Musoma Yetu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2016
- 2,633
- 2,297
Mapendekezo haya yangefaa kama ripoti mbili za makinikia zilipaswa kuyaongeza. Nimeona niongezee mwenyewe. 1. Anzisheni au imarisheni vitengo vya utafiti(research and development) kila wizara au mtakavyoona inafaa na watoe taarifa zao kila robo mwaka. Taarifa hizi mbili ni matunda ya tafiti. 2. Hivi vitengo havipo kabisa kwenye halmashauri wala mikoa yetu.Taarifa zingekuwa zinaanza kutoka huko. 3. Nchi zote zilizoendelea wanafanya maamuzi yao na kutekeleza kulingana na tafiti zilisemaje au zinasemaje.Tuache tabia za kufanya maamuzi ya vikao bila kuwa na tafiti. 4. Wizara zote zinaongozwa na mawaziri na makatibu wakuu wasomi mfano ma professor au madoctor! Mnashindwa nini kuishauri serikali kuimarisha au kuweka vitengo vya tafiti. Mbona huko vyuoni mlikotoka matafiti mlikuwa mnafanya, sasa huku mnashindwa nini? Nawasilisha.