Kwanini wanandoa/wapenzi wanapenda mapenzi gizani

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
26,138
22,709
wana JF.. najua humu ndani kuna wataalamu wengi wa mahusiano..shida yangu ni hii..Mpenzi wangu hayupo comfortable kufanya mapenzi mchana au wakati taa inawaka.. kifupi tumbo lake sijawahi liona laiv na ikulu ndo sijawahi tia jicho.... anatatizo gani... niemuomba mara nyingi tuwashe taa hataki.. na nikifosi washa taa anavaa track za kulalia .... ndo hamna mechi hapo... anatatizo gani?? wapo wengine wako hivyoooo? mawazo yenu ni very helpfull kwangu. Ni binti...mie ni (Me) naomba niwe specific.

Kalunde Jamal, kwenye gazeti la Mwananchi, Jumapili Oktoba 2, 2016 amendika makala yenye kichwa hapo juu. Anasema "tofauti na watu wa mataifa mengine, Waafrika hupenda kufanya mapenzi sehemu yenye mwanga hafifu au gizani".

Kwa Waafrika suala hilo ni siri na linahitaji faragha kukamilika. Sababu kuu ni:
1) Kusukumwa na mila
2) Kuona haya
3) Kukosa kujiamini
4) Kuamini maumbo yao hayavutii
5) Kuponzwa na majarida

Naliweka wazo hilo hapa mkuu "kiwatengu" alifanyie "exclusive interview" ukweli ujulikane.

========

PIC+WANAWAKE.jpg


Wanawake wanapenda mapenzi ya gizani
By Kalunde Jamal,

Dar es Salaam. Inaeleweka kuwa wapendanao iwe wanandoa au wapenzi hupenda kufanya mapenzi sehemu yenye mwanga hafifu au gizani.

Tofauti na watu na mataifa mengine, kwa Waafrika suala hilo ni siri na linahitaji faragha kukamilika.

Lakini kwa baadhi ya watu imekuwa kero kutokana na kutamani kufanya tendo hilo gizani, huku wanawake wakitajwa kuwa vinara wa kuzima taa.

Utafiti mpya umebaini kuwa katika kila wanawake wanne, mmoja anapenda na anakuwa huru kufanya mapenzi gizani kwa sababu mbalimbali ikiwamo kutojiamini.

Carl Loudgers aliyeshiriki kwenye utafiti huo na kuwauliza wanawake zaidi ya 2,000 kwa kukusanya majibu kwa njia ya mtandao anasema walibaini asilimia 60 ya wanawake hao wanatamani kuwa na ujasiri wa kukutana kwenye mwanga lakini wanashindwa.

Anasema zaidi ya asilimia 75 walisema hawapendi miili yao, huku asilimia 66 wakisema wanaona aibu kutokana na mwonekano wao.

Utafiti huo uliofanywa na mtandao wa Weight Watchers, ulibaini asilimia 27 wanafanya mapenzi gizani kwa sababu hawaamini miili yao kama inavutia kwenye mapenzi.

Ulionyesha pia asilimia 38 ya wanawake na wanaume waliohojiwa walisema kuwa wanaamini wapenzi wao hawatawaona wanavutia wakiwa watupu.

Sheiilar Gregam miongoni mwa wanandoa waliohojiwa kwenye utafiti huo alisema jambo linalochangia hali hiyo ni mitandao.

Alisema wanawake wanaoonekana wakiwa watupu kwenye mitandao ni wale wanaovutia kiasi ukijilinganisha nao inakuwa ngumu kukubali kukaa bila mavazi, huku wapo ambao wanavutia.

“Nikiangalia mastaa walivyo na maumbile ya kuvutia, baadhi yao wamezaa, natambua kuwa wapo wanaojirudishia wakiharibika kama mimi baada ya kuzaa, lakini nakosa kujiamini kabisa na ninaamini hao wanapendeza zaidi yangu,” alisema Sheiilar katika mahojiano ya utafiti huo.

Baadhi yao wamekuwa wakiona aibu ya vitu vilivyomo mwilini mwao kama matiti, alama za mwilini na makovu ya upasuaji.

Maziwa kuanguka baada ya kunyonyesha mara tatu.

Kuning’inia nyama za tumbo na kuongezeka uzito ni moja ya sababu za kuzima taa.

Matokeo ya utafiti huo pia umebaini wanawake wawili katika kila wanawake watatu huchukia kuangalia wanawake wenzao wakiwa hawajavaa nguo.

Ulibaini kuwa asilimia 60 ya wanawake hawapendi kabisa kujitizama wao wenyewe kwenye kioo wakati wa kuvua nguo.

Loveness Ayoub mkazi wa Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam anasema hupata wakati mgumu anapokutana na mwanaume mzuri kwa sababu hukosa kujiamini na hivyo hufurahia zaidi wakijamiiana gizani.

Anasema akijitizama na rafiki zake humwambia amenenepa, hivyo akiwa na mwanaume anayevutia huamini atamuacha kutokana na umbo lake lilivyo.

“Tangu nipo chuo rafiki zangu walikuwa wananishangaa nikivua nguo, kiasi kwamba sikuwa nafanya hivyo wakiwepo, hali hiyo imenijengea uwoga na kunipotezea kujiamini.

“Nikiwa na mwanaume mtu mzima huwa sijali kwa sababu naamini ameona wanawake wengi amekuja kwangu kwa ajili ya kupumzika na sihitaji kuwa naye maishani ukilinganisha na wanaovutia ambao natamani hata wanioe,” anasema Ayoub.

“Nimeoa nina watoto wawili na huyo mke wangu, lakini nikitaka kumuona vizuri umbo lake akiwa mtupu nimvizie anaumwa au kalala, tofauti na hapo hajawahi kuvua nguo akakaa mbele yangu,” anasema Omari Kiyungi.

Kiyungi anasema licha ya kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka tisa mkewe hataki kabisa kukaa mtupu mbele yake kwa madai ya kuona aibu.

“Sipendi, natamani nimuone akiwa hajajiziba na ‘manguo’, lakini juhudi zangu zimegonga mwamba, hana dalili hiyo na hataki kabisa,” anasema.

Anasema alikuwa anachukia hadi sasa amezoea na akimuona mwanamke amevaa kihasara hasara anamdharau na kumuona hajiheshimu kwa sababu amezoea kufichiwa maungo.

Alisema akitizama mwili wake kwenye kioo hasa baada ya kuzaa mara mbili na kunenepa huogopa na kuhisi anamuangusha mumewe kwa umbile lake.

Msimamizi mkuu wa utafiti huo na mshauri wa masuala ya saikolojia Keren Smedley alisema wengi wa waliobainika kuona aibu kuvua nguo mbele ya wapenzi wao hawakuwa na tatizo na walikuwa na kila sifa ya kumshawishi mtu kuwatizama.

Akizungumzia hali hiyo mfundaji kutoka Mbagala Charambe, Zakia Kilimi maarufu Mchambaji, anasema wanawake wamekuwa na hali hiyo kutokana na tamaduni za siku za nyuma kuwa mapenzi hufanywa kwa siri.

Anasema wakati huo hasa kwa familia za kawaida walikuwa wanaishi katika chumba kimoja, hivyo upende usipende utazungumza na mwenzi wako gizani.

“Hii hali imesababisha hata wanawake wengi kushindwai kuachia hisia zao kwa wapenzi wao wakiamini wataonekana malaya na wasio na maadili kwa sababu imezoeleka mambo hayo ni ya kunyata nyata,” anafafanua.

Anaongeza kuwa siku hizi hayo mambo ndiyo yanakwisha na wanawake bila kujali wana umbo zuri, baya, makovu wanajiachia na kutambua umuhimu wa faragha ni kuonana hivyo wazazi wasiwatishe watoto wa kike kuwa kujiachia ni uhuni.

Zainabu Jumanne (siyo jina lake halisi) anasema kuwa mpenzi wake anajivunia kuwa naye lakini wakiwa faragha anashindwa kukaa mtupu. Anasema vivyo hivyo hata wanapojamiiana kukiwa giza hufanya kila aina ya mbwembwe tofauti taa ikiwa inawaka.

Anafafanua kwa sababu hiyo mumewe akitaka kuburudika na kukata kiu ya kuzungumza naye faragha huzima taa kabla hajaambiwa.

“Sijiamini kabisa kukiwa na taa, nahisi kama ananichora ninavyoweweseka, lakini kukiwa giza ashindwe yeye tu,” anasema.

Anaitaja sababu nyingine ya kupenda kujamiiana gizani ni matiti yake yamelala halafu hayana nyama.

Anasema anatumia ufundi wa faragha kuziba yote hayo kwa kumuonyesha mitindo mipya, lakini ili ayapate hayo sharti iwe gizani.

“Kukiwa giza akakubali kukutana nami, akiniacha nitatambika sina historia ya kuachwa tangu nikiwa msichana hadi nimeolewa, ingekuwa najiamini na kujamiiana kwenye mwanga na mautundu niliyonayo, naamini ningekuwa mkali zaidi, nimejaribu nimeshindwa na kwa hapa nilipofika haiwezekani tena,” anasema.

Mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam, Yusufali Yusuph anasema hataki hata kumsogelea mwanamke anayependa kujamiiana gizani kwa sababu huamini kuna kitu anaficha.

Anasema siku hizi maradhi mengi, anaweza kudhani anaona aibu au hajazoea kumbe kuna jambo anaficha.

“Haa raha ya mapenzi muonane jamani gizani tena! Siwezi na simtaki mwanamke wa aina hiyo,” anasema Yusuph.

Mtaalamu wa masuala ya saikolojia Modester Kamongi anasema yapo mambo mengi yanayochangia mwanamke kuogopa ikiwamo kutokujiamini.

Anasema mila, desturi na tamaduni ni miongoni mwa mambo yanayochochea hilo kwa sababu wanawake wengi huamini stara ndiyo sifa ya kuwa mke bora na kushindwa kutofautisha mahali pa kujistiri pa kujiachia.

Kamongi anasema linapokuja suala la aibu siyo kwa wanawake pekee wapo wanaume wenye aibu na wameumbwa hivyo, ikitokea kukutana na mmoja wa watu hao cha kufanya ni kuwazowesha taratibu hatimaye kama binadamu watakubaliana na hali halisi japo kwa shida.

“Huwachukua muda kuzoea, lakini uwezekanao upo na wakasahau kabisa kama walikuwa hawawezi, lakini inahitaji utayari wa kuwazowesha badala ya kuwalazimisha, ”alisema Kamongi.

Anaitaja sababu nyingine inayochangia wanawake kukataa kukaa utupu kuwa ni kutojiamini.

Anasema hali hii hutokana na maneno anayosikia au aliyosoma kuhusu umbo lake.

Anafafanua kuwa kuna baadhi ya familia mtoto akiwa mnene au mwembamba au ana umbo fulani uhusisha umbo hilo na neno ukiolewa sijui itakuwaje.

“Mtoto hukuwa na neno au misemo ya aina hiyo hivyo anapoolewa au kuwa na mpenzi hukumbuka na kutamani asimuone kwa sababu hajui itakuwaje kama alivyokuwa anaambiwa.

“Wengine hudhani mwanaume akiona umbile lake ambalo lilikuwa linawaisha ndugu, rafiki zake litamtisha pia na kuamua kumuacha, hivyo huona afadhali nusu shari kuliko shari kamili ya kuachwa,” anasema Kamongi.

Anaeleza wote hao wanaweza kubadilika iwapo wataeleweshwa na kujengewa kujiamini ikiwamo kwa kusifiwa kila wanapokaa bila nguo hata kwa bahati mbaya.

“Wengi wao hawajiamini, wakisifiwa na muhusika kuonyesha kutamani kuona maumbile yao mazuri yakiwa wazi taratibu watabadilika,” anasema.

Ushauri wazazi wawajenge watoto wa kike kuthamini vile alivyo navyo hususan kuukubali mwili wake badala ya kuwasema kwa ubaya kwa eneo lolote la mwili lililozidi au kupungua.

Chanzo: Mwananchi

Jaman Wana MMU hukunajua kuna hadi watoto maliobalehe leo ila wanajua mgegedo.kwahio watanijibu
swali ni kwanini baadhi ya wanandoa au wapenzi wanapenda kugegedana gizani kama ni usiku basi taa zinazimwa na wakati mpo wenyewe mapazia milango mmefunga hakuna anae waona inamana nikutokujiamini,aibu ,au hamjazoeana
nazungumzia usiku maranying ndo muda wa wagegedanao kugegedana baada ya pilika za mchana kutwa.
huku kwa wanatafsida wakubwa wenzangu tutakutana kwenye uwanja wa burudani wa kuchambua mchele na chuya
 
Hajiamini ndio maana!Sema nae kwa sauti ya mahaba umsifie mpaka ajisahau!

baby girl.. nimejaribu mara kibao kaa na kitandan huku taa inawaka... napiga nae story nzuuri za mahaba.. nikianaza peleka mkono.. anasema ..zima taa..
 
Vipi ulishawahi kuoga nae(namaanisha kuoga kwa pamoja wote wawili) au labda kuenda nae beach? Huko hali inakuwaje?
 
Heshimu maamuzi yake, wala usimlazimishe. Tafuta lugha laini ambayo itamshawishi kuwa vyovyote atakavyo yeye ni sawa, lakini pia hakuna tatizoiwapo kutakuwa na mwanga. Pia weka mazingira ya kukubaliana na hali yoyote utakayoiona kwake kwani inawezekana akawa amekeketwa na hataki ujue!
 
wana JF.. najua humu ndani kuna wataalamu wengi wa mahusiano..shida yangu ni hii..Mpenzi wangu hayupo comfortable kufanya mapenzi mchana au wakati taa inawaka.. kifupi tumbo lake sijawahi liona laiv na ikulu ndo sijawahi tia jicho.... anatatizo gani... niemuomba mara nyingi tuwashe taa hataki.. na nikifosi washa taa anavaa track za kulalia .... ndo hamna mechi hapo... anatatizo gani?? wapo wengine wako hivyoooo? mawazo yenu ni very helpfull kwangu. Ni binti...mie ni (Me) naomba niwe specific.

Klorokwini psychological analysis.

possibilities

Ana woga wa kizembe: So pengine wewe una sura mbovu na ukiwa katika ile shuhuli unang'aruza mimacho na mimeno unatoa nje, hii inamtisha na kumkata stimu, ameonelea bora gizani ili asikuone.

Mambo ya kiswahili (ushirikina): pengine amefundwa hivyo kwa taratiib maalum za kifamilia

Mchumi: ameamua kusave bill ya umeme ili mnunue kabajaji.

Anafeki: Haumfikishi kileleni so anafake na anahisi utamshtukia akifake mchana kweupe (low self confidence)

Aibu: amekuwa na kufunzwa kuwa ngono ni aibu.

Extra sex abnormal activities (ambayo pia ni sub heading ya aibu) : ana mambo ya ajabu anafanya wakati wa kungonoka na hataki wewe uyaone na hayakubaliki kijamii na kimaadili.

Post litakuwa refu acha niishie hapa.
 
salute mkuu...nadhani ya uchumi ina sound zaidi!
Klorokwini psychological analysis.possibilitiesAna woga wa kizembe: So pengine wewe una sura mbovu na ukiwa katika ile shuhuli unang'aruza mimacho na mimeno unatoa nje, hii inamtisha na kumkata stimu, ameonelea bora gizani ili asikuone.Mambo ya kiswahili (ushirikina): pengine amefundwa hivyo kwa taratiib maalum za kifamiliaMchumi: ameamua kusave bill ya umeme ili mnunue kabajaji.Anafeki: Haumfikishi kileleni so anafake na anahisi utamshtukia akifake mchana kweupe (low self confidence)Aibu: amekuwa na kufunzwa kuwa ngono ni aibu.Extra sex abnormal activities (ambayo pia ni sub heading ya aibu) : ana mambo ya ajabu anafanya wakati wa kungonoka na hataki wewe uyaone na hayakubaliki kijamii na kimaadili.Post litakuwa refu acha niishie hapa.
 
Vipi ulishawahi kuoga nae(namaanisha kuoga kwa pamoja wote wawili) au labda kuenda nae beach? Huko hali inakuwaje?

sijawaza kuomba nioge nae.. sidhani kama atakubali
 
Na mwanga wa mchana nao analipia?!
wa usiku wahusika zaidi kwani utaongeza billwa mchana nadhani anawaonea imani watumiaji wa solar...asiwapunguzie nguvu.halafu game raha yake usiku mkuu.mchana kazi.
 
Klorokwini psychological analysis.

possibilities

Ana woga wa kizembe: So pengine wewe una sura mbovu na ukiwa katika ile shuhuli unang'aruza mimacho na mimeno unatoa nje, hii inamtisha na kumkata stimu, ameonelea bora gizani ili asikuone.

Mambo ya kiswahili (ushirikina): pengine amefundwa hivyo kwa taratiib maalum za kifamilia

Mchumi: ameamua kusave bill ya umeme ili mnunue kabajaji.

Anafeki: Haumfikishi kileleni so anafake na anahisi utamshtukia akifake mchana kweupe (low self confidence)

Aibu: amekuwa na kufunzwa kuwa ngono ni aibu.

Extra sex abnormal activities (ambayo pia ni sub heading ya aibu) : ana mambo ya ajabu anafanya wakati wa kungonoka na hataki wewe uyaone na hayakubaliki kijamii na kimaadili.

Post litakuwa refu acha niishie hapa.

huna msaada kwangu.. klorokwin... styupidii
 
wa usiku wahusika zaidi kwani utaongeza billwa mchana nadhani anawaonea imani watumiaji wa solar...asiwapunguzie nguvu.halafu game raha yake usiku mkuu.mchana kazi.
Kumbe huna uhakika na unachokisema!!Haya wenye shida kakusikia natumaini kasaidika‘
 
sijawaza kuomba nioge nae.. sidhani kama atakubali
hehehe mkuu nyinyi sio "wapenzi " nyinyi ni "waheshimiwa" , siku utakayoweza kutafautisha haya maneno mawili ndio siku utajua nini cha kufanya.
 
huna msaada kwangu.. klorokwin... styupidii
Aiseee!Inawezekana anafanya hivyo kwasababu ya upeo wako mdogo!Ungekua nao mkubwa ungeweza kuona point za maana alizoonyesha huyo Klorokwini au hata kama hazikupendezi (maana unaonekana unataka visemwe vitu vya kumsifia huyo mpenzio) ungenyamaza tu badala ya kuanza kumwaga maneno yasiyo na staha kwa mtu aliyejisumbua kukusaidia mawazo!
 
Aiseee!Inawezekana anafanya hivyo kwasababu ya upeo wako mdogo!Ungekua nao mkubwa ungeweza kuona point za maana alizoonyesha huyo Klorokwini au hata kama hazikupendezi (maana unaonekana unataka visemwe vitu vya kumsifia huyo mpenzio) ungenyamaza tu badala ya kuanza kumwaga maneno yasiyo na staha kwa mtu aliyejisumbua kukusaidia mawazo!

ulianza vizuri kweli..baby girl.. sasa wapoteza muelekeo
 
Back
Top Bottom