Mapendekezo ya katiba mpya: Kipengele cha bunge kuthibiti safari za nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapendekezo ya katiba mpya: Kipengele cha bunge kuthibiti safari za nje

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Nov 30, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Safari za nje za Viongozi na Maofisa wetu zimekuwa nyingi mno, ni muhimu tukawa na kipengele maalum katika Katiba kinachofuatilia hizo safari, ninaamini sana kwamba Mikutano mingi wanayokwenda huko nje inaweza kuwakilishwa na Maofisa wa Balozi zetu zilizoko nje. I mean tumefikia kupeleka maofisa wa Serikali nje kwenye Mikutano ya Misitu I was like are you kidding me or what? Kwa misitu gani tuliyonayo Bongo? Enough!

  - Pia Viongozi na Maofisa wetu wasafiri kwenye Economic Class I mean what went wrong na hili taifa na kusafirishana kwenye Business na First Class, hivi mnaosafiri kwenye hizo Class kwa jasho la wananchi hamuoni huruma hata kidogo? We need to stop this madness, na pia marupu rupu ya Viongozi wa juu Wastaafu yapunguzwe it is just another insanity!

  - Katiba mpya irudishe power to the people, kupitia kwenye Bunge letu, na ilenge hasa kwenye Uwajibikaji, Heshima kwa Sheria na Checks and Balance kwenye Utawala wa Juu, nimesema before ninasema tena kwenye hili la Katiba Mpya CCM lazima ichukue Bullet for the Good of our Nation na hasa the Future, no other way au tuwache kabisa lakini tusidanganyane!

  MUCH RESPECT PEOPLE!

  William @....NYC, USA: Mutuz Le Baharia!
   
 2. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni wazo zuri, ila sijui kama itawezekana. Kutowaruhusu wananchi kuchangia mawazo yao imeharibu kabisa "reliability" ya hiyo katiba.
  Bungeni wachangiaji walikuwa ni wawili tu, Andrew Chenge, na mbunge mmoja nimesahau jina lake. Wabunge wengine waliochangia waliishia kuijadili Chadema.
   
 3. wasaimon

  wasaimon R I P

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena...kisingizio ni hizo semina kumbe wanaenda kuona watoto wao kwa gharama za serikali..ujinga huu ifike mahala tusema basi..mbona Raisi wa majirani zetu wa Kenya hatumsikii akitoka mara kwa mara?
   
 4. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,972
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Willy,
  Sidhani kama kuna ulazima wowote wa kuweka kifungu kwenye katiba ili kudhibiti safari za nje. Dawa nzuri ya kudhibiti huu Vasco da gama ni kurudisha nguvu ya usimamizi wa shughuli za serikali mikononi mwa wananchi kupitia kwa wawakilishi wao bungeni. Bunge linapaswa kupewa MENO kikatiba, na uwezo wa kuhoji matumizi ya serikali, BILA hofu ya kupigwa mikwala wala manyanyaso ya watawala wala vyama vya siasa. Mtu mmoja na tamaa zake za kubembea asisababishe tuharibu katiba yetu bure.
   
 5. Banzi

  Banzi Member

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mutuz le Baharia........kwa hakika umeugusa moyo wangu mno, na kwa hili nasema hata mungu aone nia yako na maombia yako. Kwa hakika kuna mambo mengi mno ya hovyo hovyo ambayo kimsingi yanapaswa kuepukika na kupunguza gharama zisizo za lazima kwa wananchi. Sitaki kuyataja hapa kwani si nia yangu ku deviate hii post...lakini hili ni NENO KUU. Huu uzururaji usio kuwa na tija unapaswa kukomeshwa maa moja na kudhibitiwa vilivyo. Balozi zetu zinakosa maana ya uwakilishi iwapo hata event zisizo tuhusu saana safari zinaandaliwa kwa mabilioni ya fedha, delegate za hovyo hovyo n.k watu wanakwenda kufanya utalii na kushangaa shangaa...what the hell is that. We must stop it now.
  Asante sana kwa ujumbe mzuri na wenye hekima za juu mno.
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wazo zuri mjomba ingawa linaweza maybe kudhibitiwa kwa kuwa na spending cap kwa ajili ya trip za nje. wakiwa hawana hela hawawezi kusafiri. lakini inakatisha tamaa kwani hata kabla ya katiba haijaandikwa tunaambiwa hata kujadili mswaada ambao wengi tunauona haufai tunaambiwa ni criminal offense kujadili kitu ambacho hatukubaliani nacho. yaani inaonyesha huko tunakokwenda kunaweza kuwa kubaya zaidi kuliko tuliko toka. its madness.
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Jamani hivi hili na lenyewe linahitaji kuweka kifungu kwenye katiba ni vitu vingapi ambavyo vimewekwa vifungu kwenye Katiba lakini still nothing has been done, halafu tunapozungumzia na kuliwasilisha hili suala kuna watu wako hapa na wazee wao wako serikalini na ndio wa kwanza kwenda kutibiwa nje na kupanda first class na kutumia hela za walipa kodi wa Tanzania.
   
 8. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #8
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Yes hili linahitaji kufungu cha Sheria, Bunge lithibiti safari za Nje ama sivyo hili taifa tutaishia kudanganyana maana safari sasa imekuwa ndio new EPA, nasikia mpaka Mawaziri siku hizi kama ni safari ya nje lazima iwe unaiunganisha nchi kama tano ndio wanakubali ambako atahudhuria mikutano isiyo na faida yoyote kwa taifa, iwepo kamati ya bunge ambayo wakirudi watatakiwa kuripoti faida ya safari yao kwa taifa, ama sivyo warudishe hela za safari walizopewa, kurudisha power kwa wananchi ni kulipa bunge nafasi kuwakilisha wananchi ndio maana tunasema Bunge lisiwe na wabunge wa bure tena, ikibidi majimbo yaongezwe lakini wote wawe wawakilishi wa wananchi.


  - Otherwise mkuu tunajadili policies sio watu, siasa za majina ya watu ndio zimetufikisha hapa tulipo tumekwama!


  William@...NYC,USA: Le Baharia!
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mawazo mazuri. Lakini mimi nadhani nchi hii inataka overhaul. Hao wabunge ambao tunataka tuwape madaraka ya kudhibiti wao wenyewe huwa wamo kwenye hizo safari. Pia hawa wabunge wetu ndio wanaotuzunguka na kujilimbikizia posho lukuki; siowaoni kama wakiaminika hawa. Kumbuka safari za nje huambatana na posho nono!! Kila kitu hapa Tanzania ni posho posho posho!! Nadhani tuanze na posho kwanza mambo mengine yatakuja tu. Kama hakuna posho nono za kwenda ughaibuni hakika nakuambia watu hawataenda. Kama unataka mpigie hesabu mtu ya kwenda kulala na kula kula tu asifanye saving utaona watu wanazikimbia safari. Utashangaa mtu anaenda kwa kutumia First Class kwenye ndege ila akifika ughaibuni analala chumba cha ku share ili atunze posho. Posho ina mengi. Mimi kila nikiona mjadala hapa nauoanisha na posho tu.
   
 10. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mkuu tumepiga kelele sana mchakato wa katiba mpya uhusishe wananchi na makundi mbali mbali kijamii lakini hili limefumbiwa macho na badala yake zimeibuka kejeli na vijembe vingi kwamba wanaohoji seem wanampoka Mkuu nguvu yake (Kikatiba)....

  Rais ni victim katika hili la safari of which kwa kipindi alichokaa madarakani kafanya safari nyingi mno,nyingi kati ya hizo zikiwa ni zile ambazo wangestahili kwenda ama mawaziri ama wawakilishi wa mawaziri kutokana na jambo linaloundiwa safari kugusa idara zao!

  Hivyo basi kwa mwendo huu hii proposal yako tuitegemee kwenye katiba ya miaka hamsini ijayo baada ya Mungu kuamua kumteua mwana mwema mwingine km Mzee wetu Nyerere (alale mahala pema peponi)

  Hili la madaraja ya usafiri ni tusi lingine ukiacha hili la wabunge kuamua kujilipa zaidi ya 150% kama posho huku wakijua walipa kodi wa nchi hii hawana uhakika na mlo wa siku moja potelea mbali malazi bora na uhakika wa matibabu!
   
 11. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni sheria inayoweza kupitishwa na bunge, ila utakuwa ni upunguwani kama itawekwa kwenye katiba. Jamani hatujui hata katiba maana yake ni nini?
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  William Malecela umeinuka na kuwa hewani JF baada ya luidanganya JF uliposema wale mapacha watatu wamefukuzwa katika kikao cha CCM ilichotanguli hiki cha juzi.
   
 13. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #13
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Katiba ni Sheria, Yes safari za Viongozi na Maofisa wa Serikali nje ya Nchi zinahitaji uthibiti wa Kisheria. Ndugu tizama huku kwa waliondelea New Jersey State Gavana wao alitumia Helikopta ya State kwenda kuhudhuria mpira wa mtoto wake Shuleni lakini aliporudi akaambiwa na kamati ya bunge la State yake kuwa kisheria amekosea hakutakiwa kutumia Helikopta ya Serikali kwenda kwenye michezo ya Mtoto, akaamriwa arudishe mara moja hela za mafuta yaliyotumika na posho ya pilot aliyempeleka na akawaomba radhi wananchi na kuapa kutorudia. Mama Kitine unakumbuka safari yake ya Canada, si ilibidi kamati ya Bunge letu kuingilia kati ili Kitine arudishe hela za wananchi! I mean Dunia nzima kuacha sisi tu Bongo ndio hakuna Sheria za Safari za Viongozi, Sasa saa ya Ukombozi imefika na Katiba mpya ndio Ukombozi wenyewe! I understand huenda tunafaidika na Safari but it has to be Stopped! - William
   
 14. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #14
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Candid Scope, heshima yako mkuu jaribu kuheshimu Mada maana hii hahihusu, HOWEVER wewe unaongelea kikao ambacho Mh. Chenge aliomba kujivua na akakataliwa mwishoni mwa kikao, Otherwise muhimu ungeanzisha Thread yake ili usiwavuruge wananchi hapa na Focus ya Katiba yao, Wachana na mimi jadili hoja Mkuu! - William
   
 15. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CCM ya leo inaweza kutoa power to the people? CCM hii ambayo inawaita wabunge wake kwenye kikao na kuwapiga mkwara kwamba jambo fulani na fulani lazima lipite??

  the bigger picture.........kama wabunge in a way wanakuwa mali ya chama, je, CHADEMA nao hawatafanya the same thing??

  Mkuu, issue hapa sio kuweka kifungu, issue ni principles za good governance zinafuatwa na serikali na kuheshimiwa na vyama?
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huwezi kuweka kipengele kama hicho kwenye katiba, bali kwenye Sheria.
  Na hata katiba iliyopo hivi sasa inaruhusu sheria kama hiyo kuwekwa nchini.
  Unajua mkuu, katiba ni mwongozo au sheria mama ambayo inaweka upeo wa sheria za nchi. Kwa mfano, kwa katiba iliyopo Tanzania sasa hivi, unaweza kumkatalia mtu nafasi ya kazi, kwa sababu ya jinsia yake. Lakini kwa nchi za wenzetu huwezi, kwa sababu katiba inakataza.
   
 17. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu, hatujaonyesha dhamira ya dhati ya kuzisimamia sheria zilizopo, ziwe ndogo au kubwa......
  ......wabunge/mawaziri wanapata posho za kukaa kikaoni na hazikatwi kodi.........sheria inasemaje?
  ......Wanatokea wajanja wachache wanakwapua mahela ya nchi yetu masikini (EPA).......hawafikishwi mahakamani, wanambiwa warudishe, na majina yao kuwa siri.

  sasa kama sheria zilizopo hatuzisimamii...........hizi sheria mpya zitafanye kazi?

  Sisemi mambo haya yasiingizwe kwenye katiba au yasitungiwe guidelines, no, nachosema ni kwamba tatizo letu ni kubwa sana.......umeyasikia ya Jairo, umeyasikia ya Luhanjo na Utoh, kweli hawa ndio viongozi wetu.......na kiongozi mkuu yupo, anaangalia tu na kuchekacheka.
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Mkuu Soby, ha! Ha! Ha! Naona tupo One page, Karibu sana! Ha! Ha! @ Mkuu Memo Tanzania ni nchi yetu wote ni Muhimu tuendelee kudai Uhuru kumbuka Historia ya Kudai Uhuru Ilianzia Egypt ambapo Nabii Musa alidai Uhuru hakupewa bure! - William
   
 19. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #19
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Memo tunataka kuanza upya ndio maana ni muhimu tukapigania Katiba mpya kwa ku-cite viroja vyao, hakuna aliyesema ni rahisi lakini hatuwezi kukata tamaa hakuna aliye-Bigger than Taifa! - William
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Le Baharia! Pamoja Mkuu
   
Loading...