Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
- Thread starter
- #21
Kwa muda mrefu tumeweka Madini na Nishati mahali pamoja kiasi kwamba ni vigumu kuzionea zikitenganishwa. Binafsi ninaamini Madini ni sekta kubwa mno kwa nchi yetu kiasi kwamba kuiweka na wizara nyingine hatuitendei haki. Nishati ni sekta kubwa na yenye kugusa watu na taasisi mbali mbali (zote) nahivyo kuiweka na sekta nyingine kubwa ni kutoitendea haki. Matatizo ya nishati na madini ambayo tumeyapata miaka hii naamini kiasi kikubwa ni kutokana na kuunganishwa kwa sekta hizi mbili na hivyo kuzifanya zikose mkazo unaostahili. Wakati umefika tuzitenganishe kama tunataka kuzisimamia vizuri.