CripWalkin' Nephew
Member
- Apr 2, 2012
- 75
- 159
Ninaomba kuwasilisha mapendekezo ya mfumo wa kodi Tanzania. Kwa kuanzia, mimi ninaishi jimbo la Ohio nchini Marekani kwa miaka takriban 20 sasa. Nimeuangalia mfumo wa Marekani wa kukusanya kodi na ninaona unaweza kuwa na faida na manufaa kwetu kama tukautengeneza kwa mahitaji yetu.
Kwanza, ili kuweza kukusanya kodi na takwimu zingine, kila raia wa Marekani lazima awe na namba ya "ustawi wa jamii" (social security number). Watoto wakizaliwa hospitalini, wafanyakazi wa ustawi wa jamii wako katika kila hospitali kuanzisha utaratibu wa kuwapatia social security numbers zao. Huwezi kuanzisha biashara, kumpeleka shule mwanao, kufungua account ya benki, kufanya kazi, na kadhalika bila kuwa nayo. Tunaweza kufanya hivyo Tanzania kwa kufuata mfumo kama huo. Social security numbers ndio zinazotumika kukusanya kodi za mapato kwa kila mwananchi. Tunaweza kuanzisha sera kuwa huwezi kupata huduma zozote serikalini kama kuanzisha biashara, kufungua account ya benki yoyote, au kutofanya huduma kama ya MPESA kama hujajisajili kupata social security number yako.
Pili, kuanzisha mfumo mpya wa kutoza kodi kutokana na wanapoishi raia. Kwa mfano tukianzia na mkoa wa Dar es salaam, tuanzishe mfumo wa vitongoji (mfano Upanga, Oyster bay, Sinza, Magomeni, Mbezi nk) na kila kitongoji kiwe na zip code yao. Kwa hiyo, anuani za makazi za raia inaweza kuwa kama hivi (43123 inakuwa ni zip code ya Upanga):-
CripWalkin' Nephew
911 Kibasila Road,
Upanga, Dar es salaam 43123
Tatu, kila kitongoji kinakuwa na serikali yao. Kwahiyo, serikali ya kitongoji (ikiongozwa na meya wao) wanakuwa wasimamizi wakuu wa mipango ya maendeleo kama shule za serikali za vitongoji vyao, polisi, vituo vya zimamoto, huduma za dharura (911), barabara, hospitali, huduma za kijamii, kuleta wawekezaji wa viwanda na biashara, nk). Watapata wapi fedha za maendeleo? Tazama kipengele cha nne.
Nne, mfumo mzima wa TRA wa kukusanya kodi ubadilishwe. Hapa ninapokaa (Pickerington, Ohio), tunatozwa kodi (na IRS - ni sawa na TRA) kutokana na kipato chako kama ifuatavyo:-
- Kodi ya serikali kuu (Federal government - ya Obama - kwa Tanzania inakuwa ni serikali ya Magufuli).
- Kodi ya jimbo ninaloishi (hapa inakuwa Ohio - kwa Tanzania inakuwa mkoa wa Dar es salaam).
- Kodi ya mji ninaoishi (hapa inakuwa Columbus. Pickerington ni kitongoji cha jiji la Columbus - kwa
Tanzania inakuwa jiji la Dar es salaam).
- Kodi ya kitongoji (hapa inakuwa ni Pickerington - kwa Tanzania inakuwa Upanga, Manzese, Sinza, nk).
- Kodi ya ustawi wa jamii (social security tax - hii ni kodi ya kukusaidia kujikimu na maisha ukifikisha
umri wa kustaafu kazi - hapa ni maka 65).
- Kodi ya matibabu ya wastaafu (Medicare/Medicaid - kusaidia wastaafu na wazee/senior citizens
kuweza kulipia gharama za matibabu).
Mfumo wa IRS wa kukusanya kodi uko kwenye kila sehemu ya biashara ama sehemu yoyote yanapopatikana au yanapoingia mapato. Kwahiyo, kila serikali kuanzia serikali kuu, ya jimbo/mkoa, ya mji, na ya kitongoji inapata fedha kutokana na kodi ya wakazi wao kuweza kuendesha mambo mbalimbali ya maendeleo. Kila kitongoji kina haki yake ya kuongoza inayoendana na matakwa ya wakazi wa kitongoji hicho. Kazi ya serikali kuu ni kutoa miongozo ya jumla, kulinda mipaka ya taifa, mifumo ya barabara za kitaifa (interstate highways), nk.
Katika kila mfumo kuna mazuri na mabaya yake. Kwenye vitongoji ambavyo wakazi wake wana vipato vikubwa (mfano - Oysterbay na Upanga), serikali za vitongoji vyao zitakuwa na uwezo zaidi kutokana na kukusanya mapato zaidi. Kwahiyo shule zao zinakuwa na fedha nyingi za kuziendesha na kwa kiwango kikubwa zitakazofanya vizuri zaidi kimasomo, polisi wao watalipwa vizuri zaidi, barabara na shughuli nyingine za kijamii zinakuwa nzuri zaidi. Kwahiyo ni kazi ya viongozi wa vitongoji vya watu wa kipato cha chini kuvutia wawekezaji ili waweze kuleta ajira zaidi katika vitongoji vyao, ambazo zitaleta mapato zaidi ya kodi. Ndio maana ukiwa unatafuta mahali pa kuishi au kununua nyumba, unaangalia ripoti zote za hiyo sehemu (zip code) kuanzia takwimu za usalama wa raia, huduma za kijamii, kodi, nk kabla hujafanya maamuzi.
Nafikiri kwa kujaribu kujifunza wanavyofanya waliofika mbali kimaendeleo na kuubadilisha kukidhi mahitaji wa jamii yetu, tunaweza kuwa na mfumo ambao utawasaidia wananchi wote. Tunaweza kuanzia na jiji la Dar es salaam na kuangalia kama utaleta mabadiliko.
Nawasilisha.