Mapendekezo ya Muundo na Utendaji wa Baraza la Mawaziri

small mind

Senior Member
Jun 1, 2012
129
58
Ndugu wadau,

Mimi ni mtia nia wa kugombea Ubunge katika Jimbo la Kigamboni. Kwa kuwa kipindi cha Kampeni bado napenda niweke baadhi ya sera na itikadi zangu kuhusu masuala mbalimbali ambayo nitayafanyia kazi nitakapofanikiwa kuwa Mbunge.

Katika uzi huu nataka kuzungumzia mabadiliko ambayo nitayawasilisha Bungeni ili kurekebisha sheria katika namna na Muundo wa Baraza La Mawaziri.

Natambua kwamba kwa sasa Mawaziri wanateuliwa na Rais(Kwa kushirikiana na Waziri mkuu) na kwamba Rais anao uwezo wa Kuwafuta kazi mawaziri wakati wowote.Wakati huo huo Mawaziri hawa ni wabunge ambao wanao wajibu wa kibunge. Mapendekezo ambayo ninalenga kuyawakilisha bungeni mara baada ya kuwa mbunge ni kurekebisha hili eneo.

Kwanza Kabisa Nafasi ya Waziri Mkuu iwe ya Kugombea ndani ya Bunge kama ilivyo nafasi ya Spika, Kwamba baada ya Spika kuchaguliwa basi atasimamia uchaguzi wa waziri mkuu kutoka kati ya wabunge watakao kuwemo bungeni.

Baada ya kuchaguliwa waziri mkuu atapokea kutoka kwa Mheshimiwa Rais mwongozo wa idadi ya wizara ambazo ameziunda kwa kuzingatia mahitaji na mipango na kwa kuzingati orodha hio Waziri mkuu atapendekeza majina ya wabunge kuwa mawaziri na majina yao yatajadiliwa na kupitishwa na wabunge.

Rais Naye atateua Makatibu wakuu wa wizara alizopendekeza na kisha ataitisha kikao cha Baraza la mawaziri ambalo litaundwa na Makatibu wakuu pamoja na mawaziri huku RAIS akiwa ni mwenyekiti na Waziri mkuu Katibu. Katika kikao hicho maamuzi yatafanyika kwa kura,na maelekezo yatakuwa kwa makatibu wakuu katika utekelezaji.

Mawaziri watakuwa na majukumu ya kufuatilia utendaji wa Makatibu wakuu na wote walioko Chini yao kwa kuzingati mipango ya Bunge na Cabinet.

Waziri mkuu atapewa uwezo wa kuteua mbunge yeyote kuwa waziri bila kujali Chama Chake.

Ninajua hili ni wazo ambalo linahitajika kufinyagwa zaidi ila lengo ni kuhakikisha kwamba, RAIS anakuwa HURU na BUNGE linakuwa HURU. Kitendo cha RAIS kuteua wabunge kuwa mawaziri na kuwapa maelekezo kinawafanya mawaziri kuwa na double loyalty ambalo ni tatizo katika utendaji wao kwani wakiwajibika kwa wabunge basi watawasimamia makatibu wakuu kwa ukaribu ambao nao watasimamia shughuli za serikali kwa ukaribu.

Ni maoni yangu na mipango yangu nitakapochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni kuyafanyia kazi haya katika ngazi ya taifa
 
Kwa maana hiyo tu tweak katiba maana ndio mama muongozi wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom