Mapendekezo: Serikali iongeze kodi kwenye vifurushi vya data

Haya ni mapendekezo yangu kwa serikali.

Tanzania ni nchi yenye gharama ndogo sana ya vifurushi vya mtandaoni kuliko nchi yoyote hapa Afrika.

GB moja ya data Tanzania unaweza kuipata kwa kuanzia dollar senti hamsini hadi dola moja(tzs 1000-tzs2000) nchi nyingine GB moja ya data iko juu ya dollar 5(zaidi ya tzs 10,000) hadi dollar 10(tzs 20,000).

Watanzania hatutumii urahisi huu wa bei ya vifurushi mtandaoni kwa uzalishaji au mambo yenye tija(wapo wachache sana) zaidi ya kujikita kwenye umbea, uzandiki, uzushi, uongo na kila kitu cha namna hiyo.

Haya mambo yote ya uzushi na umbea yamepata nafasi kwa sababu ya urahisi wa vifurushi vya data kuingia mitandaoni. Kila mtu anaweza kumudu kuingia mtandaoni kwa urahisi na akatukana au kutengeneza ushushi wa aina yoyote na akapata wafuasi wa kutosha.

Napendekeza serikali iongeze kodi kwenye gharama za vifurushi vya data, GB moja ya data iuzwe si chini ya tzs 3000 kwenda juu.

Ongeza kodi, ongeza mapato kwa maendeleo ya nchi yetu.View attachment 1210682
Ww huna Nia ya kufanya uchumi upande, ww unakereka na maoni ya watu mtandaoni, Sasa Kama unakereka kwa nn uwe unasoma moani ya watu wengine , Kama vip usiwe unaingia mitaondaoni kabisa , Kama unatumia smartphone uza nunua kitochi ili ufurahishe nafsi yako, lakin usipende kuipangia serekali vitu vya hovyo hovyo
 
Ukiangalia hapo utaona nchi za kimaskini ndio zinakimbilia kuweka bei kubwa ya data bila kuelewa dunia hii ya utandawazi data ndiyo mambo yote ktk kuleta maendeleo,elimu na teknolojia mpya
Kule malaysia kuna baadhi ya miji ya viwanda ni internet free zone,na kulikua na mpango wa kuufanya mji wote wa Kuala lumpur kuwa wifi free zone....
Mpaka sasa Malaysia wana viwanda vyao wenyewe vya electronics,magari nk,hali ya ustawi wa jamii ni mzuri ule umasikini uliokithiri hawana kila mwananchi amepewa purchasing power...kwa maana hata mwananchi wa mtogole au tandika yombo ana uwezo wa kwenda shooping mara mbili kwa juma mlimani city.....
Sasa kwa nchi masikini zisizojielewa ni rahisi kuwa na mawazo ya kimasikini namna hii ya kuifanyainternet kuwa anasa badala ya hamasa
 
Napendekeza serikali iongeze kodi kwenye gharama za vifurushi vya data, GB moja ya data iuzwe si chini ya tzs 3000 kwenda juu.

Ongeza kodi, ongeza mapato kwa maendeleo ya nchi yetu.


Nashauri wakuanzishie kodi wewe binafsi kwenye hewa unayovuta ndipo waje internet
 
Haya ni mawazo ya vijana wa like lichama likongwe, mawazo ya hovyo kabisa... Halafu wanasingizia yote haya ni shauri ya njaa
 
Maoni yako yamefika pia yamesomwa ila yamepuuzwa kwa maana yana lengo la kuturudisha kwenye ujima na sio utandawazi.
Ila naamini mkuu wew ndo wale watumishi mnasumbua sana kwenye ofisi zenu yaaani hamtaki kubadilika mmeushikilia uzamani sanaa.
 
Umbea na uzandiki sio maoni hayo.
Hata wewe Hakimu
Sidhani kama unao ubavu wa kununua vifurushi vya bei juu hata kama mnalipwa vizuri.
Kujikweza na kujifanya uko juu kuna faida gani kwa wenye uwezo wa chini.

Hapo ndio kauli yako ya, umbea na uzandiki inapokurudia
 
Moja ya mada/hoja ya kijinga na ya kipumbavu kabisa kuwahi kuisoma humu JF kwa mwaka huu 2019!
 
Tumeshafanyia kazi pendekezo lako sisi kama Vodacom Tanzania na Tigo Tanzania tunakushukuru sana.
.
Viwonder
 
Back
Top Bottom