu siku hiyo sishauri chochote kinachohusu mapenzi
 
Mapenzi ni matamu nahofia kuumiza moyo, nashindwa kujaribu roho inaniuma sana, rafikiyo kapenda madam, ila hakutakiwa kurudiana nae huyo bwankaka lkn furaha yake ni yeye tutafanyaje!!
Aaah Kapeace usitihukumu Me wote bana, mi sita choka kukupangia mikakati...

Ha ha ha ha
 
Haya mambo hatari tupu,


Wengine wanasema "Moyo sukuma damu na si vingine" lakini wengine mnasema ausikilize moyo.....!

Miaka mitatu ni mingi mno alitakiwa kuwa alishafanya maamzi tayari bt ajiandae kuumia zaidi na zaidi lakini ajue akili ni kitu mhimu ktk mapenzi ikistack ni hatari tupu.
Ni kweli kuu,miaka mitatu hata Mimi nilitarajia awe ameshashukuru Mungu
 
Alifunga naye ndoa?
Hapana, hata posa hajamtolea mwenzangu ndio nimemwambia tu mkirudiana angalau mumpendeze M/Mungu basi mfunge ndoa muda huu naandika huyo mwanaume yupo huko Tanga acheza na mtoto means washarudiana hawa
 
Lady Naona rafiki yako kashafanya maamuzi....


Ingekuwa hajafanya ningemshauri asirudiane na huyo jamaa ila kwa ndoa tu. Wachunguzane tena nini wakati walishaishi na kuzaa wote?

Angemwambia Kama unataka turudiane Tangaza ndoa kwanza.


Je mtoto alikuwa anahudumia????
Nami nilimweleza hilo kwa kinyume nyume Daby maana hatutakiwi kukatisha watu tamaa wala kushiriki kuvunja mahusiano yao ila niliongea nae kama mtu ninayemzidi umri (alisoma na yule Mdogo wangu aliyekua akichezea kichapo mpaka kuzimia) nilimwambia mwambie sasa muende kwenye hatua ya heshima zaidi, aliniambia huyo bwana kakubali ila sasa amesema anataka kumuhakikishia kua yeye huyo bwana kabadilika hivyo ampe hiyo miezi mi 4 kisha wafanye hayo maamuzi ya ndoa ila hakika namuhurumia huyu binti maana wabondei hawaachagi mambo zao wanakwepesha tu
 
Back
Top Bottom