mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Serikali imeamua kushusha kiwango cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) kutoka asilimia 11% mpaka asilimia 9%. Nafuu anayopata mfanyakazi ni tshs 3800 tu. Jambo la kushangaza ni kwamba Serikali imebakiza kiwango cha kutozwa kodi kuwa kile kile cha zaidi ya shilingi 170,000.
Tulitaraji kuwa kipato cha chini ya shilingi 360,000 kisingetozwa kodi na kiwango cha juu kingeongezwa mpaka kufikia zaidi ya shilingi 15 milioni. Rais mara kwa mara amekuwa akizungumza kuhusu dhamira ya kupunguza malipo makubwa wanayopata watu (“wanaoishi kama malaika kuwashusha waishi kama mashetani”).
Serikali inapaswa kurekebisha tofauti ya kipato kati ya wenye nacho na wasio nacho kwa kupitia sera za kodi. Tulitarajia Serikali ingetumia Bajeti yake ya kwanza kurekebisha tofauti hizo. ACT Wazalendo inapendekeza mfumo mbadala wa kodi ya Mapato.
Mapendekezo ya ACT Wazalendo ya Viwango vipya vya Kodi ya Mapato (PAYE)
1 Mapato ya Jumla kwa mwezi yasiyozidi Shilingi 360,000/ Asilimia sifuri (0%)
2 Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 360,000/= lakini hayazidi shilingi 720,000 Shilingi 36,000 + 11% ya kiasi kinachozidi shilingi 360,000/=
3 Mapato ya jumla yanayozidi shilingi 720,000/= lakini hayazidi shilingi 1,440,000 Shilingi 72,000 + 20% ya kiasi kinachozidi shilingi 720,000/=
4 Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 1,440,000/= lakini hayazidi shilingi 2,880,000 Shilingi 144,000 + 25% ya kiasi kinachozidi shilingi 1,440,000/=
5 Mapato ya jumla yanayozidi shilingi 2,880,000/= lakini hayazidi shilingi 15,000,000 Shilingi 288,000 + 30% ya kiasi kinachozidi shilingi 2,880,000/=
6 Mapato ya jumla yanayozidi shilingi 15,000,000/= Shilingi 3,000,000 + 40% ya kiasi kinachozidi shilingi 15,000,000