Mapenzi: Dogo katendwa na Baba Mkwe, anahitaji msaada wa kisaikolojia zaidi kuliko Vitisho vya Polisi

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,180
85,339
Siku zote natamani sana sana nchi yetu ingekua na vitengo vya wanasihi, sio kila kitu kinahitaji polisi na kutumia nguvu. Mfaano mzuri ni huyu kijana ambaye kwa majibu wake ni kwamba Baba mkwe kavunja ndoa yake iliyodumu tangu 2012-2021. Miaka Tisa ya mahusiano si michache.
Katika kutafuta relief ameprint ujumbe wake na kuuweka kwenye bajaj, mke kaenda kutoa report polisi. Dogo kaitwa, katoka hapo kapost status, huyu anahitaji psychological support kuliko vitisho, anapitia kipindi kigumu sana.

Sasa polisi wanamtisha huyu kijana wakati wao kidogo tu yaani Polisi akigundua tu kuwa anagongewa anakimbilia silaha...huyu kijjana afanyiwe Counselling kuliko vitisho. Tutampoteza na Ryan atabaki yatima

IMG-20211122-WA0032.jpg


IMG-20211122-WA0086.jpg
 
Baba mkwe alikua sahihi kuvunja hiyo ndoa ... Kijana hana busura, heshima na hekima hata kidogo inshort kijana hajastaarabika bado.
Siku ikikutokea ndo utajua ....Kila mtu Ana maana yake ya hekima na busara yakwako inaweza kuwa kunyamaza Ila wengine mpaka kieleweke
 
Siku zote natamani sana sana nchi yetu ingekua na vitengo vya wanasihi, sio kila kitu kinahitaji polisi na kutumia nguvu. Mfaano mzuri ni huyu kijana ambaye kwa majibu wake ni kwamba Baba mkwe kavunja ndoa yake iliyodumu tangu 2012-2021. Miaka Tisa ya mahusiano si michache.
Hahahaha
 
Ila hajataja mtu
Yes hajataja ila ni kijana hana adabu mkuu na yeye ndio ana kosa sijawahi ona mtu anagombana na baba mkwe, aeleze two sides of the same coin, wamegombana why aanze kumzalilisha kwa watu, na ku post status, while watu huwa tunagombana huwa hatupostiani mitandaoni
 
Yaani wachuchu walivyo wengi hivi bado mtu anahangaika kupoteza hela na muda kuweka bango kubwa hivyo...

Mchuchu mmoja akizingua, unatafuta mchuchu mkali zaidi yake halafu unamuweka status bango kubwaaaa...
Ooghh
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom