Mapendekezo ya watu wa kuwakilisha CHADEMA kwenye tume ya Katiba Mpya ni haya

HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
Kutokana na CHADEMA kutangaza kupitia kwa Mnyika kuwa watu watoa mapendekezo ya akina nani watawakilisha CHADEMA kwenye tume katiba mpya, mimi napendekeza hawa.

1.Tindu Lissu-Huyu ni mtaalum wa sheria na mtetezi wa haki za binadamu. Ana ufahamu mzuri wa mambo ya sheria na katiba.

2.Prof Mwesiga Baregu-Huyu ni mtaalum mzoefu wa elimu ya siasa na vyama vya siasa. Kwa kuwa hatuwezi kutengenisha siasa na katiba basi prof Baregu atakuwa ni hazina kubwa kwenye hiyo tume.

3.Prof Safari- Huyu ni mtaalum wa sheria na siasa za Zanzibar. Atatumia uzoefu wake huo kuhakikisha masuala ya Zanzibar yana pewa kupaumbele na jinsi gani ya kuboresha Muungano wa Tanzania

Haya ndiyo mapendekezo yangu na ninyi tuone mapendekezo yenu.
 
sawa. Nilikuwa naangalia kama umemtaja DR SLAA humo ili nikushambulie vizuri.
 
Dr Slaa yeye itakuwa ni kama kumpendekeza Kikwete awe mjumbe. Si unajua kuwa watu wengi tu hapa Tanzania wanamuona Dr Slaa kama rais mbadala kwa Kikwete???
 
Mzee wa hisia kali Tundu Lisu ni Mbunge hivo hawezi kuingia humo kwa mujibu wa sheria ya marekebisho ya katiba. Hivyo vichwa viwili Kamili viingie vitani. Labda Tuongeze Malando hapo
 
Napenda kuwa mmoja wa wawakilishi toka chadema. Mimi ni mwanasheria mtaalamu wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, ni mhadhiri wa sheria hii masters progrm tumaini uni makumira college, ni mmoja wa watumishi waanzilishi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC, nimetoa mafunzo kwa wtu zaidi ya 900 katika wilaya zote za mkoa wa arusha na ninaendelea kutoa elimu kupitia radio inayofikia mikoa ya arusha, kilimanjaro, tanga, manyara, dodoma na singida kila jumamosi kwa nusu saa kupitia snrise radio ya mjini arusha, nimehamasisha na kutoa mafunzo kwa vijana, wanawake, na wajasiriamali kujua maana ya sheria hii, nilikuwa mgombea ubunge arumeru mashariki ambapo nimekuwa wa pili toka chadema, kwa sasa niko katika timu ya mgombea wetu Joshua aliechukua nafasi ya kwanza. Ni mwanamke mtaalamu na nitaleta mawzo ya wanawake katika suala hili na mawzo ya makundi mengine ya pembezoni katika jamii yetu. Naamini sifa zangu zinakidhi vigezo naomba kuungwa mkono na kupitishwa na chadema kushiriki jambo hili muhimu katika historia ya nchi yeti.
 
ISKARIOTE
 
.....................mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmlll LM l
L l ll limo ooo9kkkk mm m
 
Back
Top Bottom