Mapendekezo ya mpango mkakati wa kupambana na Malaria na Homa ya Dengue!

Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,373
6,756
Ninapenda kuleta kwenu mapendekezo yangu ya namna ya kupambana na uenezi wa ugonjwa wa Malaria na Homa ya Dengue.

Katika utafiti wangu nilioufanya nimebaini kuwa zaidi ya 80% ya mbu wanaoeneza magonjwa haya wanazaliwa kwenye mashimo ya maji taka (septic tanks).

Iwapo tutafanikiwa kudhibiti mazalia haya ya mbu basi kwa kiasi kikubwa tutakuwa temeweza kudhibiti kusambaa au kuenea kwa magonjwa yote yanayoenezwa na mbu.

Nini kifanyike?

Kwa kuwa Tayari tunacho kiwanda cha kuzalisha dawa za kuua wadudu wa Malaria kilichopo Kibaha mkoani Pwani, serikali ianzishe mradi wa majaribio (pilot project) kwa kuchukua wilaya au jimbo moja kujaribu iwapo mradi huu utafanikiwa.

Tunaweza kuanza mathalani na jimbo la Tabata kwa mkoa wa Dar Es Salaam ambapo serikali itatoa dawa kwa kila kaya kiasi cha lita ishirini, dawa ambayo itanyunyiziwa kwenye kila shimo moja, moja kiasi cha lita kumi kwa kila shimo (nyumba nyingi zina mashimo mawili ya maji taka).

Hii itasaidia kuua mazalia ya mbu ambao kwa kiasi kikubwa ndio waenezao magonjwa haya.

Iwapo mradi huu utafanikiwa na kuonesha mafanikio katika mradi wa majaribio, hapo sasa itakuwa ni mandatory kwa kila nyumba kumimina dawa hii kwenye mashimo yao kwa nchi nzima tukianzia na mikoa yenye high prevalence rate of Malaria.

Dawa hii itatolewa bure lakini kila nyumba itawajibika kulipia gharama angalau za Tsh elfu tano, pesa ambayo itakusanywa na serikali sambamba na kodi ya majengo…
Tukifanya zoezi hili kwa miaka mitano ijayo, Malaria inaweza kubaki historia katika nchi yetu pendwa ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom