Mapendekezo ya Chadema, yakitekelezwa kuchelewesha Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapendekezo ya Chadema, yakitekelezwa kuchelewesha Katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theophilius, Nov 29, 2011.

 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ukipitia kwa makini mapendekezo ya CHADEMA kwa Rais, utagundua kwamba yakitekelezwa yatapunguza ‘kasi ya ajabu’ ya kutengeneza katiba mpya, iliyoanzishwa na CCM na washirika wake na kumuongezea madaraka Rais wa jamuhuri, tofauti na madaraka aliyonayo, katika 'sheria mpya' ya mchakato wa kupata katiba mpya.


  Kwa mfano pendekezo kwamba, “Sheria ibadilishwe ili kuweka utaratibu wa kuanzishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika itakayoweza kujadiliana mustakbala wa Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa usawa.” Na kwamba: “Sheria ibadilishwe ili kuweka utaratibu wa kuitishwa kwa kura ya maoni juu ya muungano na muundo wake ” Ikiwa yatakubaliwa, utekelezaji wake utafanya mchakato mzima wa uandikaji wa katiba mpya kuchelewa, kulingana na ratiba iliyopo sasa ya CCM na washirika wake


  Vile vile mapendekezo kwa ujumla yanahoji, nafasi kubwa anayopewa rais wa zanzibar katika mchakato mzima: “Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato mzima wa Katiba Mpya” kwa hali hiyo, Rais wa jamhuri anapendekezwa, kuwa na madaraka kamili katika mambo yanayohusu, mchakato wa uandishi wa katiba mpya, tofauti na wengi wanavyodhani kwamba rais, hususani JK anatakiwa kuwekwa pembeni kabisa katika mchakato mzima.


  Cha msingi, hata hivyo, ni hoja zilizotolewa kuhusiana na masuala hayo ambayo, kwa 'akili za kawaida' za wana-CCM na wapambe wao, wasingeweza kubaini uzito wake.

  My take: Wananchi watafakari hoja hizo na ikibidi ziungwe mkono kwa njia zozote zile, maana kwa hakika watawala “ wanapima hali ya hewa” bila kujali kwamba Katiba mpya tunayoitamani inaweza kuchelewa, kutokana na kazi kubwa ya kuandaa ‘mapito’ ya katiba mpya inayokidhi haja na wala si kufanya harakaharaka na matokeo yake ikatengenezwa katiba mbaya pengine kuliko tuliyonayo sasa
   
 2. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,161
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  theophilius

  Heading yako, Maelezo (Body) yako na Conclusion (Ure take) yako zimepishana, haujaeleweka upo upande upi ??? Ila mada, hoja yako ina mshiko.
   
Loading...