ENANTIOMER
JF-Expert Member
- Sep 22, 2014
- 1,419
- 804
Wakuu habari za usiku.
Ntumaini sisi sote tunafahamu kuhusu hili swala la elimu msingi ambayo inamtaka kila mwanafunzi kusoma kuanzia elimu ya awali mpaka kidato cha nne bila malipo (maarufu kama elimu bure). Hi elimu msingi haitaki mwanafunzi aishie njiani, bali amalize kidato cha nne na ikibidi aendelee na masomo kama akifaulu. Kiufupi hii itakua elimu ya lazima kwa kila mtanzania kama ilivyo lazima kwa elimu ya mpaka darasa la saba kwasasa.
Pamoja na kua kuna mambo memngi ya kuangaliwa ktk elimu msingi, ila tuangalie hili moja la jinsi ya kutatua tatizo la wanafunzi kuingia kidato cha kwanza bila kujua kusoma wala kuandika. Kwa kuzingatia kua, lengo la mwanafunzi kujiunga na shule ni kwa ajili ya kujifunza na sio kukua, napendekeza jambo lifuatalo.
*** Napendekeza iwekwe sheria ya kuwabana walimu wakuu wahakikishe kua asiyejua kusoma na kuandika haruhusiwi kujiunga darasa la tano hata kama alitazamia majibu na kufaulu. Tena akiruhusu mwanafunzi asiyejua kusoma na kuandika kuingia darasa la tano, basi achukuliwe hatua za kisheria na mamlaka zinazohusika. kama hajui kuosma na kuandika, akariri darasa mpaka ajue.
kama mwanafunzi akifaulu kuingia kidato cha kwanza huku hajui kusomaa wala kuandika, sheria imuwajibishe mwalimu mkuu wa shule aliyotoka kwa kosa la kumruhusu mwanfunzi huyo kuingia darasa la tano bila kujua kusoma wala kuandika.
Mwalimu mkuu asijitete kua mimi nilihamia tu ktk ile shule nikakuta huyo mwanafunzi yuko darasa la 5, 6 au 7. Ikitokea mwalimu mkuu akahamia ktk shule fulani na akakuta kuna mwanafunzi yuko darasa la 5, 6 au 7 huku hajui kusoma wala kuandika, basi amrudishe mwanafunzi huyo darasa la nne akakae huko mpaka ajue kusoma na kuandika. Tena ikibidi mwalimu wa darasa husika ( darasa la 5, 6 au 7) awajibishwe kwa kuruhusu mwanafunzi huyo kuingia ktk daarasa analolisimamia yeye (darasa la 5, 6 au 7) huku akiwa hajui kusoma wala kuandika.
Tujiulize. Tunamvusha mwanafunzi asiyejua kusoma wala kuandika kuingia darasa la tano aende kufanya nini huko wakati hata kusoma wala kuandika hajui? Mwanaaunzi anapata faida gani kwa kuingia darasa la tano huku akiwa hajui hata kusoma na kuandika?
Nahitimisha kwa kusema kua lengo la mwanafunzi kujiunga na shule ni kwa ajili ya kujifunza na sio kukua, hivyo mwanafunzi asiyejua kusoma wala kuandika akariri darasa la nne mpaka ajue kusoma na kuandika.
Yangu ni hayo tu. Kama kuna marekebisho au nyogeza, basi ni vyema ukayaweka ili yajadiliwe.
Asanteni sana.